vijana wa Arusha wanapigana kwa visu. Wanaume tunazichapa kavu na maisha yanaendelea

vijana wa Arusha wanapigana kwa visu. Wanaume tunazichapa kavu na maisha yanaendelea

Mtu atatokea tu from nowhere aanze kukushambulia bro?
Umewahi kuishi Arusha au unaisikia tu ?

Kuna waporaji wa simu wanatumia visu, wahanga wanajeruhiwa wengine wanafariki, chuo cha uhasibu hapo Njiro kuna mwanafunzi alipigwa sime kisa simu.

hapo mianzink niliwahi pita kuna dogo nilomsikia "yule anti tuliemtaiti ana bahati nimekwaruza, asingetoa simu ningemvuruga maini"
 
hii ya lini tena?? apumzike kwa amani aisee. unakufa ukiwa unajua kabisaa hapa ndo nakufaa inasikitisha sana.
 
Kwamba huko dar hampigani visu? We wapi wee? Mwanaume unakosaje kisu cha kukunja ukiswampa usiku? Maana najua mguu wa kuku huna 😁

Yule mjeshi mliyemchoma beto Kawe?? Yule jamaa ni wa Arusha?
 
Imagine una mtoto moja kisha anachomwa kisu kwenye ugomvi wa kawaida ambao ungemalizika kwa kuzichapa kavu, utajisikiaje kama baba ?

tuweke visu chini tuzichape kavu
Nenda kwanza Lugalo kawaambie
Mbona washkaji wa Kawe wana visu?
 
Bangi,
Mirungi
Shisha
K vant
Konyagi,l
Ugolo
Ndio wanaweza vijana wa arusha, kupigana hizo nguvu watoe wapi muda wote wamelewa hovyoo.. anayebisha nipo hapa daraja la nduruma aje nimpasue live🏃
Sa hapo shisha inatafuta nn?

Njoo hapa round about nikumwagie ugolo, upanick nikimbie 😁
 
Ni miendelezo wa matukio ya vijana kupigana kwa visu badala ya kuzichapa kavu.

ARUSHA ifike mahali tunapogombana na kushindwa kujizuia hasira zetu, basi zipigwe kavu, Huu mtindo wa kukimbilia kupigana visu sio kabisa, ni ushamba. Pumzika kwa amani Bennyrick Lamar (pichani kapakizwa kwenye pikipiki baada ya kupigwa kisu)

Mbaya zaidi ni hata vijana wastaarabu wanapigwa visu, mtu anajipitia zake mhuni anaanza kumletea pigo sizo kujionyesha ni mbabe, ukijitete unapigwa kisu, hata Marehemu Faza Nelly alikuwa ni mwanamziki wa huko alisifika kea ustaarab wake kuishi vizuri na watu lakini kitendo cha kutaka kusuluhisha ugomvi wa majirani akapigwa kisu na kufariki.

View attachment 2807797
Arusha Hakuna Vijana,bali kuna Wadudu.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Mtu atatokea tu from nowhere aanze kukushambulia bro?
Arusha inawezekana hiyo ipo siku nilipanda Hiace yule konda alimwambia abiria sogea naomba kukaa yule jamaa akamtukana na kumwambia toka lini konda anakaa kwenye siti yule konda alisonya tuu daah alikula ngumi za uso kama tatu hivi ila baadae walipofika Samunge waliita polisi jamaa akawekwa chini ya ulinzi Arusha watu wengi ni wagonvi hata watu wazima kabisaa...
 
Daaa watoto na vijana arusha noma sana......visu na chupa ndio zaooo
 
Umewahi kuishi Arusha au unaisikia tu ?

Kuna waporaji wa simu wanatumia visu, wahanga wanajeruhiwa wengine wanafariki, chuo cha uhasibu hapo Njiro kuna mwanafunzi alipigwa sime kisa simu.

hapo mianzink niliwahi pita kuna dogo nilomsikia "yule anti tuliemtaiti ana bahati nimekwaruza, asingetoa simu ningemvuruga maini"
Yani unaniuliza kama nimewahi kuishi nyumbani kwetu nilipozaliwa na kukulia arif?

Hao vibaka wapo kila mahali mjomba, mimi pia nilishakabwa Dar Mlalakuwa Mwenge kule, nilishakutana na vibaka Shilabela Geita.

Hakuna mahali ambapo hamna vibaka jomba acha kupotosha watu.
 
Back
Top Bottom