Vijana wa Kiislamu hawaogopi ndoa kama Wakristo

Ndoa ya kiislamu 120,000 inatosha. wakati hiyo hela ni ya mkanda na tai.


Suti shati na kiatu unafunga harusi kumi za kiislamu.

Bajeti ya harusi ya kiislamu.
1. Hina 5000
2.Ubani 1500
3.Unga ngano kg 25 kwa ajili ya mandazi.
4.Sukar. Majani ya chai
5.Kukodisha vikombe 5000
6.Pilao. Mchele kg 20
7. Nyama kg 2(huwa hawapendi sana nyama chamsing pilao)
8. Mziki 40,000
9. Makobasi 8,000
10. Kanzu tutaazima kwa shehe juma

Waislamu wanaraha kwenye kuoa.

Kule kwetu uchagan pete sherehe.Wazaz Kuona nyumban kwa mke sherehe. Wazaz Kuona nyumban kwa mume sherehe. Sendoff sherehe. Harusi sherehe. Kuvunja kamati sherehe.


Gharama ndo inafanya wakristo wanachelewa kuoa.
 
Kwa sasa jamii nyingi zinajuwa umuhimu wa elimu, kwahiyo hoja yake haina uhalisia.
Nimesema sababu namba sabini. Katika mpangilio wa umuhimu.

Halafu jamii zinajua umuhimu wa elimu lakini elimu ni gharama. Kwa hiyo watafika form 4 halafu basi.

Level ya ufikaji chuo kikuu kwenye wilaya za Lindi ,Pwani, Zanzibar bado zinazidiwa na mikoa mwingine sana
 
 
Very Interesting...

Nikikumbuka ndoa yangu ilikuwa ya gharama ndogo sana.

Kwenye jambo hili lazima nipande kizimbani bila diary kumwaga nondo za ushahidi
 
Hivi mbona wale waarabu wanaoa kwa gharama kubwa, mahari zao mh! Halafu ni waislam
 
mleta mada, vipi kuhusu divorce rate ya wanandoa waislamu?. ipo juu au chini ya wanandoa wakristo?. jibu please.
Nadhani na wakristo wangetuhusiwa kuachana pia nao divorce rate yao ingekuwa juu.

Wakristo wengi hawaachani so usitegemee divorce rate yao kuwa kubwa.

Waislamu ndio ambao wana huo utaratibu wa kupeana talaka mkuu so divorce rate yao lazima iwe juu.
 
Waislam Wana mlango wa kutokea mambo yakiwa mabaya humo ndani

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Hivi mbona wale waarabu wanaoa kwa gharama kubwa,mahari zao mh!halafu ni waislam
Mkuu mahari inategemea na jamii ama kipato.

Mtoto wa bakhresa hawezi kuoa kwa 20000 eti kwa kuwa dini imetaka mahari iwe ndogo hapana.

Mtoto wa samia hawezi kuoa kwa mahari ya laki moja au milioni.

Sisi watoto wa uswahilini hadhi yetu ni laki tano,laki saba n.k.

So mkuu waarabu wanatumbua sana wale wana pesa.
.dini iliposema mahari iwe chache maana yake mtu kama maskini asipigwe mahari kubwa,
apigwe mahari ambayo ataimudu na sio anaoa kwa mkopo kisa ukubwa wa mahari no.
 
Kasi ya kutengana na kufa kwa ndoa ni ile ile haina cha muislamu au mkristu, chagamoto za ndoa ni zile zile, isipo kua wanawake wa kiislamu wanapenda na kuheshimu sanaa ndoa zao ukilinganisha na wa kuristu
 
Marafiki zangu wengi hawaja divorce ni miaka kama minne ivi wakristo gharama tatizo zinawaangusha na process NJ ndefu sijui fungate ,sendoff hata Kwa bible havipo

Labda wakristo wa vijijini
Issue ya gharama ni maamuzi ya mtu binafsi unaweza kufunga ndoa kanisani tu ikawa inatosha bila kwenda fungate, sendoff wala ukumbi, mbona wapo wengi wamefanya simple tu.
 
Shida ndoa nyingi za Kikristo zina complications kuanzia kwenye kuoa mpaka kuachana mkichokana.
Taraka za kikristo ziko complicated za Kikatoliki ndo kabisa. Mtu anaachana na mkewe lakini eti kanisa halitambui hawezi kuoa tena wala mwanamke kuolewa akifanya hivyo hawaitambui.
Sasa mtu anaona bora asubiri subiri kwanza apate mtu ambaye anaamini ni 100% sahihi
 
Ndoa za kikristo si gharama sema ni uamuzi wa mtu binafsi. Kuna ndoa nyingi na zijua zimefungwa zile misa za saa kumi na mbili asubuhi, mbili kati ya hizo wasimamizi walikuwa wazazi wangu, wamefunga asubuhi misa ya saa 12,saa 12 na nusu washamaliza na kurudi kwenye shughuli zao.
 
Mkuu kwa mujibu wa maandiko wanandoa wakristo hakuna kuachana isipokua tu kutengana kwa sababu za uzinzi/kuchepuka tu... na hapo pamoja na kwamba mmetengana huruhusiwi kutoka na mtu mwingine au kuoa mwingine. Condition ya kuoa mwingine ni pale tu mwenzako atakapofariki, basi. Ni hatare sana upande wa christian... Na ndio mana kuna kile kiapo cha ndoa kuwa ' hadi pale kifo kitakapotutenganisha' ...
 
Huoni kama hyo sheria ni batili haiendani na maumbile ya binadamu kingine haiendani na mabadiliko ya dunia
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Nimependa hiyo no.9
Hahahaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…