Vijana wa Kiislamu hawaogopi ndoa kama Wakristo

Vijana wa Kiislamu hawaogopi ndoa kama Wakristo

Kasoro sitaku kuzijua... nataka kujua mazuri tu...

Nitatoa 2.5Million
Hapo ndo utawafanya wanyakyusa niwe mtumwa kwao,nisilalamike kidogo watasema mkorofi mwenyewe yaan hata univunje shingo watasema nimejivunja makusudi ili nikusingizie.Hapana kwa kweli toa tu laki 2
 
Wakristu ili uoe lazma uwe umejiona wewe na huyo unaetaka kumuoa u mmekomaa vyakutosha maana mkiingia mmeingia. Ila kwa Waislamu unaweza oa tu utapoona unaweza oa nna unaweza acha unapoona unaitaji kuacha(kutoa talaka)
 
Hapo ndo utawafanya wanyakyusa niwe mtumwa kwao,nisilalamike kidogo watasema mkorofi mwenyewe yaan hata univunje shingo watasema nimejivunja makusudi ili nikusingizie.Hapana kwa kweli toa tu laki 2
Laki2 pesa ya vocha tu hiyo... Hapana ndogo sana...
Million 2.5 sawa...

Kwani wewe una ukorofi...
 
Laki2 pesa ya vocha tu hiyo... Hapana ndogo sana...
Million 2.5 sawa...

Kwani wewe una ukorofi...
Sana...mkorofi sana hasa kiuchumi nikiyumba afu upande wa pili hauna msaada.Ni draaaa....nyumba utahama
 
Ukifuata mafundisho ya dini ya kiislamu bila kuwaiga wachaga na wakristo basi swala la ndoa na msiba wala halina tatizo kila kijana au mzazi wako anaweza kulimudu.

Kwa sisi tulio mijini wachaga ndio wametuletea hii tabia mbovu swala la ndoa kuambatana na uharibifu mkubwa wa pesa kwenye sherehe.
Sio kweli
 
Kwa kukusahihisha padogo waislamu mahari anataja mwanamke sio wazazi.
Ndugu yangu unanibambikia kosa kisha wataka kusahihisha..

Hakuna sehemu kwenye comment yangu nimesema kwamba mahari ataje mzazi ndugu.

Hata hivyo wazazi sasa hivi ndio wanakaa na binti kumshauri kiasi cha mahari kiwe vipi na hii pia haina ubaya kwa sababu kushauriana katika mambo inajuzu.
 
Nadhani hujafikiria Wala hujataka hata kutumia akili za kawaida kwa suala kama Hili.

Vijana wa kiislam inakuwa rahisi kwa kuwa kwanza ndoa sio gharama, lakini pia kuna option ya talaka wakishindwana.

Wakati vijana wa kikristo kwanza gharama ni kubwa ya ndoa/harusi, halafu ni hadi kifo kiwatenganishe.

Kwa hiyo inahitaji mwanaume aamue chaguo sahihi, pia ajipange kukamisha Hilo zoezi.

Na wao wanaachana/tengana ila sio kama waislamu
ndoa sio gharama mkuu gharama ni sherehe na mbwembwe zingine zisizo na maana.
 
Sidhani kama gharama ndo inachelewesha ila nachofikiria kile kipengere cha HADI KIFO ndo kinafanya Vijana wachelewe kuoa, Mtu anafikiria NIKIMUWEKA NDANI HUYU ALAFU AKIZINGUA ILIHALI NDO HADI KIFO!!!!!!
 
Nadhani hujafikiria Wala hujataka hata kutumia akili za kawaida kwa suala kama Hili.

Vijana wa kiislam inakuwa rahisi kwa kuwa kwanza ndoa sio gharama, lakini pia kuna option ya talaka wakishindwana.

Wakati vijana wa kikristo kwanza gharama ni kubwa ya ndoa/harusi, halafu ni hadi kifo kiwatenganishe.

Kwa hiyo inahitaji mwanaume aamue chaguo sahihi, pia ajipange kukamisha Hilo zoezi.

Na wao wanaachana/tengana ila sio kama waislamu
Ahsante, jibu lipo clear kabsa
 
  • Thanks
Reactions: Luv
Wakuu nimekaa nikajiuliza kwanini vijana wa Kikristo hawaoi kama wa Kiislam?

Nina maarafiki wa pande zote ndio maana nimefikia hatua ya kujiuliza kutokana na trend niliyoiona.

Marafiki zangu waislam wengi wameoa na wanaoa lakini wakristo sioni muelekeo wao kuhusu ndoa.

Je, chanzo ni nini? Mbona vijana waki-ostaz wanaoa kila kukicha na wagalatia hatuoi? Tunaogopa nini?
Kwa tamaduni ya imani ya kislam, kuna yafuatayo:

1. Dini inamuwajibisha sana mwanamke katika wajibu wake kama mke wa mtu na sio kumpa uhuru wa kuamua anachotaka kwa mujibu wa imani.

2. Kuna Talaka. Wanawake wanaogopa sana mifumo ya uwajibushaji kama talaka sababu wanajua kuwa kuna vitu huwa wanafanya ambavyo kiimani ni kosa ila kama hakuna mfumo wa kuwawajibisha wanakuwa huru kufanya wanachotaka.

3. Ndoa za kiislam ni affordable na very cheap interms of cost but very expensive in Marriage value. Wadada wa kiislam washika dini hawana utamaduni wa kutaka sherehe kubwa ni shughuli au hafla ndogo tu. Na hiyo ni sehemu ya ibada kwao.

4. Procedure za kiimani za kuoa kwa mwislam ni fupi na hazina gharama. Imagine mwanamke anaambiwa yeye ataje mahari yake. Anaweza sema mahari ni msahafu au kitu fulani very cheap.

Ngoja tu niishie hapo
 
Wakuu nimekaa nikajiuliza kwanini vijana wa Kikristo hawaoi kama wa Kiislam?

Nina maarafiki wa pande zote ndio maana nimefikia hatua ya kujiuliza kutokana na trend niliyoiona.

Marafiki zangu waislam wengi wameoa na wanaoa lakini wakristo sioni muelekeo wao kuhusu ndoa.

Je, chanzo ni nini? Mbona vijana waki-ostaz wanaoa kila kukicha na wagalatia hatuoi? Tunaogopa nini?
So what!!sasa ndoa ni ajira?inaleta tija gani kiuchumi?
Hizi mada nyingine huwa zinaonyesha akili za waafrika wa kada ya chini,badala ya kuwaza kujenga makampuni na kutengeneza ukwasi,wao wanawaza kuoa na ngono,
Bora kuleta mada vikwazo gani vinawazuia wasomi kutengeneza pesa,au si Bora tuwafundishe vijana Sanaa Ili tute geneze matajiri kama mond,
 
Back
Top Bottom