Vijana wa zamani tukutane hapa - old school

Tukirudi nyuma miaka ya 80, ambapo Tz ilingia kwenye madisco ya mchana maarufu kama Boogie, wakali wa wakati huo kama David Joseph na wimbo wake wa You Cant hide walitamba... Nani anaweza kumsahau Colonel Abrams na Trapped yake? Au wale watoto wa kwa mama(UK) na kibao chao cha I.O.U, hapa sitaki kuwataja akina C&C Music Factory wala Technotronic ..(unaweza kugoogle kwa info zaidi)

Midas Touch ya Midnight Star nayo ilitesa sana, then kuna hili kundi la Linear na kibao chao cha Sending All My Love... Kama uliwahi kusikiliza kipindi cha Mtaa wa Mangoma, Radio One (TZ) hapana shaka unaweza kuwakumbuka!

Hivi tunaweza kuwasahau kirahisi kundi la Nu Shooz? Au yule mdada wa Mantronix... Vipi kuhusu Steve V na single yake ya Dirty Cash? Au Shannon na Let the Music Play ambao muziki wao ulifanana na Show Me ya The Cover Girls... Ni kipindi ambacho Walatini walitamba sana kwenye Pop Music.

Pale Ghorofa ya saba, baada kufa kwa Maggoti Living in the Box ilikuwa ndio issue... ilikuwa sio rahisi usiku kupita bila kusikia Peope hold on ya Coldcut...

Then yakaja haya madisco ya beach, kuanzia Msasani hadi Osterbay Vijana wakikodi daladala kwenda kucheza Pump Up The Jam na Criticize ya Alexander O'Neal...

Kabla ya hapo kulikuwa na makundi ya breakdance, kila kitaa kikiwa na kundi lake, kibao kilichowazungua wengi kikienda kwa jina la Rockit kilichotengenezwa na Herbie Hancock.....
 
Haaaa haaaa umenikumbusha Safari za Beach tulikuwa na washikaji tunapenda sana Mini Bus Moja nzuri imeandikwa SCABA SCUBA. Hapo ni mwendo wa raba za kenya chini, suruali ya Kitambaa, shati nyeupe na bow tie nyeusi na glovu moja nyeupe. Kutoka Home unakamata Ikarusi UDA hadi Mbowe ndo kituo cha kwanza.

Duuh halafu kuna Ngoma ya Kiswahili "Beautiful Island of Zanzibar" ilikuwa ni balaa. lazima mtu kati wajae kwenye dancing Floor.

Ngoma zingine ni kama: Go back to my root
Holiday - Madona
Akina Colonel Abraham, David Joseph
nk nk

Si mchezooo
 
Safi sana mkuu. Tuseme wimbo huo unaoitwa "Zanzibar" ulioimbwa na Sipho "Hotstix" Mabuse na kundi lake la "Harari" siyo kwamba ni wa kiswahili japo unazungumzia visiwa vya Zanzibar. Wimbo mwingine mkali kutoka kwa Sipho "Hotstix" Mabuse uliotamba sambamba na huo wa Zanzibar unaitwa "Burn Out". Na hiyo ngoma ya "Going Back to My Roots" kutoka kundi la "Odyssey" kwa hakika ilikuwa ni moja ya ngoma kali sana kwa kipindi hicho. Pia ngoma za "Baby Won't You Take my Love" na "You Can't Hide your Love From Me" za David Joseph zilikuwa ni habari nyingine zikipigwa kwenye disco. Na hizo zilitangulia kabla ya ujio wa Colonel Abrams na ngoma zake kama "Trapped", "Speculation", na "The Truth" mwaka 1985.
 
Sijambo...

Sasa enzi hizo zile nyimbo kama......sasa nimehamia mtaa wa saba.....ile nyumba sio nyumba......imejaa mikosi eeeh........mapaka kulia lia.....
Nina hakika ulikua hujazaliwa.........
 
Kama ni kweli dada yangu basi umeniacha mbali...kama nitakuwa nilikuwa nimezaliwa basi nilikuwa kababy sana.
 
Hahahahaha bado hujatoa tongotongo? Siku hizi Dar kuna BRT na Flyover zimeanza kujengwa... ukipata nauli uje ufanye utalii wa ndani
....hahahahahaha..mi nilikuwa nawaita kiaina washamba wa mikoani wanaobanaga pua humu Wanaume wa Dar hivi sijui vile,waje nao maana Wanaume wenyewe wa Dar wanaongea sasa!
 
Kwani umeambiwa hao wote bado wapo Dar?
Au tuseme wapo Dar ndiyo,je wanaongelea nini?
Anyway nimependa sana hizo memories nilikuwa mdogo sana huwa nakumbuka collection za santuri za mzee nyumbani na mara chache sana walikuwa wananichukua tunaenda wote RTC Club Uhindini Mbeya pale.
 
....hahahahahaha..mi nilikuwa nawaita kiaina washamba wa mikoani wanaobanaga pua humu Wanaume wa Dar hivi sijui vile,waje nao maana Wanaume wenyewe wa Dar wanaongea sasa!
Vitoto bado vinamwaga mkojo kitandani vinafubaa na ushamba wa kupalilia maharage. Vinatamani kuliona japo soko la Kariakoo vinakosa nafasi.... basi ile sizitaki mbichi hizi vinajifanya kuwaua watoto wa mjini. Havijui kuishi Dar ni bahati kutoka kwa Mungu. Si kila mtu anapewa bahati hiyo.
 
Old school ilikuwa balaa, nyimbo kama Kasongo yeye nangae nangae.
 
Mi kipindi hiki nilikuwa nakaribia kumaliza A level. Disco nilikuwa naona ni ujinga kudansi miziki ya nchi zingine wakati muziki wetu ulikuwa mzuri zaidi, hivyo nilijikita kwenye magoma ya Sikinde, Msondo, Talakaka, Zembwela, na nyinginezo kipindi nikiwa likizo.
 
Back
Top Bottom