Tukirudi nyuma miaka ya 80, ambapo Tz ilingia kwenye madisco ya mchana maarufu kama Boogie, wakali wa wakati huo kama David Joseph na wimbo wake wa You Cant hide walitamba... Nani anaweza kumsahau Colonel Abrams na Trapped yake? Au wale watoto wa kwa mama(UK) na kibao chao cha I.O.U, hapa sitaki kuwataja akina C&C Music Factory wala Technotronic ..(unaweza kugoogle kwa info zaidi)
Midas Touch ya Midnight Star nayo ilitesa sana, then kuna hili kundi la Linear na kibao chao cha Sending All My Love... Kama uliwahi kusikiliza kipindi cha Mtaa wa Mangoma, Radio One (TZ) hapana shaka unaweza kuwakumbuka!
Hivi tunaweza kuwasahau kirahisi kundi la Nu Shooz? Au yule mdada wa Mantronix... Vipi kuhusu Steve V na single yake ya Dirty Cash? Au Shannon na Let the Music Play ambao muziki wao ulifanana na Show Me ya The Cover Girls... Ni kipindi ambacho Walatini walitamba sana kwenye Pop Music.
Pale Ghorofa ya saba, baada kufa kwa Maggoti Living in the Box ilikuwa ndio issue... ilikuwa sio rahisi usiku kupita bila kusikia Peope hold on ya Coldcut...
Then yakaja haya madisco ya beach, kuanzia Msasani hadi Osterbay Vijana wakikodi daladala kwenda kucheza Pump Up The Jam na Criticize ya Alexander O'Neal...
Kabla ya hapo kulikuwa na makundi ya breakdance, kila kitaa kikiwa na kundi lake, kibao kilichowazungua wengi kikienda kwa jina la Rockit kilichotengenezwa na Herbie Hancock.....