Vijana wengi hawajui siri hii: Nusu ya kipato chako ndio kiwango cha matumizi yako hayatakiwi kuzidi hapo

Vijana wengi hawajui siri hii: Nusu ya kipato chako ndio kiwango cha matumizi yako hayatakiwi kuzidi hapo

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
VIJANA WENGI HAWAJUI SIRI HII: NUSU YA KIPATO CHAKO NDIO KIWANGO CHA MATUMIZI YAKO HAYATAKIWI KUZIDI HAPO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

1. Usijesema ooh! Mtibeli bahili. Ooh! Upare umekuharibu Mtibeli. Nope!

2. Hiyo ni siri za pesa ambayo hutaambiwa na watu wengi waliofanikiwa hasa waliotokea kwenyw background ya kipato cha chini.

3. Kupitia Boom ambalo kipindi kile tunapewa 510k nilikuwa nasevu 255k na kutumia 255k.

4. Yaani Kila pesa lazima nusu nigawe kwenye Akiba nusu nyingine tumia kwa matumizi Yangu binafsi.

5. Kama unapokea milioni moja. Tafsiri yake. Kipato cha matumizi yako ni 500k full stop.

6. Kupitia 255k mpaka namaliza niliweza kununua shamba heka tano. Kupitia 255k niliweza kununua vitu vyote ndani vinavyomtosha kijana wa miaka 20-35.
Kitanda, godoro, sofa, kabati, mapazia, Feni, TV, n.k.

7. Unapoweka nusu ya pato lako kama Akiba. Unajijengea Money Discipline. Na hiyo ni moja ya nguzo katika kuwa na pesa.

8. Kwa nini nusu ya pesa unatakiwa kuiweka Akiba.
9. Mbali na sababu za kanuni za pesa lakini kuna kanuni za kifalsafa ikiwemo:

10. Nusu ni kwaajili ya matumizi ya leo. Alafu Nusu nyingine ni kwaajili ya future yako.

11. Baada ya Akiba, tayari unamalengo ya biashara gani ufanye kulingana na jamii inayokuzunguka.

12. Akiba lazima uizalishe.
13. Hela inapoongezeka isifute kanuni ulizojiwekea kuipata pesa hiyo.

14. Nusu ya pato ambalo ni akiba lengo lake ni kuongeza channel nyingine ya kipato. Chanzo au vyanzo vingine vya kipato chako.

15. Na hata uanzishe vyanzo vingine. Nusu ya mapato katika vyanzo hivyo lazima uisevu kisha nusu nyingine uitumie kwa matumizi yako.

17. Kamwe usihonge kama vijana wajinga.
Iheshimu pesa nayo itakuheshimu.

18. Hiyo pesa unayotaka kuhonga iweke akiba au iingize kwenye mtaji.
Biashara itakuhehimisha lakini hao unaowahonga watakurudisha chini au kukupa matatizo.

19. Epuka kupenda kuvaa nguo za gharama. Kama kijana suruali tano na nguo za juu Saba zinakutosha kwa mwaka mzima. Ilimradi uwe msafi na mtanashati.

20. Kuwa na nguo nyingi haiongezi chochote na popote kwenye uchumi na maisha yako ya kawaida.

21. Hauna tofauti yoyote na Sisi ambao tunanguo chache lakini chochote ambacho utataka ukipate hata sisi tunakipata.

22. Sio lazima uwe na simu ya bei ghali. Au ununue simu Kila mwaka. Ilhali pato lako kwa mwezi halifiki milioni mbili.. ni kiashiria bado kiuchumi unahitaji elimu.

23. Epuka kulala hovyohovyo na wanawake.
Wanawake wengi ni mashimo ya takataka. Kwani wengi sio wasafi. Kwamba wapo na wanaume wengi.

24. Tafuta mwanamke mmoja mwaminifu, msafi, nazungumzia asiye Malaya. Ishi naye.

25. Kanuni ya Akiba ya half half inabebwa na kanuni nyingine ya fedha inayosema hakuna pesa ndogo.

26. Kanuni ya mwisho ni Ile isemayo, usiitoe pesa hapohapo pale ambapo imeingia. Iache ikae walau Siku mbili au tatu. Ikiwezekana wiki.

27. Sio pesa hata haijaingia ushaitumia yote. Nope! Umepokea pesa. Iweke. Kisha endelea na mambo mengine. Mpaka mihemko na kiherehere chako kitakapotulia.

28. Watu wasione tofauti ukiwa na hela na usipokuwa na hela. Yaani uwe normal

Kufikia hapo sina la ziada.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mwathuuu hiyo vijana wa Sasa hawawez ni asilimia ndogo saaaana wanaoweza kufanya Ivo
Hii technology inawaaribu Kila kitakachotoka mtu anataka kununua Ili aonekane wa mjini hizo bajet atafanya lini

Ni kweli kabisa. Sio ajabu kwa sasa wanawake wengi katika level ya basic needs wanawake wa mjini wamewazidi vijana wengi.

Wanawake ni bahili sana. Yaani saana
 
Ukiweza kufanya hivyo hongera.

Kuna akina mimi ambao kipato kinaisha kabla hakijaingia mkononi na ukitulia ukipiga mahesabu unaona negative kama 500k hivi,hatari!

Unaposema tusihonge hizi huduma za kimwili ambazo ni haki ya kila mwanaume tutazitimizaje? Mbususu ni haki ya kila mwanaume, na ili uipate bila stress,mhonge huyo mtoto wa mtu ili hata ukiichakata msifuatiliane sababu ashachukua chake.

Ukitaka ule demu bila gharama basi utatumia muda mwingi kuwa romantic na mambo mengine huko.

Ungesema hata aslimia 5% basi ya kipato ndiyo tutunze tajiri.

Kwanza haya maisha kila mtu anaishi kwa mara ya kwanza hakuna mwenye uzoefu nayo
 
elimu ya fedha inasema money's value vary base on time,siamini sana kwenye kutunza akiba unatunza akiba ili iweje? kama unataka ujenge bora ukope kazini ukatwe kidogo kidogo au chukua mkopo kama umejiajiri halafu sasa pandisha mjengo toka kwenye kupangisha ingia kwako maliza mkopo wako,chukua mwingine fungua mradi mwingine ,fanya vitu kwa wakati uliopo na sio kusubiri wakati kwa kuweka kidogo kidogo
 
Mwathuuu hiyo vijana wa Sasa hawawez ni asilimia ndogo saaaana wanaoweza kufanya Ivo
Hii technology inawaaribu Kila kitakachotoka mtu anataka kununua Ili aonekane wa mjini hizo bajet atafanya lini

Tunatamani sana mkuu lakini background zetu zinatugomea kabisa check tunapotoka kwa clip hii...
 

Attachments

  • 1d6b7dab45b9423d9701684a060bf6a7.mov
    12 MB
Back
Top Bottom