Vijana wenzangu tusiogope kuoa, ndoa tamu

Vijana wenzangu tusiogope kuoa, ndoa tamu

Wakuu Ndoa ni tamu ndiyo ndoa ni tamu kwan kuna mtu anabisha kwenye hilo

Emu fikiria unaamshwa asubuhi upate cha asubuhi baada ya hapo unasindikizwa bafuni kuoga
Muda huo nguo zinapigwa pasi ukimaliza mke anakusaidia kujiandaa ukimaliza unakunywa chai yako safi
Dah baada ya hapo anakuaga kwa maneno matam na yenye kukutia moyo unapoenda kutafuta riziki
Kila baada ya masaa 2 lazima haakikishe hali yako huko, ukirudi unapokelewa vizuri na maneno ya pole na ahsante
Jaman hayo ni baadhi ya mazuri ya ndoa nawashangaa mnaogopa kuoa
Mwanamke anakupa ushauri mzuri naukiufuata lazima tu ufanikiwe. Mke ndo anakuwa wa kwanza kuufariji pale unapokuwa na stress hakika tabasamu lake tu ni tiba ya mambo mengi kwangu

Vijana wenzangu tusiogope kuoa tafuta yule unaempenda na yeye anakupenda hakika siku zote hitajutia kuoa

Namalizia ndoa tamu mke ni faraja ni chanzo cha mafanikio yako
Usiogope kuoa

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndoa yako bado ina wiki 2bila shaka ndyo maana unaleta upuuz wako hapa!! tunakupa mda tu
 
Achane kukariri maisha bhana.Kwani unaishi nae au umekaa hapo kwako kwenye kiti unaamua kuandika unachokiamini ili kumkatisha tamaa jamaa mwenye uzi.Kueni na sikio la usikivu!!!!
Hamna ndoa ya hivyo bana we😅 ingekuwa hivyo kelele zisingefika mtandaoni humu! Ndoa kongwe zote zinapumulia mashine
 
Back
Top Bottom