Wakuu Ndoa ni tamu ndiyo ndoa ni tamu kwan kuna mtu anabisha kwenye hilo
Emu fikiria unaamshwa asubuhi upate cha asubuhi baada ya hapo unasindikizwa bafuni kuoga. Muda huo nguo zinapigwa pasi ukimaliza mke anakusaidia kujiandaa ukimaliza unakunywa chai yako safi. Dah baada ya hapo anakuaga kwa maneno matam na yenye kukutia moyo unapoenda kutafuta riziki.
Kila baada ya masaa 2 lazima haakikishe hali yako huko, ukirudi unapokelewa vizuri na maneno ya pole na ahsante. Jaman hayo ni baadhi ya mazuri ya ndoa nawashangaa mnaogopa kuoa. Mwanamke anakupa ushauri mzuri naukiufuata lazima tu ufanikiwe. Mke ndo anakuwa wa kwanza kuufariji pale unapokuwa na stress hakika tabasamu lake tu ni tiba ya mambo mengi kwangu
Vijana wenzangu tusiogope kuoa tafuta yule unaempenda na yeye anakupenda hakika siku zote hitajutia kuoa
Namalizia ndoa tamu mke ni faraja ni chanzo cha mafanikio yako.
Usiogope kuoa