Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao


Ndio hivyo inatakiwa wadada wakazi wawe na mioyo yao mana kila saa inabidi asafishe.

Na kuna wale wanaopenda kuchezea maji kila saa anataka maji ya kunywa kumbe anataka ayachezee. Yaani ni kazi aisee.

Ila hatuna budi kushukuru kwa yote mana hata na sisi tulipitia huko hivyo tuwavumilia wakikua wataacha.
 
Hataki umguse mamaake ndio maana.
 
Ananiacha hoi ambavyo hataki kutaja wala kuitwa jina lake anataka kuitwa "kaka" ukimuuliza jina anasema anaitwa kaka, nikipita nae njiani afu watu wakubwa wanamuita mtoto wa 2.8 kaka huwa nacheka sana, hata akiwa hataki kula ukimuita kaka anakula........

Ana maswali mnoo (nadhani karithi kwa baba)
Kuna siku alikuta muhindi ndani akaanza kuhoji
Mama hii nini
Mimi: muhindi
Umepata wapi
Mimi: nimepewa na aunt
Aunt gani
Mimi: mama fulani
Ngoja nikamuulize, akatoka kwenda kuuliza.

Nikivaa nguo hajawahi kuiona lazma ahoji
Mama hii nini
Mimi: blauzi
Umepata wapi
Mimi: mjini
Mjini wapi...... Utadhani ka polisi
 
Hilo la kuchorwa liache mumy halikwepeki mana kama kwangu ukija utacheka chumba kilichopona ni cha kwangu tu kwa sababu hawaingii hovyo hovyo ila nyumba nzima imechorwa chorwa na chumbani kwao ndio usiseme.
Wangu nitofauti yeye huwa anachora kweny rim paper zake afu abandike ukutani ukibandua kazi ipo
 
Mimi mtoto wa Dada yangu,juzi katoka kutimiza miaka mitano.
Sasa on the date of his birthday mchana wake walikuwa wanacheza,watoto wenyewe kwa wenyewe wakapigana na yeye akashiriki kumpiga mmoja halafu akakimbilia home. Huko nyuma wenzake wakaendelea kupigana mmoja akampiga mwenzie jiwe. Sasa wakasema yeye alikuwepo mama wa mtoto alieumia akaja home anakauliza haka ka my nephew,kakaelezea sasa kakafika hiyo sehemu ambayo na yeye alimpiga mwenzie,akashindwa kusema akaanza kulia kwa nguvu halafu anasema "mama mi Nina usingizi nataka kulala...mi siwezi,kuongea tena Nina usingizi" tukajaribu kumbembeleza akagoma mpaka yule mama akasema basi kaacheni kakalale. Kesho yake Ndio akasema alimpiga lakini kidogo tu sio sana,tulicheka sana. Kana drama Yaani full utundu balaa
 
mtoto wa sister angu akisikia nyimbo ya hainaga ushemeji hata kama kalala anaamka kisha atacheza
lol,
mtoto wa sis yy akisikia kamatia chini,
kalivyo kafupi sasa hlf kanavyocheza ni vituko.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] [emoji122][emoji122][emoji122]
 
Hahahah.. Nilikumiss mama, nilizama kwenye mihangaiko.. Mtoto wetu vipi!?
Hahaaa. Hata nami nilikumiss baba. Pole pia hongera kwa kuwa umefanikiwa kuibuka hujazama moja kwa moja.

Mzima lakini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…