Viongozi wa Dini wanazungumza na Serikali kuhusu Mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na Dubai
Siasa imeingizwa makanisani leo hakuna kuzungumzia kuhusu masuala ya kidini ni siasa.

Serikali haina dini lakini hutaka kuitumia pale inapowafaa wao.

Hii yaonyesha wazi kuwa haya mambo yalipangwa kabla maana huwezi kuwaita viongozi wa dini siku chache baada ya bunge kupitisha maamuzi ya kuiachia bandari, kisha jumatatu uwaite viongozi wa dini.

!Desperate times, desperate measures".
Kumbuka Mwamposa amepokea sadaka ya Hangaya jana kupitia Mkuu wa mkoa Dar es salamu....Yote hii ni kujaribu kulainisha vyuma.
 
Wengine tumeshaanza mfungo wa maombi kwa ajili ya kuwashtaki kwa Mungu wote waliohusika kuuza bandari ya nchi yetu. Ni suala la muda tu Mungu atadhihirisha uwepo wake kwa wanaomlilia ktk haki.
 
Najiuliza kwa nn walisaini kabla ya kutoa elimu? japo anasema kuna vipengele vitarekebishwa ila siamini katika hilo

Viongozi wa dini mkitoka hapo msije kutuaminisha kile tunachoona kimekosewa tuseme kipo sawa maana kila mtu ana tekno yake tunaangalia kinachoendelea
 
Una point ya Msingi, ila jaribu kunielewa pia nilichoandika. Kuna wakati maji yakimwagika unatafuta wa kuyazoa japo unajua hayazoleki. Ila katika hili naamini kama halina Nia njema kwa Taifa halitafanikiwa. Likifanikiwa ujue faida ni kubwa koliko hasara kwa Taifa. Uwe na amani.
Mkuu unajua hakuna anayepinga uwekezaji kama wapo ni wachache. Shida ni vipengele vya uwekezaji. Wakija wakafunga mitambo hapo, mizigo ikaja kqa kiasi kikubwa halafu tukashangilia meli hazikai sana mizigo mingi lakini serikali inachopata kikawa kidogo kutakuwa na faida gani. Na mbaya mkataba ukawa hatuwezi kujitoa. Unakumbuka wakati ilipogunduliwa gas mtwara ahadi zilizotolewa na serikali leo hii ni kama hata gas haipo maana sijaona hiyo impact tuliyoahidiwa.
Uwezo hatuna kubinafsisha ni sawa laki i kwa terms nzuri. Ndio maana mimi ningependa akae na wataalam wamhoji atoe majibu si viongozi wa dini hiyo si field yao
 
Wewe agreement umeiona? Wapi?
Wasikilize wabunge wako pamoja na Waziri wako; acha kuhangaika na upotoshaji wa kisiasa ulioko kwenye mitandao
Kwa hiyo hiyo inayotembea mtandaoni ni agreement fake, Mkuu? Niweke sawa hapa ili Twende pamoja.
 
Mkuu unajua hakuna anayepinga uwekezaji kama wapo ni wachache. Shida ni vipengele vya uwekezaji. Wakija wakafunga mitambo hapo, mizigo ikaja kqa kiasi kikubwa halafu tukashangilia meli hazikai sana mizigo mingi lakini serikali inachopata kikawa kidogo kutakuwa na faida gani. Na mbaya mkataba ukawa hatuwezi kujitoa. Unakumbuka wakati ilipogunduliwa gas mtwara ahadi zilizotolewa na serikali leo hii ni kama hata gas haipo maana sijaona hiyo impact tuliyoahidiwa.
Uwezo hatuna kubinafsisha ni sawa laki i kwa terms nzuri. Ndio maana mimi ningependa akae na wataalam wamhoji atoe majibu si viongozi wa dini hiyo si field yao
Nimekuelewa, Nimekuelewa. Sote ni wamoja na dhamili yetu ni Moja. Maslahi mapana ya Taifa kwanza. Katika hao viongozi wa dini, Kuna watu wamebobea katika fani mbali mbali unazozijua wewe na usizozijua pia. Na pia wapo walio katika ngazi mbali mbali za kimaamuzi. japo wao wanataka kuwatumia kama gari la zimamoto katika hili, lakini lolote linaweza kutokea. Wasipojiridhisha hao na huu mchakato wakisema HAPANA itakuwa HAPANA kweli. Usiwadharau Wana nguvu mno hao. Kumbuka, Wakuu wote wa vyombo vya serikali, wanaingia kwenye Misikiti Yao, Makanisa Yao na Masinagogi Yao kusali na kuswali na wanawasikiliza na kuwaheshimu sana. Hao ni zaidi ya wale unaofikiri wangefaa katika hili. Neno lao Moja TU, linaweza kujenga au kubomoa nchi. Tafadhali waamini wape thamani wanaweza.
 
WANAZUONI WATOA TAMKO JUNE 2023

KUUZA LANGO LA UCHUMI WA NCHI AU KUTAFUTA WANAHISA NI USARITI MKUBWA KATIKA KUVUNJA KATIBA YA NCHI: BANDARI NI MALI ZA WATANZANIA WOTE HATUNA WANAHISA (SHAREHOLDERS) NA HATUHITAJI WANAHISA.

WARAKA WA WAZI KWA WAHESHIMIWA WABUNGE
NAKALA KWA WAHESHIMIWA VIONGOZI WA DINI
NAKALA KWA TAASISI YA MWALIMU NYERERE CHINI YA MZEE JOSEPH BUTIKU
NAKALA KWA VIONGOZI WA CCM
NAKALA KWA WASOMI WOTE NCHINI
NAKALA KWA UMMA WA WATANZANIA
NAKALA KWA WAPENDA AMANI DUNIANI KOTE

Jumuiya ya Wanazuoni nchini ambao tumekaa pamoja kutoka vyuo vikuu mbali mbali kutimiza wajibu wetu kama katiba ya Nchi inavyotaka pamoja na ya Chama Tawala iliyorisi misingi ya TANU kwamba nitajielimisha kwa uwezo wangu wote kwa manufaa ya nchi yangu na Elimu yangu ni kwa manufaa ya Taifa. Wanazuoni tunaanza kwa kutumia busara na kujenga hoja mahususi kupinga nchi yetu kuuzwa kienyeji kwa kisingizio cha mashirikiano ya Nchi yetu na Nchi za Falme ya Kiarabu. Hoja zetu ni kama ifuatavyo;
Kwanza; Bandari zetu zote ni mali za Watanzania zinazosimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hatuna ubia na mtu yoyote wala Taifa lolote. Wanazuoni baada ya kusoma kwa kina kile kinachoitwa mkataba wa kubadilisha uendeshaji wa Bandari zetu na kwa jinsi tulivyofuatilia hoja mbali mbali za wanaunga mkono na wanaopinga, Wanazuoni tunapenda kutoa tafsiri sahihi ya hicho kinachoitwa mkataba kwa lugha rahisi , Wanazuoni tumetafsiri kuwa ni kitendo cha kuuza Nchi kwa bei rahisi sana na kuingiza mwanahisa mpya kwenye umiliki wa Bandari zetu ambao utakuwa umiliki wa milele au wa muda husiokuwa na kikomo maana hata waziri ameshindwa kusema huo mkataba utakwisha lini? Tafsiri yetu inatokana na jinsi hao wanaoitwa washirika wanavyogawiwa bure Bandari zetu eti kwa kigezo wanajua kuendesha Bandari. Hata kama wanaleta mtaji bado kwa kupewa mkataba tu kwao ni pesa na watapata mikopo midogo na mikubwa huko Duniani kwa kutumia Bandari zetu. Kwa kuwa Waheshimiwa Wabunge wameamua kulisariti Taifa na kupitisha ridhio la makubaliano hayo wajue kuwa mkataba huo utalindwa na sheria za Kimataifa huwezi kuuvunja na ukifanya hivyo Nchi itaingia kwenye Vita maana kila upande wa umiliki wa Bandari utatumia jeshi kulinda haki zake za kiuchumi (economic interests). Hoja yetu ya msingi hapa kuwa tutapoteza umiliki ambao tulipewa na Mungu “Sovereign ownership of the ports”. Wanazuoni tunasikitika kwani serikali zilizotangulia zote zimewekeza sana kwenye maboresho ya Bandari zetu kwa kiwango cha juu mno kwa viwango vya Afrika. Ni ujinga (ignorance) wa kiwango cha juu sana kujilinganisha na Nchi za Falme za Kiarabu (Emirates au Dubai) ambazo zinamilikiwa na falme au koo(familia). Ni rahisi sana Mabeberu wa Kimarekani kujificha kwenye kivuli cha Falme za Kiarabu au Vivyo hivyo hata Umoja wa Ulaya ambao wanao mkataba mbovu wa EPA uliokataliwa na Afrika nao ni rahisi sana kuwa kwenye kivuli cha Falme za Kiarabu au Dubai.
Kumbuka Umoja wa Ulaya ulitumia pesa nyingi na muda wa miaka mingi kutaka moja ya masharti yao ya EPA ni kutumia Bandari zetu bila malipo yoyote as Free ports for European goods/products. Ukizingatia uchumi wa Marekani na Umoja wa Ulaya upo kwenye kipindi kigumu sana kuliko wakati wowote. Marekani na Umoja wa Ulaya wanaongezeko kubwa la umasikini, ukosefu wa Ajira na wamezidiwa na China katika uzalishaji viwandani (Manufacturing industries). Hivyo basi , sehemu pekee ya wao kupona na kushindana na China ni kupora utajiri wa Tanzania (Afrika) na kuendeleza unyonyaji ili waweze kuwatunza wazungu wenzao kwa kuwapa sera kinga (social Protection policies). Cha ajabu kubwa na ya karne Tanzania ambayo inataka kugawa Bandari zetu Bure kwa madalali wa Dubai ni moja ya Nchi Duniani ambayo haina sera kinga kwa watu wake na hasa makundi maalum (Lack of National Social Protection Policy). Ina viproject kama vile TASAF nayo inategemea pesa za wafadhili na mikopo ya Benki ya Dunia.
Lakini kwa Wazungu wa Ulaya na Wamarekani wanazo sera kinga ambazo zinalipiwa na pesa za Serikali za Walipa kodi wao na nyingine wanapora nje ya Nchi kama vile Ufaransa inavyopora west Afrika. . Na hii inawezekana tu kwa kuendelea kupora rasimali za Afrika na kupora uchumi wa Nchi zetu. Wanajua wakichukua Bandari zote za Tanzania watakuwa wanamiliki uchumi wa Nchi Karibia kumi zinazotegemea Bandari zetu kwa sababu Nchi yetu ipo kijiographia eneo la kimkakati sana na ndiyo moyo wa Nchi zote zinazotuzunguka. Ukiharibu uchumi wa Tanzania na Amani ya Tanzania umeharibu uchumi wa majirani zetu, Rejea Wosia wa Baba Taifa Mwalimu Nyerere kwenye hotuba aliyotoa SADC mwaka 1984 ikiwa sehemu ya kuaga kama Mkuu wa Nchi. Hivyo Wanazuoni tunawaomba Waheshimiwa Wabunge wetu wakatae kabisa siyo tu kubadili vipengele vya mkataba waachane kabisa kucheza na Taifa letu maana historia itawahukumu vibaya sana. Wajifunze Libya jinsi Mabeberu walivyowatumia wanasiasa na kuharibu Taifa lile. Ukiingiza Mabeberu wa kimarekani na Ulaya kwenye umiliki wa Nchi kama wanahisa wa Bandari zetu kwa mgongo wa Madalali wa Vinchi vya Falme za Kiarabu vinavyomilikiwa na kuendeshwa na familia za Kifalme ujue umeuza Nchi kabisa na Rushwa waliokupa utajuta maana watakutupa mbali na kutafuta serikali ya kulinda masilahi yao ya kiuchumi. Na hiki ndicho kitakuwa kifo cha chama Cha Mapinduzi na laana ya Waasisi na Watangulizi itatutafuna na kuwatafuna wabunge wote pamoja na spika wao. Mungu tuepushe laana hii. Ndiyo maana tunawaomba wazee wa Taifa hili kupitia Mwalimu Nyerere Foundation wajaribu kumshauri Mh. Rais aweze kupata Neema ya kuona hatari tunayoiona.Wazee mkikaa kimya Taifa letu likauzwa basi mjue nanyi historia haiwezi kuwaacha salama nyinyi na vizazi vyenu.
Hoja ya pili ya Wanazuoni ni kwamba Uchumi wa Tanzania tangia awamu zilizopita na kuchagizwa na awamu ya Tano imeweka Miundo Mbinu mikubwa sana ya Matrilioni ya Shilingi. Tumejenga reli ya Kisasa na tunamiliki wenyewe hatuna ubia, tumejenga vyanzo vya umeme ili kuweza kuendesha Treini za umeme. Tumewekeza sana kuboresha Bandari zetu kwa uwekezaji wa matrilioni ya shilingi na hatuna ubia. Tunahitaji kuendesha wenyewe Bandari na kutumia treini ya umeme kufikisha mizigo ndani ya masaa 20 kwenye Nchi zinazotuzunguka na tutaweza kupata pesa nyingi za kulipa madeni ya miundo mbinu. Ukiweka mbia yaani shareholder kwenye Bandari zetu hutaweza kucontrol mapato na matumizi ili uweze kulipa deni.
Hawa Madalali wa mabeberu wa Vinchi vya Falme za Kiarabu watapewa mgao wao yaani dividends na Tanzania itapewa dividends na tutakuwa wajinga kusaini mikataba kama iliyosainiwa na Kar Peter karne za 14 na Chifu Mangungo wa Msovero. Mikataba siyo tu ya kitapeli bali ni ya kinyonyaji maana thamani ya Bandari ni kubwa mno ni Sovereign wealth na hawa madalali wa Mabeberu watatumia bandari zetu kukopa Duniani hawaji na chochote bali pesa za kuwahonga viongozi wetu pamoja na kuwapa ahadi hewa za umiliki sehemu ya shares. Watawatupa nje kama Mobutu wa Congo zamani Zaire. Imperialists have permanent interests not permanent friends. Baada ya miaka ishirini Nchi itakuwa imeuzwa kabisa kwa Mabeberu ambao watajitanua sana na tutajiingiza kwenye mgongoro wa kiuchumi wa Kimtaifa (Geo political conflicts among imperialists powers). Tujifunze kwa Ufaransa na Nchi walizozitawala wanaendelea kuzinyonya kiuchumi. Hivyo basi tunawaomba Waheshimiwa Wabunge tusikubali kupuuza ushauri huu wa wasomi na kukubali mawazo ya kijinga ya wanaojiita darasa la saba ambao hawana uelewa wa uchumi wa Dunia na vita ya kiuchumi Duniani.

Hoja ya tatu ya Wanazuoni kwa Waheshimiwa Wabunge ni kuomba kabisa kukataa kabisa kutumika kuuza Nchi. Tunapinga hoja ya kusema kuwa wenzetu wana mitaji na technolojia hivyo tutaboresha uendeshaji siyo kweli. Hatuwezi kujilinganisha na Vinchi vinavyomilikiwa na familia za Kifalme ambavyo ni madalali wa mabeberu. Tutaboresha kwa viwango vyetu na tunaweza kuajili mtu yoyote kutoka dunia kuboresha uendeshaji. Tunaweza kuajili Mzungu, au Mhindi, au Mwarabu au Mkorea au MwaAfrika yoyote na tunaweza kununua technolojia popote duniani na kuweka mifumo ya Komputer ili kuondoa kero na Rushwa Bandarini. Mkataba wa TICS wa zamani husitumike kama kigezo siyo kweli, hata TICS hatutaki iwepo kabisa tunatakiwa kuimarisha mamlaka ya Bandari Nchni. Ni Ujinga wa kiwango cha Uprofesa au PhD kwa kudhani kuuza Nchi kwa kumpa mtu ubia ili aweze kuendesha Bandari zetu kwa niaba ni jambo zuri. Tutakuwa tumewasaliti watanzania. Waheshimiwa wabunge mkataba huo hata ukimpa GSM au mfanyabiashara mmarufu Mzee Bharesa au Jumuiya ya Wafanya biashara Nchini watafanya maboresho na utajiri utabaki hapa hapa na usalama wa Taifa utabaki pale pale. Huhitaji kuwa Profesa wa Uchumi kuona kuwa mkataba tajwa ni utapeli wa kimataifa na kuuza Nchi kienyeji ni mtu mjinga pekee anayeweza kukubali bila kupovushwa na Rushwa kubwa (grand corruption).

Hoja ya Nne kutoka kwa Wanazuoni, tunakataa Madalali wa Kiarabu wanaotumiwa na Mabeberu na wanaomiliki Vinchi vyao kupitia familia za kifalme zenye idadi ya watu ndogo na wote wananufaika na utajiri wa Nchi zao, mfano Dubai watu milioni mbili tu na wote wanatunzwa na serikali ya kifalme. Hivyo Social anthropology ya WaAfrika na WaTanzania ni tofauti na hao WaArabu kabisa kwa idadi ya watu na mambo mengine mengi ya kijamii, kisiasa, kiuchumi , kiutamaduni na kihistoria. Kugawa Bandari zetu ni sawa na kuuza Nchin yetu, hivyo tusitafute short cut. Lazima tupambane na Rushwa na tuongeze ufanisi katika Bandari zetu ambazo ni nguzo ya Uchumi wa Taifa letu.

Bunge lenye maprofesa wengi wazuri wakiwepo Prof. Kabudi, Prof. Kitila , Prof. Mkenda, Prof. Ndalichako na wengine. Halafu Bunge lenye Madaktari wa kusomea (PhD) nao ni wengi pia. Wapo Madaktari wa Binadamu (MD) nao wengi. Wapo wasomi wa aina mbali mbali wakiwemo wachumi . Hivyo sisi Wanazuoni tunaomba mkataba wa kukodisha Bandari husipitishwe kwani ni kuuza Nchi. Hawa wasomi wakikaa kimya historia itawaukumu huko mbele ya safari.

MAPENDEKEZO
Wanazuoni tunatoa mapendekezo yafuatayo kwa Waheshimiwa Wabunge pamoja na viongozi wote ambao wamepewa nakala ya wakara huu kutoka kwa wasomi wa Taifa. Tunawaomba wazee kama vile Mzee Butiku, Mzee Msekwa , Wastaafu wa vyombo vya ulinzi na Usalama na viongozi wa Chama Tawala wasikubali huu mkataba hata kama Bunge limepitisha wakatae maana Watanzania waliowengi wanapinga kabisa Nchi yao kuuzwa kwa mgongo wa mashirikiano kati ya Nchi na Nchi.
Kwanza; tunaomba kabisa Bunge lisitishe kabisa mkataba huu siyo kuboresha bali kusitisha mara moja na ktunga sheria ya kutoweka mbia yoyote kwenye Bandari zetu zote , iwe Bagamoyo au iwe yoyote. Liwepo katazo la kibunge .
Pili, tunaomba wabunge na spika wamshauri vizuri Mh. Rais kwa upole na uzalendo wa hali ya juu. Inawezekana washauri wa uchumi wa Rais hawajaliona jambo hili kwa bahati mbaya hivyo ushauri wetu utawaamusha uzingizini.

Tatu tunashauri Treini ya Umeme ambayo Mh. JPM aliacha imekamilika kipande cha DSM na kipande chas Dodoma ilikuwa imefikia asilimia 80%. Tunaomba mshauri Rais azindue Treini hiyo na kwenye bajeti ya mwaka huu tuwekeze kujenga reli mpaka Bandari . Tujenge Bandari kavu kubwa Dodoma kwa kutumia SUMA JKT kwa muda mfupi na gharama ndogo ili treini ianze kubeba mizigo na kuongeza ufanisi wa Bandari bila kuweka madalali wa Mabeberu wanaokuja kwa mgogo wa Vinchi vy Falme za Kiarabu wanavyomilikiwa na Familia. Tanzania ni Nchi yenye hadhi kubwa ndani ya Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Kimtaifa. Tanzania ni Nchi na Taifa ambalo halimilikiwi na Familia ni Nchi solid kabisa yenye kuheshimika Duniani tusipoteza mwerekeo tuungane na tujenge Nchi yetu kwa uzalendo na Umoja na tuache ubinafsi maana utaliangamiza Taifa.

Nne Wanazuoni tunashauri Waheshimiwa Wabunge wetu waweze kutafuta busara za wazee wa Taifa , Mzee Joseph Butiku , Mzee Warioba, Mzee Mangula, Wastaafu wa Jeshi , Wastaafu wa Usalama wa Taifa, Marais Wastaafu, Maprofesa Wastaafu , Wasomi wabobezi kama vile Profesa Shivji na wengine wengi. Wabunge aandaa semina huko Dodoma na Waite hawa Watanzania Wazalendo wawepe Busara zao ili mkifia maamuzi mtaweza kuliokoa Taifa.
Tano Wanazuoni tunashauri Waheshimiwa Wabunge wamuombe Mh. Rais amsimamishe kazi waziri Mbarawa kupisha uchunguzi maana wizara yake ndiyo inataka kuleta majanga ya Taifa.

Tunatanguliza Shukrani
Wenu Katika Ujenzi wa Taifa
Wanazuoni
 
Mheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, Shalom na pole kwa majukumu mazito ya kuiongoza nchi hii.
Mimi ni Mtanzania Mwl na ni Mchungaji. Nimeuona na kuusoma mara 4 mkataba wa uendeshaji wa bandari ya Dar es salama na uendelezwaji wa bandari nyingine kati ya Tanzania na kampuni ya Dp World ya Dubai.
Nianze kwa kukupongeza kwa wazo hili jema, la uwekezaji katika bandari ni wazo litakalotunufaisha sana kiuchumi . Mheshimiwa Rais, pamoja na mawazo haya mazuri, hapa nakuandikia kukuomba kusikiliza maoni ya Watanzania walio Wengi juu ya Uwekezaji Salama. Binafsi naelewa kuwa MoU yoyote Duniani ndiyo Msingi mama wa makubaliano yote yatakayofuata baadae.
Mheshimiwa Rais, katika Msingi ule kuna mapungufu ambayo baadae tukijenga juu yake, tutaumia badala ya kunufaika tutapata lawama nyingi kutoka kwa vizazi vingi vijavyo na itaandikwa kuwa Haya - yalitokea wakati Mama Samia Suluhu Hassan akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wanaoogopa kukuambia kwa upendo hawakupendi, ni Wanafiki watupu.
Mheshimiwa Rais, iwapo tutaendelea kujenga juu ya Msingi huu huko mbele kwa vitukuu, tutegemee umwagaji mkubwa wa damu utakaoletwa na vita ya ukombozi, ila bado unaweza kusimamisha mkataba huu.
MoU ndiyo MSINGI mkuu wa mkataba huu ifanyiwe kazi. Hatutapoteza chochote kwa kusita kidogo ili kusonga mbele. Ikumbukwe sasa ni wakati wa vita baridi ya dunia juu ya kushika na kumiliki njia zote ambazo ni kiini cha usafirishaji duniani. Mheshimiwa Rais na Bunge lako, fahamuni kuwa mkataba huu ukibaki hivi tutaumia sana huko mbele. Naamini mambo mawili; -kuwa Wabunge wengi hawajausoma mkataba huu na kuuelewa, Pili kama wameusoma na kuuelewa naona kuna kusudi kubwa la kukuangusha wewe kama Rais. Nasema hivi kwa sababu wenzetu wanachukulia vilivyoandikwa kwa uzito mkubwa na tukisonga mbele hivi hawatakubali marekebisho bila fidia kubwa kwakuwa watahitaji kujenga mikataba mingine juu ya hii MoU. Mheshimiwa Rais, haya ni Maisha yetu kama Watanzania, -Watoto, Wajukuu na Vitukuu wetu. Bandari ni moja kati ya malango makuu ya Nchi ya kuingia na kutoka. Tusipoweka mikakati mizuri bandari itakuwa lango la usafirishaji haramu wa binadamu, madini, bidhaa za misitu na Wanyama wetu na kadhalika. Tafadhali naomba utumie wataalamu nje ya bunge. Wewe ni MAMA nakuomba sana sana, ifanyike Comparative Study ya Mikataba ambayo Kampuni hii imeingia na nchi nyingine. Tumia Usalama wa Taifa, Tumia Wachumi, Wanasheria Wabobevu Viongozi wa dini nk. Mheshimiwa Rais hili suala sii la Chama tu ila ni la Kiserikali na kwa maslahi mapana ya Nchi yetu. Maamuzi yetu hayahitaji kufanywa kwa mihemko ya kiitikadi ya vyama au udini au vyovyote vile bali kwa utulivu mkubwa na Utaalamu huku tukimtanguliza Mungu. Bunge lisikilize, liwe na muda , lichambue maoni ya Waajiri wao yaani Watanzania. Kusikiliza mawazo mbadala sio udhaifu bali huongeza uimara na nguvu ya mawazo mbadala. Ni Imani yangu Mheshimiwa Rais wewe ni Msikivu na unayo mamlaka ya kurefusha muda zaidi.
Rev/ Mwl Nixon Sifuel Kowero. Msufini High School Moshi.

CC: Mbunge wa Jimbo la Hai kwa tiketi ya CCM
 
Back
Top Bottom