Labda huelewi, viwanda vilivyoko china vingi ni vya kutoka nchi zilizoendelea siyo mali ya CHINA. Waliposema hata viwanda vyao ataviua ni kwa misimamo yake China siyo kwamba anatechnologia au viwanda vingi hapana, wanaongelea akiendelea ku behave hivyo, mahusiano yakifa maana yake watalazimika kuondoa makampuni na viwanda vyao CHINA. Usidhani China ni taifa imara sana , madeni aliyo nayo migogora ikianza hayalipiki, labda kama anataka kujilipua asilipe madeni, lakini ataumia sana.
Kwa hiyo west walianzisha viwanda china mfano cha BYD, Xiomi, TCL, ili vikazalishe bidhaa ambazo zinauzwa bei rahisi halafu wao wenyewe wao waliozianzisha waziogope.
Viwanda vinavyotishia viwanda vya west wala wamiliki wake sio western investors vingi viko backed na serikali yenyewe ya China.
Mfano, Xiomi, BYD na kampuni nyingine ndogo ndogo zaidi ya 200 za kutengeneza EVs zinauza yale magari chini ya faida halafu serikali inatop up. Mfano kwa kila gari moja XIOMI inaloliuza inakuwa na hasara ya dola 10,000 ambayo inakuja kufidiwa na serikali ya china.
Hivyo viwanda vilivyohamishiwa china na west wka ajili ya production huwezi kuvisikia vikiwa part of this saga. Unasema hana teknolojia? Wewe Huawei kalimwa sanctions na US wakitegemea apate walau break through 2028 lakini ndani ya miaka mitatu katengeneza kitu ambacho kiliishngaza dunia.
Unasema china ana madeni? Unasahau kuwa US ndio inaongoza kwa kuwa na deni kubwa.
Migogoro? USA karibu ana migogoro na nchi kibao na sasa anazidi naye kupata shida ona hata Saudi kakataa kurudisha mkata wake wa kuuza mafuta kwa dollar. Unajua hili lina maana gani kwa uchumi wa USA? Na unajua USD kuwa pesa ya manunuzi kumeisaidia nini USA kwa miaka yote? Maana yake ni kwamba USA ilikuwa inaprint pesa nyingi tu hata kulipa madeni yake pasipo kusababisha inflation wakati nchi nyingine haziwezi. Itachukua miaka lakini safari ndio imeanza.
Narudia tena, west wanajua tishio la china ni mtanzania tu ambaye yuko mbagara anayepingana na ukweli. Ndiyo maana topic kubwa was china china china. Na kumbuka numbers don't lie, yote haya yako backed na statistics tena sio stastics tu za kwao wenyewe we tazama stastics za mauzo, na uwekezaji anaofanya china kwenye outlets za kiuchumi ndio utajua kuwa ukimwondoa USA china yuko mgongoni mwake.
Swali la kujiuliza na ambalo wao linawatisha ni kwamba, kama haka ka nchi just mwaka 1990 kalikuwa huko kamepitwa na nchi nyingi za ulaya, leo kanamfukuzia USA nini kinaenda kutokea after another 20 years? Ndio maana unaona wanahangaika kafunga speed governor.