kuna jirani yangu ameleta wadada wawili wa kumsaidia kazi hapo kwake, hawa wadada wametokea mikoa ya hukohuko aliko RC, hawa wadada wamemaliza darasa la saba mwaka jana na juzi. Wote wamekuja hawana chupi hata moja...anawauliza hamvai chupi kwanini wanamwambia hawana wala hawajawahi nunuliwa chupi na wazazi wao, hawajui matumizi ya chupi..wao ni magauni tu na sketi blauzi. RC Mtaka anajua watanzania wengi tulivyo na maisha magumu, anawaambia wananchi wake kuliko wakakaa nyumbani wakaisubiri uniform ambayo haijulikani ni lini mzazi atapata hela ya kuinunua bora waendelee kwenda shule wakati mzazi na watu wengine wenye huruma wakisubiriwa kumsaidia mtoto apate uniform awe sawa na wanafunzi wenzake. Mtaka yupo sahihi sana alafu nampenda sana tangu nianze kumfuatilia utendaji wake kwakweli nafarijika sana. Sijui nimeeleweka maana sina kipaji cha kujieleza!😕