Lazima niseme. Nguvu kubwa inafanywa na viongozi wetu wa CCM Taifa ambao pia ni viongozi serikalini kupata 'uungwaji mkono' na Maaskofu wa Kanisa Katoliki. Ni maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Kuanzia Mwenyekiti/Rais hadi viongozi wengine waandamizi wamekuwa 'busy' na kutafuta kukubalika na wakatoliki.
Pamoja na ukweli kuwa ili ushindi upatikane na utulivu wa kiuongozi utamalaki lazima ukubalike na TEC, sasa imekuwa 'too much'. Makada wabobezi na waandamizi (hasa tulio wakatoliki) tunatumwa bila kusemwa kwa Kardinali, Maaskofu, Mapadre na wengineo ili kusaka kukubalika kwa viongozi wetu.
Amini nawaambia viongozi wangu wa kichama na kiserikali, TEC hawatashawishika kirahisi.
Hawatasahaulishwa msimamo na Tamko lao juu ya mkataba tata wa DP World. Hawatalaghaiwa kwa ahadi za kifedha; kupokelewa uwanjani au kupewa kanzu. TEC bado wanalo la bandari na wamejipanga kuusimamia msimamo wao.
Ili CCM tujisafishe mbele ya TEC, Tamko lao liheshimiwe. Kupigana vikumbo kujisogeza kwao hakutasaidia chochote. TEC imesheheni waelewa wa mambo zaidi ya wanasiasa wa zamani na wa sasa. Si wepesi kuyumbishwa kwa ahadi zisizo na kadi; michngo ya michongo na zawadi maridadi.
CCM tumeshaanza kampeni, wenzetu vipi?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
Na isiwe na hao TEC pekee, CCM hii na viongozi wake wanatakiwa kukataliwa na kila mTanzania mwenye mapenzi mema na nchi hii.
Uongozi huu na serikali zake ni kundi linaloendeshwa na genge hatari sana. Hawa wakipewa awamu yao ya uongozi wataitumbukiza nchi nzima katika majanga yasiyoelezeka.
Mifano ipo wazi, hata wakijitahidi kuifunika na kusahaulisha watu.
Kule kushika madaraka tu toka kwa mtu waliyekuwa wasaidizi kwake, huku wakiwa wamejivika joho la kondoo waonekane wapo pamoja na kiongozi huyo, kule kushika tu madaraka, wakaanza kukana kila kitu kilichofanywa na uongozi ule ule waliokuwa sehemu yake. Sasa mara hii wanataka tena kujivisha joho la kondoo watu wasahau maovu yote yaliyokwishafanyika chini ya uongozi wao? Ufisadi umekuwa ni kama jadi kwao. Hawana wanalojua kuhusu mwelekeo wa nchi inakokwenda. Wanadhani watu wenye akili hawaoni haya maovu yote yaliyofanyika kwa muda mfupi sana chini ya utawala wao?
Hawaoni hata aibu, kwenda kwa watu hao hao TEC, waliokataa kunajisiwa kwa nchi hii; wao wanadhani hilo lililkuwa jambo dogo?
Wamejitokeza mbele na kueleza hiyo DP World na IGA yake kwa nini ilikuwa vile. Wameomba msamaha kwa makosa (?) waliyotaka kulifanyia taifa hili?
Wanataka sasa waungwe mkono na hao hao TEC waliowatapisha hujuma waliyopanga kuifanyia nchi hii ili iweje? Kwamba wakishasimikwa madarakani waendelee na mipango yao miovu?
Hawa watu washukuru tu kwamba nchi hii ni ya watu watulivu sana, vinginevyo matendo yao yangekuwa yametosha kabisa kuwatupilia mbali, na baadhi yao kuwekwa magerezani.