Viongozi wangu wa CCM inatosha sasa, TEC hawatatuelewa hadi tueleweke!

Inaonekana huyo kijana hamfahamu Mzee Tupa Tupa
 
Umazungumza utumbo

Benki ya Mkombozi inafanya kazi za kibenki kwa,mujibu wa sheria na inasimamiwa na Benki kuu . Benki hiyo haikufanya kosa lolote kupokea, pesa zilizowekwa na mteja wake na ilichukua hatua zote ikiwemo kuitaarifu TRA.

Mkombozi haiwezi kufutwa hata zje nani mradi sheria zinafuatwa. Kanisa kwanza halikupokea fungu kama unavyolopoka. Pili yule askofu alipewa pesa na muumini kama matoleo na si kazi ya anayepewa pesa kuhoji uhalali wa pesa inayotolewa sadaka . Wewe hapo unapotoa sadaka huwa unatoa maelezo ya hizo hela umepata wapi.

Tena huyo aliyetoa pesa ni zake kwa sababu aliuza hisa zake kihalali na alikuwa anatambulika Brella kuwa anamiliki hisa hizo na hakuna mahakama yeyote inayoweza ku.mtia hatiani.

Fanya analysis kidogo kabla hujakurupuka kuposti.
 
Mi naona mnaongea sana.Muhimu ni hili TEC inaundwa na watanzania,TEC ni mdau muhimu wa marndeleo ya nchi hivyo viongozi kuwa karibu na TEC sio kujikomba Bali ni kuwa karibu na mdau,TEC kuwa karibu na serikali au viongozi ndio wajibu wake kwa ndio wachunga kondoo.Huwezi mwacha kondoo wako ajichunge.Hivyo linapoinuka jambo na kutofautiana maono haimanishi kanisa linajitenga au kushawishi watu waichukie serikali ni wajibu wake kuwatia moyo viongozi na kuwakemea kwa kuwa wakati huo husema kwa niaba ya waamini na wasio waamini.
 
TEC haiwezi kutaka CCM ishindwe uchaguzi hata mara moja !!
 
Benki ilitumika kutakatisha pesa za wizi hilo hawawezi kulikuepa hamna sadaka ya 100m huo ni wizi, nyie chokozeni serikali na TEC yenu isio kua na mchango wote katika uchumi wetu, mtaliona la mtema kuni......
 
Mmmh
Mmmh... nadhan huna Nia njema na baadhi ya watu Mashuhuri...Mkombozi haiwezi kufungwa..na ikifungwa hiyo ndio watajua hawajui... Serikali ni watu na watu wenyewe sasa
 
🀣🀣🀣
Limebarikiwa au ndo ivoivo tu.....?

Nitajuaje ,kwani nimelitoa Mimi?
Hata yusuph walimpelekea mzee wake yakobo kanzu yake iliyokuwa na damu ,akapapasa akasema ni kanzu ya mwanangu yusuph,hapo mzee yakobo alikuwa mzee kwa upofu,akamlilia mwanae yusuph mwaka mzima ,akaomboleza🀣Kumbe mwanae yusuph alikuwa kauzwa na ndugu zake kwa wafanyabiashara wamidiani,walioenda kumwuza yusuph utumwani Misri,ambapo baadae yusuph alikuja kuwa waziri mkuu wa Misri πŸ™
 
Isimamie na Wala hakuna mtu amekataza wao kusimamia na nakereka na kujipendekeza Kwa viongozi wa Serikali.

Serikali nayo inatakiwa kusimamia na inachokiamini,hii Nchi haiongizwi na TEC
Inaongozwa na majizi ya kura.
 
Kweli wewe akili yako haijui kupambanua mambo! Ngoja nikusaidie........
Kwanza ujue walio mshauri Samia kwenda Kwa Maaskofu ndio hao hao state....
Pili, Bank ya mkombozi katika Saka like ilitumika kama kakapu kinavyo tumika kubeba matunda sokoni. Fedha zile ni za mtu mwenye akaunti halali pale na akataka fedha zake zipitie kwenye akaunti Ile. Lakini pia lazima ujue Bank kuu walijulushwa kabla muamala ule haijatoka!!
 
Mkuu mpaka ww umemind , ujue kwenye DP World kuna kitu hakiko sawa,
 
Viongozi kuwa na madhehebu Yao ni sawa ila msimamo wa madhehebu Yao haupaswi kuwa msimamo wa Nchi.

Ukiwa na madaraka kwenye Nchi hipaswi kuleta mambo ya madhehebu yenu.

Upuuzi wa hivi ukome maana unaweza kuja kuleta shida baadae
Mazeli anatafuta ungwaji mkono Kwa nguvu Sana,
 
Umeandika chuki zako kwa Wakatoliki, unataka chuki iwe hoja, usipoukubali ukweli haiwezi kushughulikia changamoto
 
Na isiwe na hao TEC pekee, CCM hii na viongozi wake wanatakiwa kukataliwa na kila mTanzania mwenye mapenzi mema na nchi hii.

Uongozi huu na serikali zake ni kundi linaloendeshwa na genge hatari sana. Hawa wakipewa awamu yao ya uongozi wataitumbukiza nchi nzima katika majanga yasiyoelezeka.

Mifano ipo wazi, hata wakijitahidi kuifunika na kusahaulisha watu.
Kule kushika madaraka tu toka kwa mtu waliyekuwa wasaidizi kwake, huku wakiwa wamejivika joho la kondoo waonekane wapo pamoja na kiongozi huyo, kule kushika tu madaraka, wakaanza kukana kila kitu kilichofanywa na uongozi ule ule waliokuwa sehemu yake. Sasa mara hii wanataka tena kujivisha joho la kondoo watu wasahau maovu yote yaliyokwishafanyika chini ya uongozi wao? Ufisadi umekuwa ni kama jadi kwao. Hawana wanalojua kuhusu mwelekeo wa nchi inakokwenda. Wanadhani watu wenye akili hawaoni haya maovu yote yaliyofanyika kwa muda mfupi sana chini ya utawala wao?

Hawaoni hata aibu, kwenda kwa watu hao hao TEC, waliokataa kunajisiwa kwa nchi hii; wao wanadhani hilo lililkuwa jambo dogo?
Wamejitokeza mbele na kueleza hiyo DP World na IGA yake kwa nini ilikuwa vile. Wameomba msamaha kwa makosa (?) waliyotaka kulifanyia taifa hili?

Wanataka sasa waungwe mkono na hao hao TEC waliowatapisha hujuma waliyopanga kuifanyia nchi hii ili iweje? Kwamba wakishasimikwa madarakani waendelee na mipango yao miovu?

Hawa watu washukuru tu kwamba nchi hii ni ya watu watulivu sana, vinginevyo matendo yao yangekuwa yametosha kabisa kuwatupilia mbali, na baadhi yao kuwekwa magerezani.
 
Tuliza povu mzee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…