Visa na Mikasa vya kusaka kwangu Utajiri toka Kigoma mpaka Kongo

Visa na Mikasa vya kusaka kwangu Utajiri toka Kigoma mpaka Kongo

Mamba anameza maji tu vingine lazima avitafune tafune kwanza au avipukutishe viwe vidogo aweze kuvimeza... so kama ni Mtoto lazima amvunje kichwa kwa kukibastisha... hapo Chizi kweli Maalifa sema hadithi njoo uongo njoo utamu kolea
Usiishi kwa kukariri ndugu, huwezi kuwa mjuvi wa kila kitu vitu vingine uliza ufahamishwe. Walioishi Mwanza na maeneo yenye ushirikina wa Mamba, hili wala sio la ajabu.
 
Ujiji wanapenda sana ushirikina ndio maana hamna maendeleo watu wanaogopa kujenga nyumba nzuri kisa watarogwa
Ndio maisha ya vijijini kiujumla mkuu, hata kama unauwezo kiuchumi utajitahidi uishi kama wengine kijijini kwa sababu za 'kiusalama'

Nilishangaa kijiji flani kanda ya ziwa eti hawanunui mboga zenye hadhi kama nyama(zinaozea buchani) na samaki wakubwa hawanunuliwi.. wao ni mwendo wa furu tu.. wanadai hawataki kufatiliwa na 'wajuvi'
 
PART II

Tukiwa na wasiwasi hasa mimi na moyo ukidunda kwa kasi. Ahmed alikuwa hana wasiwasi kabisa.mara nyingi ndo alikuwa akitusemesha kila ambapo tulikuwa kimya.

Yule mzee alichora chini kutuzunguka akamwaga unga flani uliokuwa kwenye kibuyu. Akatoka akituacha hapo akaingia kichakani.

Tukiwa pale tulianza kuona mambo ya hovyo hovyo. Kule porini hatukusikia sauti za watu toka mwanzo zaidi ya wadudu wa usiku. Lakini mara tukaona mianga ya moto hewani.

Tena unaona kama watu wanakimbizana hewani wameshika mienge. Cha kushangaza hakuna mtu unayemwona. Ila unaona mioto inakimbia na kukimbizana. Kisha sauti zikaanza sikika kama za fisi wakicheka na kukimbizana kwenye vichaka.tumekaa pale tunatetemeka sana. Baadaye alirudi yule mzee.akaongea maneno kadhaa akawa kama ndo anaingia kwenye lile duara.

Alirudi na nyama kama swala au digidigi.akatupa tukala. Akatoa masizi akatupaka usoni na kutupa maji flani machungu tunywe.

Nlitaka kusita sababu nlisikia harufu kali kiasi.nlipoona wenzangu wamekunywa huku wakifinya macho kwa uchungu nami nikanywa.

Akatuambia tuvue mashati.tukavua akatupaka dawa. Akatuambia tuvue nguo za chini. Mwishowe tukawa watupu.

Hakuna aliyejali sababu palikuwa na giza.akatuchanja kwenye paji.mabegani,kitovuni na kwenye nyayo. Kisha viganjani.

Halafu akawasha moto mdogo tu kuna dawa akawa anachoma. Ni majani ambayo alikuja nayo.kisha akaanza kutusemesha kwa majina yetu akiongea maneno hatuyaelewi.

Baada ya hapo akatoa usinga na kuanza kutupiga nao kichwani,kifuani na miguuni. Kisha akaanza kutuambia anatupeleka kwa mwenye utajiri.

Kila mtu atapata maelezo huko huko ila tusingatie kuwa jasiri kama kweli tunataka utajiri.

Akatusogeza mbele kwenye mti mkubwa sana.pale chini tulikuta vibuyu na nyungo,vyungu vingi vimevunjwa porini sana lakini hapana majani kabisa.

Akaongea maneno flani ule mti ukavunguka sikuona kitu mpaka nliposhtuka nimelala sehemu kuna upepo mzuri chini ya mti.

Kule ndani kulikuwa na mji kabisa kama mji ukiwa na viumbe vingi na watu wapo busy sana.wengine wana kichwa cha mbwa kiwili wili cha mtu.wengine kichwa cha ng'ombe kiwiliwili cha mtu.

Na wengine binadamu kama sisi tu. Pembeni yangu alikuwepo mzee wa wastani tu. Akanambia niende kwenye beseni lililokuwa mbele yangu. Akanipa mkuki. Nikachome mkuki kwenye lile beseni.

Nlichukua mkuki na kusogea kwenye beseni.nikachungulia kwenye maji.nikiwa nataka kuchoma ghafla nikaona sura ya mama yangu akinitizama kwa huruma sana.nlisita.nikatizama pembeni kisha nikarudi tena.nikakuta bado naona sura ya mama.nikatupa mkuki na kukimbia kurudi chini ya ule mti.nikiwa nakimbia sikuangalia chini nikajikwaa na kupoteza fahamu.

Nlikuja shtuka napigwa upepo mkali sana nje huku yule mzee amekaa pembeni Abdul na Hemed pia wapo pembeni.

Yule mzee alinitizama.akatikisa kichwa.nlitaka kuzungumza akanishika mdomo nisizungumze kitu.

Ahmed alikuwa amekamata mfuko wa ngozi huku anatetemeka jasho linamtomka ingawa kuna badili usiku ule.

Abdul na mimi tulikuwa hatuna kitu mkononi.tukaanza kurudi mzee akituongoza....tulitembea na safari hii safari haikuwa ndefu sana tukajikuta tumefika kwenye nyumba yake.

Tukaambiwa tukaoge. Ila Ahmed akawa amebakizwa ndani.mimi na mwenzangu kwa zamu tukaenda oga.

Baadaye ahmed naye akaenda. Tukarudi tukaambiwa tulale.tulilala mpaka saa saba mchana ndipo tulikuja hamshwa.

Tumeamka.akatupaka tena dawa na kututaka tusizungumzie mambo yaliyotokea huko mpaka tukivuka ziwa.

Ahmed sasa alikuwa yupo ok. Jasho halimtoki tena na kutetemeka hakupo.ila ameshikilia fuko lake la ngozi.yule mzee akamwambia akanunue mzuri huko mbeleni.anunue na nguo mbili tatu aweke mle ndani.

Wote tulikuwa na hamu ya kusimuliana nini kimetukuta.pale nyumbani mzee alituambia tusiondoke muda ule.tusubiri kama tulivyokuja ndo tuondoke ili wenye mji wajue ndo sisi ambao walitukaribisha.

Basi tulikaa kama mpaka saa mbili hivi tulikuja vamiwa na kundi kubwa la fisi.fisi walikuwa wengi wanazunguka ile sehemu wakichimba chini na kukenua meno.

Tuliogopa sana. Yule mzee aliingia kwenye chumba chake cha duara. Kilichokuwa mashariki mwa eneo lile.alikaa baada ya muda alitoka mnyama mkubwa kama simba akaanza kimbia akikizunguka lile eneo akinguruma sana na kukwarua chini.alifanya hivi huku wale fisi nao wakipiga kelele na baadaye wakawa wanapunguza kelele.

Mwisho wakakaa wakitizamana.sisi tupo ndani tunaangalie kupitia mlango mdogo na dirisha.

Baada ya muda yule mnyama kama simba alirudi kwenye kile chumba wale fisi waliondoka. Walikuwa kama sita au saba hivi.

Zikasikika kelele mle ndani kwenye kile kijumba kisha kukawa kimya.akarudi mzee akiwa amechoka sana.

Akatwambia mimi na abdul tulipaswa kuliwa siku ile.na kama tungeondoka ile jioni tungevamiwa na fisi na kuuawa isipokuwa ahmed.sisi hatukutimiza masharti hivyo hatukufaa kurudi tena kigoma.amepambana sana kututetea. Na ni vile tu anaheshimika na ana nguvu sana.

Akasimulia jinsi waasi na serikali zinavyokuja kwake kutafuta dawa.akazungumzia mpaka viongozi wakubwa kabisa serikalini waliokuwa wakija kwake.

Usiku sana akatupa dawa na kutuogeshea nyingine akatuambia tuondoke.

This time hatukuwa na maneno mengi njiani.tulitembea kimya kimya kila mtu akiwaza yake.ila sana sana kila mmoja alitamani kusikia toka kwa mwenzake. Nasi wawili tulitaka kujua ahmed amebeba nini....

.......................
Nitaendelea.
 
Ndio maisha ya vijijini kiujumla mkuu, hata kama unauwezo kiuchumi utajitahidi uishi kama wengine kijijini kwa sababu za 'kiusalama'

Nilishangaa kijiji flani kanda ya ziwa eti hawanunui mboga zenye hadhi kama nyama(zinaozea buchani) na samaki wakubwa hawanunuliwi.. wao ni mwendo wa furu tu.. wanadai hawataki kufatiliwa na 'wajuvi'
Ujiji kumezidi vijumba vibovu wazee wakomna kanzu safi ukifika kigoma lazima uonywe usitembee na wanawake wa huko
 
Kwahiyo ulimezwa na mamba alaf ukatemwa?
1611422841812.jpg
 
Back
Top Bottom