Visa vya Uchawi na Ushirikina Mkoani Kigoma Mwisho wa Reli

Kigoma Visa vya Uchawi na Ushirikina.

Kigoma ni moja ya Mikoa ambayo inasifika kwa Uchawi nchini Tanzania. Huu mkoa kiasili una watu wachapa kazi sana. Si wazembe ukilinganisha na mikoa mingine yenye ushirikina kama Tanga,Pwani au Zanzibar.

Kigoma maeneo ambayo yanasifika sana kwa Uchawi ni Mwandiga, Ujiji,Mwamgongo n.k

Hapo Mwamgongo ni hatari sana karibu na Mbuga ya Gombe. Kunasifika na moja ya visa vya uchawi ni kimoja ambacho kilitokea mwaka 2020 ni kifo cha Diwani mmoja ambaye inasemekana alichukua Mke wa mtu.

Huyu Diwani ambaye allhamdulilah alikuwa na vijicent ilitokea akawa anatembea na mke wa raia mmoja kijijini hapo.

Yule bwana Raia alipata taarifa. Akanyamaza. Diwani akafikia hatua akaona aoe kabisa mke wa jamaa. Na mke akadai talaka ili akaolewe na Diwani.

Jamaa alimfuata Diwani na kumwambia kwa upole tu kuwa "Mheshimiwa najua unatembea na mke wangu, tafadhali usimwoe maana mimi ntapata shida kulea watoto hawa 6 nlio nao na nina mke mwingine. Uwe na uhusiano naye lakini usimuoe"

Diwani alijibu kwa jeuri tu kuwa "mkeo ndiye anayenilazimisha mzuie yeye siyo mimi"

Jamaa akamenda mpaka kwa viongozi wengine wa kijijini pale akitaka wakamsihi Diwani asimwoe mkewe. Diwani akakaza.

Mpaka jamaa akaenda kwa Rafiki mkubwa wa Diwani kumwomba amsihi rafiki yake asimwoe mkewe yeye atapata shida na watoto. Diwani akamtolea nje jamaa.

Basi jamaa akanyamaza. Siku moja Diwani akakutana na Jamaa Mitaa flani kuna Soko. Diwani akaanza mshambulia jamaa kwa maneno kuwa "nasikia unataka niroga..

Huniwezi,mimi mpaka kufika kuwa Diwani nmetoka mbali sana..." Akaendelea mbele na kumwambia haya nakupa mate na nyayo hii chukua." Akatema mate... Jamaa alimwambia tu Diwani "huo uchawi wa kuchukua mate na nyayo ni mdogo sana,wa watu ambao ni underdog/amateur"

Akaondoka zake. Baada ya siku chache tu Diwani akaanza kuumwa sukari ikapanda mara akaanguka ndo basi tena. Akafa.

Akazikwa. Baada ya siku chache wanafamilia yake wakawa wanamwona Diwani anakuja anagonga pale kwao kuwa afunguliwe mlango anateswa sana.

Diwani alikuwa amevaa pensi chafu.anagonga dirishani akisema anachapwa sana viboko. Afunguliwe.

Mke na watoto wakawa nao wanajawa woga.

Hili tukio lilitokea Mkoani Kigoma mwisho wa Reli.

Na watu wa Kigoma tofauti na Mikoa ya Pwani. Pwani mchawi wako mnaweza mkawa mnacheka naye na kula naye huku anakuroga.

Kigoma ukikorofishana na mtu anakwambia kabisa bila kuuma uma maneno "nitakuroga" hata hatumii sauti ya vitisho. Anakuambia kwa upole tu akikuahidi kuwa kweli atakuroga mbele za watu wengine.na anaenda kukuroga kweli.

Hiki ni moja ya kisa cha mambo ya Uchawi Kigoma.nitaleta Visa vingine vya Uchawi na Ushirikina Kigoma.

Kisa Cha Pili.
Kuna jamaa mmoja alikuwa ana tatizo dogo tu na jirani yake shambani. Akawa anasema migomba flani ni ya kwake.yule mzee akamwambia hapana hili shina la Mgomba lipo shambani kwangu. Jamaa mbabe akasema ni lake na atakata.

Kweli ule mgomba mmoja ukazaa. Siku hiyo jamaa akaenda shambani akachonga chonga majani ili akate ndizi. Kunyanyua panga. Mkono ulipigwa ganzi haukushuka. Ukabaki juu na panga.

Akapiga kelele sana maana mkono ukawa kama unanyongwa hivi.watu wakamchukua kumpeleka kwake. Mkono ulipooza.
Mbona HAKUNA hata kisa cha kusisimua?

Usiogope uchawi wala nguvu za giza, mwisho wa hivyo vitimbi ni DAMU NA JINA TAKATIFU LA YESU KRISTO WA NAZARETH.

Hakuna cha uchawi, ulozi, pepo, wala jini mwenye kiburi mbele ya jina la Mwana wa Mungu.

"Kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETH, Ewe pepo wa hofu juu ya uchawi unayeishi ndani ya watu wa JF NINAKUFUNGA na NAKUAMURU TOKA, kwa Jina la Yesu Kristo Toka ndani yao, Tokaaaaaa.. Amen"

Kwa imani, ukitumia Damu na Jina La Yesu HAKUNA uchawi WALA nguvu za giza ZITAINUKA na KUSIMAMA DHIDI YAKO.

Mbarikiwe.
 
Hili nalo linategemeana na maumbile. Wewe ukishikwa chuchu au sehemu gani unasisimuka?unaloana?
 
Kigoma Visa vya Uchawi na Ushirikina.

Kigoma ni moja ya Mikoa ambayo inasifika kwa Uchawi nchini Tanzania. Huu mkoa kiasili una watu wachapa kazi sana. Si wazembe ukilinganisha na mikoa mingine yenye ushirikina kama Tanga,Pwani au Zanzibar.

Kigoma maeneo ambayo yanasifika sana kwa Uchawi ni Mwandiga, Ujiji,Mwamgongo n.k

Hapo Mwamgongo ni hatari sana karibu na Mbuga ya Gombe. Kunasifika na moja ya visa vya uchawi ni kimoja ambacho kilitokea mwaka 2020 ni kifo cha Diwani mmoja ambaye inasemekana alichukua Mke wa mtu.

Huyu Diwani ambaye allhamdulilah alikuwa na vijicent ilitokea akawa anatembea na mke wa raia mmoja kijijini hapo.

Yule bwana Raia alipata taarifa. Akanyamaza. Diwani akafikia hatua akaona aoe kabisa mke wa jamaa. Na mke akadai talaka ili akaolewe na Diwani.

Jamaa alimfuata Diwani na kumwambia kwa upole tu kuwa "Mheshimiwa najua unatembea na mke wangu, tafadhali usimwoe maana mimi ntapata shida kulea watoto hawa 6 nlio nao na nina mke mwingine. Uwe na uhusiano naye lakini usimuoe"

Diwani alijibu kwa jeuri tu kuwa "mkeo ndiye anayenilazimisha mzuie yeye siyo mimi"

Jamaa akamenda mpaka kwa viongozi wengine wa kijijini pale akitaka wakamsihi Diwani asimwoe mkewe. Diwani akakaza.

Mpaka jamaa akaenda kwa Rafiki mkubwa wa Diwani kumwomba amsihi rafiki yake asimwoe mkewe yeye atapata shida na watoto. Diwani akamtolea nje jamaa.

Basi jamaa akanyamaza. Siku moja Diwani akakutana na Jamaa Mitaa flani kuna Soko. Diwani akaanza mshambulia jamaa kwa maneno kuwa "nasikia unataka niroga..

Huniwezi,mimi mpaka kufika kuwa Diwani nmetoka mbali sana..." Akaendelea mbele na kumwambia haya nakupa mate na nyayo hii chukua." Akatema mate. Jamaa alimwambia tu Diwani "huo uchawi wa kuchukua mate na nyayo ni mdogo sana,wa watu ambao ni underdog/amateur"

Akaondoka zake. Baada ya siku chache tu Diwani akaanza kuumwa sukari ikapanda mara akaanguka ndo basi tena. Akafa.

Akazikwa. Baada ya siku chache wanafamilia yake wakawa wanamwona Diwani anakuja anagonga pale kwao kuwa afunguliwe mlango anateswa sana.

Diwani alikuwa amevaa pensi chafu.anagonga dirishani akisema anachapwa sana viboko. Afunguliwe.

Mke na watoto wakawa nao wanajawa woga.

Hili tukio lilitokea Mkoani Kigoma mwisho wa Reli.

Na watu wa Kigoma tofauti na Mikoa ya Pwani. Pwani mchawi wako mnaweza mkawa mnacheka naye na kula naye huku anakuroga.

Kigoma ukikorofishana na mtu anakwambia kabisa bila kuuma uma maneno "nitakuroga" hata hatumii sauti ya vitisho. Anakuambia kwa upole tu akikuahidi kuwa kweli atakuroga mbele za watu wengine.na anaenda kukuroga kweli.

Hiki ni moja ya kisa cha mambo ya Uchawi Kigoma.nitaleta Visa vingine vya Uchawi na Ushirikina Kigoma.

Kisa Cha Pili.
Kuna jamaa mmoja alikuwa ana tatizo dogo tu na jirani yake shambani. Akawa anasema migomba flani ni ya kwake.yule mzee akamwambia hapana hili shina la Mgomba lipo shambani kwangu. Jamaa mbabe akasema ni lake na atakata.

Kweli ule mgomba mmoja ukazaa. Siku hiyo jamaa akaenda shambani akachonga chonga majani ili akate ndizi. Kunyanyua panga. Mkono ulipigwa ganzi haukushuka. Ukabaki juu na panga.

Akapiga kelele sana maana mkono ukawa kama unanyongwa hivi.watu wakamchukua kumpeleka kwake. Mkono ulipooza.
Wakukutishia tena uanze kulalamika kama kipindi kileee
 
hii pimbi inaleta ujuaji kisa ipo NYU York pambaf kabisa aje huku Nyumbanitu ajifunze mavitu!

Kwahiyo wachawi wanapaa, wanayeyuka, wanafufuka ila hawawezi kufika NY?

Hapo hapo mnasema wachawi wanaweza kila kitu ila hawawezi kupata details zangu au nywele bila mimi kuwapa?

Nimewarahisishia kabisa toeni jina tu la huyo Diwani mliyedanganywa na Chizi Maarifa niwape 500K napo mnashindwa. Sasa uchawi wenu unaweza nini enyi midanganyika?

Story zenu don't add up. Kiwango chenu cha uzwazwa inabidi mkilipie tozo nyie midanganyika empty set kabisa.
 
Kuna siku nilikiwa kibondo pale wilaya ya kgm sasa kuna guest nifikia (jina lina anza na miku...) sasa umefika ucku mda wa kulala nikavyua ngua zangu nikazitupa chini tu, asubu kuamka nikakuta nguo zimeloanishwa maji yani ukizikamua zinatoa maji na hakuna mvua iliyonyesha wala maji waliyoingia ndan chumba kizima likuwa kikavu na chumba kilikukuwa sio self labda kusema maji yametoka chooni kuingia ndani na chumba nilifunga na funguo kwa ndani!

Sitisahau lile tukio
Labda ulipiga vyombo sana ukajikojolea
 
Nimetunga Tu ili kustawisha mjadala. Ni kweli Nina shida lakini siwezi kuchukua Kwa namna hii nilikuwa nastawisha Uzi Tu hata Jina nimetunga SASA hivi.

I love your honesty. Ubarikiwe

To keep my word I was willing to pay you some for giving it a shot and still am.

Asante for being honest.
 
Hili nalo linategemeana na maumbile. Wewe ukishikwa chuchu au sehemu gani unasisimuka?unaloana?
Ndugu ulikusudia kuni-quote mimi?

Ukija kimwili nakulipua kimwili ukija kiroho nakumaliza kiroho na ukija kifedhuli Mungu amenipa kibali cha kukupasua kifedhuli.

Katika yote, nakukumbusha tubu dhambi zako na Mungu ATAKUSAMEHE.
 
Again, story zote za ushirikina ni hearsay stories, wewe umesimuliwa na aliyekusimulia naye alisimuliwa ukitrace mzizi wake ni mjinga mmoja tu alijitungia na nyie mnaamini kama ilivyo.

Kwa ujinga huu kwenye hayo mafuvu yenu bora serikali iendelee kuongeza kodi tu. Hakuna uchawi
Hayati Jpm aliwai kusimulia tukio walipo kua wanatengeneza barabara alisema bulldoza lilikua linang'oa mti....mti ukagoma....mpaka wanafanya mambo ya kimila

Waulize tanesko walipo kua wanapitisha umeme kweny kaburi la martin njia ya Iringa....

Ishu zinginee kama hauna Cha kuchangia unanyamaza unasoma comment za watu...
 
Uchawi upo na hakika Upo. Nimewahi pata ladha ya hii kitu usiombe. Ila hii Dunia ina mambo.

Usiku mmelala unasikia watu wanaongea na kucheka ndanii ukiangalia huoni watu. Watu wanatembea ndani au harufu ya ugali kupikwa ndani. Acha tu Haya mambo.

Miaka ya 90s nikiwa mdogo huko kijijini kwetu kuna bibi alikua anasifika kwa uchawi balaa na alikua anaishi peke yake tu. Siku moja nimetumwa jioni jioni nikakutana nae huko vijijini unakuta barabara nyingi pembezoni zimepandwa maminyaa alafu kuna kua na gizagiza afu barabara zina vichakavichaka basi nikakutana nae yule mzee anatembelea fimbo yuko pekee na nywele zake nyeupe peee, aseee ukimtazama tu kwa macho unakubali huyu ni jabali. Sema Ardhi imemeza vingi.
 
Mbona HAKUNA hata kisa cha kusisimua?

Usiogope uchawi wala nguvu za giza, mwisho wa hivyo vitimbi ni DAMU NA JINA TAKATIFU LA YESU KRISTO WA NAZARETH.

Hakuna cha uchawi, ulozi, pepo, wala jini mwenye kiburi mbele ya jina la Mwana wa Mungu.

"Kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETH, Ewe pepo wa hofu juu ya uchawi unayeishi ndani ya watu wa JF NINAKUFUNGA na NAKUAMURU TOKA, kwa Jina la Yesu Kristo Toka ndani yao, Tokaaaaaa.. Amen"

Kwa imani, ukitumia Damu na Jina La Yesu HAKUNA uchawi WALA nguvu za giza ZITAINUKA na KUSIMAMA DHIDI YAKO.

Mbarikiwe.
Mkuu kwa imani yako uchawi upo au haupo?
 
Hayati Jpm aliwai kusimulia tukio walipo kua wanatengeneza barabara alisema bulldoza lilikua linang'oa mti....mti ukagoma....mpaka wanafanya mambo ya kimila

Waulize tanesko walipo kua wanapitisha umeme kweny kaburi la martin njia ya Iringa....

Ishu zinginee kama hauna Cha kuchangia unanyamaza unasoma comment za watu...

Sababu JPM kasema ndo niamini? Story yake inatofauti gani na story ya kusadikika aliyoleta huyu bwana hapa. Sio JPM huyo huyo aliyewaambia hakuna corona na kugomea chanjo afu ikamuondoa yeye mwenyewe?

Kuhusu kaburi la Kiyeyeu Isimila Iringa ukweli ni huu: Survey ya kwanza ya kupitisha nyaya za umeme eneo hilo ilifanyika bila kuzingatia uwepo wa makaburi hayo ya familia ya Kiyeyeu. Nguzo zilipofikishwa hapo ikaonekana kuwa nyaya za umeme itabidi zipite juu ya makaburi hayo, hivyo yakaibuka masuala ya FIDIA KWA FAMILIA YA KIYEYEU NA KUHAMISHA YALE MAKABURI. Kwa kuwa mradi ulikwisha anza, wenye mradi wakaamua kuyakwepa makaburi hayo ili kutatua matatizo hayo mawili niliyoyataja. Hilo watu hawakuambiwa hali ambayo imeelekea kuleta tafsiri potofu kama inavyoenezwa!

Aidha 2010 TANROADS ilifukua na kulitupilia mbali huko na hamna kitu kilitokea. Link hii hapa:

Tatizo lenu kila mnachoambiwa nyie mnaamini tu kama minyumbu hamtumii bongo zenu kabisa kufikiri, kichwa sio kwaajili ya kufuga nywele tu nyie midanganyika tumieni akili.

Mwisho, wasaidie wenzio kutaja jina la huyo Diwani ambalo hata mleta uzi mwenyewe halijui ila nyie midanganyika mnaamini nikutumie muamala 500k taslim TSH.

Mh Mwigulu Nchemba kwa kiwango hiki cha ujinga wanachoonyesha hawa wadanganyika kwenye jukwaa la great thinkers natoa rai kuwe na tozo ya uzwazwa. Hawa watu ni empty set kabisa inabidi walipie ujinga wao.
 
Mkuu kwa imani yako uchawi upo au haupo?
2 Wafalme 17:17
"Wakawapitisha watoto wao, waume na wake, motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, hata kumkasirisha."

Uchawi upo, Ramli ipo.. Ninafahamu upo na ni kazi yangu kwa IMANI yangu kupambana nao kila iitwapo leo.

Isaya 47:12
"Simama sasa na uganga wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaabisha nao tangu ujana wako; labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda."

Huko kwa waganga ndiko ulikojaa uchawi, Lakini Tumaini letu ni kwa Bwana, Kristo Yesu Mfufuka.

Binafsi, nimekwisha kutuna na visa kadhaa vya kichawi na ndio maana nikasema mbona visa vyake si vya kusisimua.. nimekishwa pambana na visa vingi vya kichawi juu yangu na juu ya watu wa Mungu, Lakini katika yote Wachawi ni watu wasio na uwezo wowote mbele ya waamino halisi.. mchawi hana nguvu mbele ya Damu na Jina Takatifu lipitalo Majina yote la YESU KRISTO WA NAZARETH.

Je, unataka kufahamishwa nini kuhusu wachawi?
 
Back
Top Bottom