2 Wafalme 17:17
"Wakawapitisha watoto wao, waume na wake, motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, hata kumkasirisha."
Uchawi upo, Ramli ipo.. Ninafahamu upo na ni kazi yangu kwa IMANI yangu kupambana nao kila iitwapo leo.
Isaya 47:12
"Simama sasa na uganga wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaabisha nao tangu ujana wako; labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda."
Huko kwa waganga ndiko ulikojaa uchawi, Lakini Tumaini letu ni kwa Bwana, Kristo Yesu Mfufuka.
Binafsi, nimekwisha kutuna na visa kadhaa vya kichawi na ndio maana nikasema mbona visa vyake si vya kusisimua.. nimekishwa pambana na visa vingi vya kichawi juu yangu na juu ya watu wa Mungu, Lakini katika yote Wachawi ni watu wasio na uwezo wowote mbele ya waamino halisi.. mchawi hana nguvu mbele ya Damu na Jina Takatifu lipitalo Majina yote la YESU KRISTO WA NAZARETH.
Je, unataka kufahamishwa nini kuhusu wachawi?