Seran
JF-Expert Member
- Feb 7, 2025
- 36,315
- 104,500
Tupo katika zama za mwisho aisew!! Yani unakuta baba mtu mzima anakomalia waende sambamba na mwanamke wake! Na wanavyochukulia poa swala zima la mwanamke kuzaa watoto kwanini na wao wasijaribu? Majukumu huwa hayaingiliani kabisa! Mtu amekosa point ya kuzuia mwanamke kupewa kipaumbele katika jamii, basi anakuja na hayo mawazo ya kijinga jinga eti 50/50 ndani ya familia! Uliona wapi katika jamii yetu??Hizo hua ni dalili za mwanaume kutamani kua mwanamke yaani anaumia akiona mwanamke wake anabaki nyumbani kulea watoto na yeye anaenda kusulubika kwa kazi ngumu, anatamani yeye angekua mwanamke ili abakishwe nyumbani bila kujua huyo anayemuona golikipa ndie anayemlelea watoto wake na kusaidia mambo ya nyumbani yakae sawa na ndie anayepokea wageni wake wakija kumtembelea,
Nadhani wazee wangeirudisha Jando, wavulana wa siku hizi wanaukimbia sana uvulana wao wanapenda kushindana na wanawake kwenye kila kitu hadi kulelewa wenyewe wanawaita mishangazi.
Acha waendelee kujifariji! Ni kama kutwanga maji kwenye kinu! 🚮🚮