Kwa mazingira haya usitarajie Syria Arab Army iwe na maajabu, hata hivyo Syria hawajawahi kuwa na jeshi la maana katika historia. Ila sasa wamezidi yani kama mgambo.
One on one Israel dhidi ya Hamas au Israel dhidi ya Hizbullah lakini Israel ikichangiwa lazima US aisaidie.Pale Israel usa akikata msaada kwa miezi 6 tu hata hakuna nchi pale
Hii Israel iliyo peleka wanajeshi zaidi ya elfu hamsini wenye kila aina ya siraha kupambana na wanamgambo wa Hizbullah wakaambulia kuteka eneo la km za mraba 7 ambazo ukubwa wake haufiki hata kitongoji?
Shambuliz uchwara sio angeendeleza kama alikuwa kidume. Si alisema kikirushwa hata kijiko.Hizi hadithi tushazichoka huyo iran anaetafutwa kamdunda Israel mchana kweupe jua linawaka dunia imeona kama ni hiyo vita si ingeanzishwa pale,, zaidi ya kumjibu kwa shambulizi uchwara lililopambwa na propaganda nyingi kuficha aibu.
Hongera Mkuu ,umechambua vyema nimekuelewaUkiangalia kwa undani makundi ya waasi yanayopigana dhidi ya utawala wa dikteta Bashir Al-Assad nchini Syria hayatoi matumaini mema kwamba endapo yatafanikiwa kumng'oa Assad siku za usoni za Syria zitakuwa njema chini ya utawala wao mpya, makundi yanayompinga Assad ukiondoa Wakurdi nusu yake ni makundi ya kijihadi yenye msimamo mkali. Haya makundi yakishika madaraka ina maana Syria itageuzwa taifa la kidini rasmi na inaweza kugeuka changamoto nyingine kubwa si kwa raia wa ndani tu bali hata nchi majirani ikiwemo Israel.
Familia ya Assad ambayo ni alawites , tawi la Washia lenye msimamo tofauti na sehemu kubwa ya Waislamu ikiwemo kuruhusu matumizi ya pombe na kutoamini kabisa wanawake kuvaa hijabu ni takwa la lazima la dini wameiendesha Syria kama taifa jumuishi la imani zote kwa muda mrefu japo chini ya utawala wa chama kimoja cha Baath, hakuna uhakika kama waasi watakoingia kumrithi Assad watadumisha taifa jumuishi la Syria lisilo la kidini au lenye mrengo wa upande mmoja zaidi wa kidini na hapo ndipo migogoro itapozidi na kuharibu mambo kabisa.
Ni kweli kihistoria Syria chini ya utawala wa familia ya Assad haujawahi kuwa rafiki sana wa Israel lakini pia haijawahi kuwa utawala wa uadui wa kiwendawazimu sana kuipasua kichwa Israel, mara nyingi imejizuia au imejiepusha kuingia katika migogoro isiyo ya lazima na Israel. Mtihani mkubwa ni kwamba Syria ya Assad imekuwa kibaraka wa Iran wakati wote ambaye ni adui mkubwa wa Marekani na Israel.
Waarabu huwa wanashindwa kupiga mahesabu ya kina aisee.
Badala mkubali kukaa chini ya bendera moja ya utawala mujenge taifa mnaleta utofauti unaowagawanya na kuharibu nchi na kuipasua kipande kipande.
Hili la Syria na Libya halina tofauti sana.
Ndio maana kuna mtu kule juu nikamwambia mbumbumbu waarabu.Waarabu wana mihemuko ya kikabila na kidini.... ndio maana ni rahisi kuwa manipulate .. hapo Syria, Libya, hata Iraq ilikuwa hivyo
Ww serikali yako haiuwi wapinzani wake ?We jamaa ni mnafiki sn , eti Mashariki ya kati ilikuwa imetulia , Kwa vile walikuwa hawakuonesh Sadam anavyoua wapinzan wake ?
Sunni imegawanyika katika madhebu/sects mbalimbali, wapo Wahhabi wanaojulikana kwa misimamo mikali na kukosa uvumulivu dhidi ya imani nyingine, magaidi wengi ndio wanatokea mkondo huu. Wapo salafi, sufi, hanafi n.k Ukiwa bongo sio rahisi uelewe kwa sababu hakuna hii migawanyiko kwa uwazi kutokana na udhibiti wa BAKWATA.It has nothing to do with Sunni, Sadam ni Sunni na alikuwa ni rafiki mkubwa Wa wakristo Middle East, same kwa Pan Arab leaders wengine kama Kina Yaser Arafat. Haya makundi yanayofadhiliwa na west na Marekani ndio yanayoua wakristo Middle East. Divide and Conquer kuhakikisha kila kundi linapigana na mwenzake wao wachote Mafuta kirahisi.
Jeshi la Syria halikuwa katika utiyari wa kimapambano kwa sababu ilionekana vita ya Syria inaelekea kuisha baada ya makubaliano ya Urusi,Iran na Uturuki huko Astana Kazakhstan.Assad muda wote alikuwa busy kulifanya jeshi lake kuwa coup-proof tu mambo mengine ziada. Kati ya Marais nawakubali kwa kujilinda dhidi ya mapinduzi duniani ni Bashar al-Assad.
Mkuu wa 4th Armored Division, kikosi maalum cha jeshi la Syria kinachokuwa kusini mwa Damascus kinaongozwa na Major General Maher al-Assad mdogo wake Rais.
Assad ana mashirika ya ujasusi kama matatu hivi yanayojitegemea na yanachunguzana, kama sikosei jeshi wana la kwao, Airforce ina la kwake (nahisi sababu baba yake Hafez alipindua kutokea Airforce aliasisi hili), polisi wana la kwao, wizara gani sijui mambo ya ndani wana la taifa kiujumla.
Assad anaongoza nchi ambayo dhehebu lake na jamii yake ni minority hivyo wanajeshi wengi sio dini yake wala jamii yake. Anachokifanya anakusanya wanajeshi kutoka maeneo yanayomuunga mkono ila maofisa wa juu wa majeshi yake ni kutoka minorities. Si rahisi Msuni kutoka Allepo awe ofisa mkubwa kwenye jeshi la Assad. Kwa hiyo jeshi maofisa wake sio competent bali asili, eneo, uchawa na dhehebu ndio vinawabeba.
Hata kwa wanajeshi wenyewe, baada ya vita kutokea kulikuwa na forces recruitment. Serikali ya Assad ina rushwa kubwa na ufisadi kupindukia, na jeshini hachukui hatua kuzuia ilimradi maofisa ni machawa wake anawaachia nafasi "wale" ili walinde serikali yake huku wanalinda matumbo yao. Kwahiyo recruitment inakwepwa endapo kijana familia yake ina hela kutoa rushwa asiende jeshini. Recruitments waliopo jeshini hawako motivated, huwezi wapiganisha na waasi au magaidi ambao wengi wamejiunga kwa kutaka wenyewe.
Training ya Syrian Arab Army ni dhaifu. Wana miaka zaidi ya 10 vitani ila hawana defensive lines, hawajui repelling of fast attack, hawajajipanga dhidi ya drones, hawajui kufanya retreat wakiondoka sehemu wanakurupuka wanaacha silaha ziko intact zinachukuliwa na adui badala kuziharibu au kuzihamisha.
Na kwa sababu ya vikwazo vya kiuchumi na hali ngumu nchini Syria, Assad alitumia vyombo vya usalama kuzalisha kipato kwa madawa ya kulevya. Wanasafirisha shehena ya madawa pale Middle East angalau wapate kipato cha kudunduliza juu ya hali yao ngumu.
Kwa mazingira haya usitarajie Syria Arab Army iwe na maajabu, hata hivyo Syria hawajawahi kuwa na jeshi la maana katika historia. Ila sasa wamezidi yani kama mgambo.
Acha kurahisisha mambo vita sio rahisi kama unavyo fikiri.Huu ndio ulikuwa muda wa Israel kumalizana na Hizbullah na Iran wakati mwingine kuwaelewa Hawa Wazungu wanataka nini ni kazi sana
Hata bongo wapo hao salafi,suffiyyah n.k.Sunni imegawanyika katika madhebu/sects mbalimbali, wapo Wahhabi wanaojulikana kwa misimamo mikali na kukosa uvumulivu dhidi ya imani nyingine, magaidi wengi ndio wanatokea mkondo huu. Wapo salafi, sufi, hanafi n.k Ukiwa bongo sio rahisi uelewe kwa sababu hakuna hii migawanyiko kwa uwazi kutokana na udhibiti wa BAKWATA.
Nchi zenye utajiri lazima ziwe na fitina. Kama huyajuwi usiyaingilie, maliza matatizo yako kwanza.
View: https://x.com/Osint613/status/1863602609455546419?t=wxCrPgA_WgTLkcV-OyMd0Q&s=19
FaizaFoxy Assad na yeye ni mzayuni au hana namna 😂😂😂
Unajua Israel ikisema itupe zile Silaha ilizokamata kwa Hezbollah na Iwe inafanya Mashambulizi 10 Syria kila siku kuwasaidia Makobazi ndani ya miezi 3 Assad atabaki na Kijiji tu
Huyu jamaa kweli mtoto wa kidiplomasia.Nchi zenye utajiri lazima ziwe na fitina. Kama huyajuwi usiyaingilie, maliza matatizo yako kwanza.
Najiuliza hapa Hawa jamaa wakiuwana pia watahesabika ni martyr ama vipi?Kataib Hezbollah na Vikundi vingine vya Kishia vimeanza kuingia Syria kama Nzige, vinatokea Iraq and Beyond👇
View: https://youtu.be/MeBckllq07w?si=UKdRx3wpMxZoZK9k
Mambo yanazidi kuwa Motomoto.
Gaidi ni dictator kwako ni watu wa aina gani ?Ukiangalia kwa undani makundi ya waasi yanayopigana dhidi ya utawala wa dikteta Bashir Al-Assad nchini Syria hayatoi matumaini mema kwamba endapo yatafanikiwa kumng'oa Assad siku za usoni za Syria zitakuwa njema chini ya utawala wao mpya, makundi yanayompinga Assad ukiondoa Wakurdi nusu yake ni makundi ya kijihadi yenye msimamo mkali. Haya makundi yakishika madaraka ina maana Syria itageuzwa taifa la kidini rasmi na inaweza kugeuka changamoto nyingine kubwa si kwa raia wa ndani tu bali hata nchi majirani ikiwemo Israel.
Familia ya Assad ambayo ni alawites , tawi la Washia lenye msimamo tofauti na sehemu kubwa ya Waislamu ikiwemo kuruhusu matumizi ya pombe na kutoamini kabisa wanawake kuvaa hijabu ni takwa la lazima la dini wameiendesha Syria kama taifa jumuishi la imani zote kwa muda mrefu japo chini ya utawala wa chama kimoja cha Baath, hakuna uhakika kama waasi watakoingia kumrithi Assad watadumisha taifa jumuishi la Syria lisilo la kidini au lenye mrengo wa upande mmoja zaidi wa kidini na hapo ndipo migogoro itapozidi na kuharibu mambo kabisa.
Ni kweli kihistoria Syria chini ya utawala wa familia ya Assad haujawahi kuwa rafiki sana wa Israel lakini pia haijawahi kuwa utawala wa uadui wa kiwendawazimu sana kuipasua kichwa Israel, mara nyingi imejizuia au imejiepusha kuingia katika migogoro isiyo ya lazima na Israel. Mtihani mkubwa ni kwamba Syria ya Assad imekuwa kibaraka wa Iran wakati wote ambaye ni adui mkubwa wa Marekani na Israel.
Syria haijawahi kuwa na jeshi competent hata kwenye vita ya Ramadhani Misri ndio ilipigana vizuri wakati concentration ya majeshi ya Israel ilikuwa dhidi yake pale Sinai. Syria ilikumbana na resistance ya majeshi kidogo ya Israel na ilikuwa na numbers ikashindwa basic manouvers na uharaka. Ikapigwa ikakaribiwa kufika Damascus ikahaha ikaanza mazungumzo.Jeshi la Syria halikuwa katika utiyari wa kimapambano kwa sababu ilionekana vita ya Syria inaelekea kuisha baada ya makubaliano ya Urusi,Iran na Uturuki huko Astana Kazakhstan.
Hivyo Syria ilipunguza wanajeshi kwenye mstari wa mbele ili kupunguza gharama za vita na wanamgambo wengi kutoka Lebanon,na Iraq walio kuwa wanapigana upande wa jeshi la Syria waliondoka.
Na pia kulikuwa na mazungumzo kati ya serikali ya Syria na Uturuki kuhusu kurudishwa kwa mahusiano kati ya nchi hizo hivyo akuna aliye tarajia iwapo hiyo ambush ingetokea.
Mimi nadhani hata washirika wa Uturuki barani Ulaya na Marekani watakuwa wamebaki na mshangao mkubwa wa kipi anacho kitaka Edorgan nchini Syria.
Mkuu huwezi kulibeza jeshi lililo pambana na rundo la makundi yaliyo kuwa yakipokea siraha kutoka kila nchi inayo itwa kubwa hapa duniani kwa miaka kumi na kitu.
Hata hivyo hao waasi wanaenda kuipoteza hata hiyo Idilibu walio kuwa wameachiwa na serikali maana kwa sasa Uturuki hatokuwa na maneno yeyote mazuri ya kuwashawishi Urusi na Iran juu ya waasi hao kama alivyo fanya 2020.
Kwahiyo kama siyo mengi ni Bora yachukuliwe si ndioMafuta ya Syria sio mengi kihivyo
Wahabi=salafi na kila kundi linalofadhiliwa na Saudi litaitwa Wahabi/Salafi.Sunni imegawanyika katika madhebu/sects mbalimbali, wapo Wahhabi wanaojulikana kwa misimamo mikali na kukosa uvumulivu dhidi ya imani nyingine, magaidi wengi ndio wanatokea mkondo huu. Wapo salafi, sufi, hanafi n.k Ukiwa bongo sio rahisi uelewe kwa sababu hakuna hii migawanyiko kwa uwazi kutokana na udhibiti wa BAKWATA.