Assad muda wote alikuwa busy kulifanya jeshi lake kuwa coup-proof tu mambo mengine ziada. Kati ya Marais nawakubali kwa kujilinda dhidi ya mapinduzi duniani ni Bashar al-Assad.
Mkuu wa 4th Armored Division, kikosi maalum cha jeshi la Syria kinachokuwa kusini mwa Damascus kinaongozwa na Major General Maher al-Assad mdogo wake Rais.
Assad ana mashirika ya ujasusi kama matatu hivi yanayojitegemea na yanachunguzana, kama sikosei jeshi wana la kwao, Airforce ina la kwake (nahisi sababu baba yake Hafez alipindua kutokea Airforce aliasisi hili), polisi wana la kwao, wizara gani sijui mambo ya ndani wana la taifa kiujumla.
Assad anaongoza nchi ambayo dhehebu lake na jamii yake ni minority hivyo wanajeshi wengi sio dini yake wala jamii yake. Anachokifanya anakusanya wanajeshi kutoka maeneo yanayomuunga mkono ila maofisa wa juu wa majeshi yake ni kutoka minorities. Si rahisi Msuni kutoka Allepo awe ofisa mkubwa kwenye jeshi la Assad. Kwa hiyo jeshi maofisa wake sio competent bali asili, eneo, uchawa na dhehebu ndio vinawabeba.
Hata kwa wanajeshi wenyewe, baada ya vita kutokea kulikuwa na forces recruitment. Serikali ya Assad ina rushwa kubwa na ufisadi kupindukia, na jeshini hachukui hatua kuzuia ilimradi maofisa ni machawa wake anawaachia nafasi "wale" ili walinde serikali yake huku wanalinda matumbo yao. Kwahiyo recruitment inakwepwa endapo kijana familia yake ina hela kutoa rushwa asiende jeshini. Recruitments waliopo jeshini hawako motivated, huwezi wapiganisha na waasi au magaidi ambao wengi wamejiunga kwa kutaka wenyewe.
Training ya Syrian Arab Army ni dhaifu. Wana miaka zaidi ya 10 vitani ila hawana defensive lines, hawajui repelling of fast attack, hawajajipanga dhidi ya drones, hawajui kufanya retreat wakiondoka sehemu wanakurupuka wanaacha silaha ziko intact zinachukuliwa na adui badala kuziharibu au kuzihamisha.
Na kwa sababu ya vikwazo vya kiuchumi na hali ngumu nchini Syria, Assad alitumia vyombo vya usalama kuzalisha kipato kwa madawa ya kulevya. Wanasafirisha shehena ya madawa pale Middle East angalau wapate kipato cha kudunduliza juu ya hali yao ngumu.
Kwa mazingira haya usitarajie Syria Arab Army iwe na maajabu, hata hivyo Syria hawajawahi kuwa na jeshi la maana katika historia. Ila sasa wamezidi yani kama mgambo.