Vita vya Syria vina mchanganyiko sana, ila dikteta Assad ni uovu wenye afadhali (lesser evil) kuliko waasi Wanajihadi

Vita vya Syria vina mchanganyiko sana, ila dikteta Assad ni uovu wenye afadhali (lesser evil) kuliko waasi Wanajihadi

Hii Israel iliyo peleka wanajeshi zaidi ya elfu hamsini wenye kila aina ya siraha kupambana na wanamgambo wa Hizbullah wakaambulia kuteka eneo la km za mraba 7 ambazo ukubwa wake haufiki hata kitongoji?

Yaani huko Syria huwa wakipigwa na Assad wanamuita Netanyahau na Leo ametoa dozi
 
Hizi hadithi tushazichoka huyo iran anaetafutwa kamdunda Israel mchana kweupe jua linawaka dunia imeona kama ni hiyo vita si ingeanzishwa pale,, zaidi ya kumjibu kwa shambulizi uchwara lililopambwa na propaganda nyingi kuficha aibu.
Shambuliz uchwara sio angeendeleza kama alikuwa kidume. Si alisema kikirushwa hata kijiko.
 
Ukiangalia kwa undani makundi ya waasi yanayopigana dhidi ya utawala wa dikteta Bashir Al-Assad nchini Syria hayatoi matumaini mema kwamba endapo yatafanikiwa kumng'oa Assad siku za usoni za Syria zitakuwa njema chini ya utawala wao mpya, makundi yanayompinga Assad ukiondoa Wakurdi nusu yake ni makundi ya kijihadi yenye msimamo mkali. Haya makundi yakishika madaraka ina maana Syria itageuzwa taifa la kidini rasmi na inaweza kugeuka changamoto nyingine kubwa si kwa raia wa ndani tu bali hata nchi majirani ikiwemo Israel.

Familia ya Assad ambayo ni alawites , tawi la Washia lenye msimamo tofauti na sehemu kubwa ya Waislamu ikiwemo kuruhusu matumizi ya pombe na kutoamini kabisa wanawake kuvaa hijabu ni takwa la lazima la dini wameiendesha Syria kama taifa jumuishi la imani zote kwa muda mrefu japo chini ya utawala wa chama kimoja cha Baath, hakuna uhakika kama waasi watakoingia kumrithi Assad watadumisha taifa jumuishi la Syria lisilo la kidini au lenye mrengo wa upande mmoja zaidi wa kidini na hapo ndipo migogoro itapozidi na kuharibu mambo kabisa.

Ni kweli kihistoria Syria chini ya utawala wa familia ya Assad haujawahi kuwa rafiki sana wa Israel lakini pia haijawahi kuwa utawala wa uadui wa kiwendawazimu sana kuipasua kichwa Israel, mara nyingi imejizuia au imejiepusha kuingia katika migogoro isiyo ya lazima na Israel. Mtihani mkubwa ni kwamba Syria ya Assad imekuwa kibaraka wa Iran wakati wote ambaye ni adui mkubwa wa Marekani na Israel.
Hongera Mkuu ,umechambua vyema nimekuelewa
 
Waarabu huwa wanashindwa kupiga mahesabu ya kina aisee.

Badala mkubali kukaa chini ya bendera moja ya utawala mujenge taifa mnaleta utofauti unaowagawanya na kuharibu nchi na kuipasua kipande kipande.

Hili la Syria na Libya halina tofauti sana.

Waarabu wana mihemuko ya kikabila na kidini.... ndio maana ni rahisi kuwa manipulate .. hapo Syria, Libya, hata Iraq ilikuwa hivyo
 
We jamaa ni mnafiki sn , eti Mashariki ya kati ilikuwa imetulia , Kwa vile walikuwa hawakuonesh Sadam anavyoua wapinzan wake ?
Ww serikali yako haiuwi wapinzani wake ?
Kwa hiyo na ww unatamani nchi yako ivamiwe na kufanywa kama Syria?
 
Huu ndio ulikuwa muda wa Israel kumalizana na Hizbullah na Iran wakati mwingine kuwaelewa Hawa Wazungu wanataka nini ni kazi sana
 
It has nothing to do with Sunni, Sadam ni Sunni na alikuwa ni rafiki mkubwa Wa wakristo Middle East, same kwa Pan Arab leaders wengine kama Kina Yaser Arafat. Haya makundi yanayofadhiliwa na west na Marekani ndio yanayoua wakristo Middle East. Divide and Conquer kuhakikisha kila kundi linapigana na mwenzake wao wachote Mafuta kirahisi.
Sunni imegawanyika katika madhebu/sects mbalimbali, wapo Wahhabi wanaojulikana kwa misimamo mikali na kukosa uvumulivu dhidi ya imani nyingine, magaidi wengi ndio wanatokea mkondo huu. Wapo salafi, sufi, hanafi n.k Ukiwa bongo sio rahisi uelewe kwa sababu hakuna hii migawanyiko kwa uwazi kutokana na udhibiti wa BAKWATA.
 
Assad muda wote alikuwa busy kulifanya jeshi lake kuwa coup-proof tu mambo mengine ziada. Kati ya Marais nawakubali kwa kujilinda dhidi ya mapinduzi duniani ni Bashar al-Assad.

Mkuu wa 4th Armored Division, kikosi maalum cha jeshi la Syria kinachokuwa kusini mwa Damascus kinaongozwa na Major General Maher al-Assad mdogo wake Rais.
Assad ana mashirika ya ujasusi kama matatu hivi yanayojitegemea na yanachunguzana, kama sikosei jeshi wana la kwao, Airforce ina la kwake (nahisi sababu baba yake Hafez alipindua kutokea Airforce aliasisi hili), polisi wana la kwao, wizara gani sijui mambo ya ndani wana la taifa kiujumla.

Assad anaongoza nchi ambayo dhehebu lake na jamii yake ni minority hivyo wanajeshi wengi sio dini yake wala jamii yake. Anachokifanya anakusanya wanajeshi kutoka maeneo yanayomuunga mkono ila maofisa wa juu wa majeshi yake ni kutoka minorities. Si rahisi Msuni kutoka Allepo awe ofisa mkubwa kwenye jeshi la Assad. Kwa hiyo jeshi maofisa wake sio competent bali asili, eneo, uchawa na dhehebu ndio vinawabeba.

Hata kwa wanajeshi wenyewe, baada ya vita kutokea kulikuwa na forces recruitment. Serikali ya Assad ina rushwa kubwa na ufisadi kupindukia, na jeshini hachukui hatua kuzuia ilimradi maofisa ni machawa wake anawaachia nafasi "wale" ili walinde serikali yake huku wanalinda matumbo yao. Kwahiyo recruitment inakwepwa endapo kijana familia yake ina hela kutoa rushwa asiende jeshini. Recruitments waliopo jeshini hawako motivated, huwezi wapiganisha na waasi au magaidi ambao wengi wamejiunga kwa kutaka wenyewe.

Training ya Syrian Arab Army ni dhaifu. Wana miaka zaidi ya 10 vitani ila hawana defensive lines, hawajui repelling of fast attack, hawajajipanga dhidi ya drones, hawajui kufanya retreat wakiondoka sehemu wanakurupuka wanaacha silaha ziko intact zinachukuliwa na adui badala kuziharibu au kuzihamisha.

Na kwa sababu ya vikwazo vya kiuchumi na hali ngumu nchini Syria, Assad alitumia vyombo vya usalama kuzalisha kipato kwa madawa ya kulevya. Wanasafirisha shehena ya madawa pale Middle East angalau wapate kipato cha kudunduliza juu ya hali yao ngumu.

Kwa mazingira haya usitarajie Syria Arab Army iwe na maajabu, hata hivyo Syria hawajawahi kuwa na jeshi la maana katika historia. Ila sasa wamezidi yani kama mgambo.
Jeshi la Syria halikuwa katika utiyari wa kimapambano kwa sababu ilionekana vita ya Syria inaelekea kuisha baada ya makubaliano ya Urusi,Iran na Uturuki huko Astana Kazakhstan.
Hivyo Syria ilipunguza wanajeshi kwenye mstari wa mbele ili kupunguza gharama za vita na wanamgambo wengi kutoka Lebanon,na Iraq walio kuwa wanapigana upande wa jeshi la Syria waliondoka.
Na pia kulikuwa na mazungumzo kati ya serikali ya Syria na Uturuki kuhusu kurudishwa kwa mahusiano kati ya nchi hizo hivyo akuna aliye tarajia iwapo hiyo ambush ingetokea.
Mimi nadhani hata washirika wa Uturuki barani Ulaya na Marekani watakuwa wamebaki na mshangao mkubwa wa kipi anacho kitaka Edorgan nchini Syria.
Mkuu huwezi kulibeza jeshi lililo pambana na rundo la makundi yaliyo kuwa yakipokea siraha kutoka kila nchi inayo itwa kubwa hapa duniani kwa miaka kumi na kitu.

Hata hivyo hao waasi wanaenda kuipoteza hata hiyo Idilibu walio kuwa wameachiwa na serikali maana kwa sasa Uturuki hatokuwa na maneno yeyote mazuri ya kuwashawishi Urusi na Iran juu ya waasi hao kama alivyo fanya 2020.
 
Sunni imegawanyika katika madhebu/sects mbalimbali, wapo Wahhabi wanaojulikana kwa misimamo mikali na kukosa uvumulivu dhidi ya imani nyingine, magaidi wengi ndio wanatokea mkondo huu. Wapo salafi, sufi, hanafi n.k Ukiwa bongo sio rahisi uelewe kwa sababu hakuna hii migawanyiko kwa uwazi kutokana na udhibiti wa BAKWATA.
Hata bongo wapo hao salafi,suffiyyah n.k.
Na madrasa zao zipo,isipokua uzuri wa bongo ni hekima.
Hata mataifa mengine huko kama ya Indo-chinese hayo madhehebu yapo ila hukuti wakinyanyuliana mikono kwasababu ya hekima.
Muarabu na hekima wapi na wapi!??
 
Nchi zenye utajiri lazima ziwe na fitina. Kama huyajuwi usiyaingilie, maliza matatizo yako kwanza.
Huyu jamaa kweli mtoto wa kidiplomasia.
Kwa akili zake anaona Assad atakubali kweli kuwaondoa askari wa IRGC.
Kama huyo Israel ana nguvu mbona alishindwa kuwamaliza Hamas huko Gaza!?
Hao Hizbollah hadi sasa amewagwaya.
 
Ukiangalia kwa undani makundi ya waasi yanayopigana dhidi ya utawala wa dikteta Bashir Al-Assad nchini Syria hayatoi matumaini mema kwamba endapo yatafanikiwa kumng'oa Assad siku za usoni za Syria zitakuwa njema chini ya utawala wao mpya, makundi yanayompinga Assad ukiondoa Wakurdi nusu yake ni makundi ya kijihadi yenye msimamo mkali. Haya makundi yakishika madaraka ina maana Syria itageuzwa taifa la kidini rasmi na inaweza kugeuka changamoto nyingine kubwa si kwa raia wa ndani tu bali hata nchi majirani ikiwemo Israel.

Familia ya Assad ambayo ni alawites , tawi la Washia lenye msimamo tofauti na sehemu kubwa ya Waislamu ikiwemo kuruhusu matumizi ya pombe na kutoamini kabisa wanawake kuvaa hijabu ni takwa la lazima la dini wameiendesha Syria kama taifa jumuishi la imani zote kwa muda mrefu japo chini ya utawala wa chama kimoja cha Baath, hakuna uhakika kama waasi watakoingia kumrithi Assad watadumisha taifa jumuishi la Syria lisilo la kidini au lenye mrengo wa upande mmoja zaidi wa kidini na hapo ndipo migogoro itapozidi na kuharibu mambo kabisa.

Ni kweli kihistoria Syria chini ya utawala wa familia ya Assad haujawahi kuwa rafiki sana wa Israel lakini pia haijawahi kuwa utawala wa uadui wa kiwendawazimu sana kuipasua kichwa Israel, mara nyingi imejizuia au imejiepusha kuingia katika migogoro isiyo ya lazima na Israel. Mtihani mkubwa ni kwamba Syria ya Assad imekuwa kibaraka wa Iran wakati wote ambaye ni adui mkubwa wa Marekani na Israel.
Gaidi ni dictator kwako ni watu wa aina gani ?
 
Jeshi la Syria halikuwa katika utiyari wa kimapambano kwa sababu ilionekana vita ya Syria inaelekea kuisha baada ya makubaliano ya Urusi,Iran na Uturuki huko Astana Kazakhstan.
Hivyo Syria ilipunguza wanajeshi kwenye mstari wa mbele ili kupunguza gharama za vita na wanamgambo wengi kutoka Lebanon,na Iraq walio kuwa wanapigana upande wa jeshi la Syria waliondoka.
Na pia kulikuwa na mazungumzo kati ya serikali ya Syria na Uturuki kuhusu kurudishwa kwa mahusiano kati ya nchi hizo hivyo akuna aliye tarajia iwapo hiyo ambush ingetokea.
Mimi nadhani hata washirika wa Uturuki barani Ulaya na Marekani watakuwa wamebaki na mshangao mkubwa wa kipi anacho kitaka Edorgan nchini Syria.
Mkuu huwezi kulibeza jeshi lililo pambana na rundo la makundi yaliyo kuwa yakipokea siraha kutoka kila nchi inayo itwa kubwa hapa duniani kwa miaka kumi na kitu.

Hata hivyo hao waasi wanaenda kuipoteza hata hiyo Idilibu walio kuwa wameachiwa na serikali maana kwa sasa Uturuki hatokuwa na maneno yeyote mazuri ya kuwashawishi Urusi na Iran juu ya waasi hao kama alivyo fanya 2020.
Syria haijawahi kuwa na jeshi competent hata kwenye vita ya Ramadhani Misri ndio ilipigana vizuri wakati concentration ya majeshi ya Israel ilikuwa dhidi yake pale Sinai. Syria ilikumbana na resistance ya majeshi kidogo ya Israel na ilikuwa na numbers ikashindwa basic manouvers na uharaka. Ikapigwa ikakaribiwa kufika Damascus ikahaha ikaanza mazungumzo.

Syria karibia Hafez al-Assad hajapindua serikali waliishambulia Jordan kulazimisha agenda yao ya Wapalestina na majeshi ya Jordan yakawapiga vibaya na kuwadhibiti kabla Jordan hawajakimbilia kuomba security assurance kwa Israel.

Syria walipopata civil war waasi walikuwa na speed, jeshi lilihasi mno hasa 2011 na 2015. Namba kamiri haijulikani ila Syria ilipoteza almost nusu ya wanajeshi kwa utoro, kukimbia na kujiunga na magaidi. Kabla ya vita wapo wanajeshi zaidi ya 300,000 ila katikati ya vita wapo kama 150,000.

Ndio maana offensives nyingi Assad alipendelea makundi yanayomuunga mkono na si jeshi hasa. Jeshi lake alipenda kuliweka nje na frontline kama hamna ulazima maana hata kupigana lina performance ndogo. Hata Iran na Syria zilijua bora upigane alongside Hezbollah na makundi yanayounga mkono Assad kuliko ushirikiane na jeshi la Assad wanaweza kukuacha frontline wakajifiche.
 
Sunni imegawanyika katika madhebu/sects mbalimbali, wapo Wahhabi wanaojulikana kwa misimamo mikali na kukosa uvumulivu dhidi ya imani nyingine, magaidi wengi ndio wanatokea mkondo huu. Wapo salafi, sufi, hanafi n.k Ukiwa bongo sio rahisi uelewe kwa sababu hakuna hii migawanyiko kwa uwazi kutokana na udhibiti wa BAKWATA.
Wahabi=salafi na kila kundi linalofadhiliwa na Saudi litaitwa Wahabi/Salafi.

Ila kama una hata Abcd za Hao salafi utaona ni Bullshit tu. Katika madhehebu yote ya kiiisilamu wao ndio wa mwisho kwenda Jihadi kutokana na akida yao. Hata Unapoongelea Ulamaa mkubwa Wa Salafi Zama Zetu Sheikh Albani Fatwa yake ni wapalestina Waondoke Palestina hii hapa

Hapa Tanzania tuna salafi wengi mno watu kama Kina Kishki ama Answari sunna etc, ushawahi hata siku moja kuwasikia wana Criticise Serikali? Kwa Imani yao Kiongozi Anakuwa criticised kwa siri tu, unamfata kimya kimya unamuambia

So kusema Salafi ndio wanaongoza hizo Jihadi ni Ignorance ya wasio waisilamu kuhusu Uisilamu.

Kwenye Uisilamu Vita ama Jihadi Zinatokana na Fatwa za Scholars, Hawa maulamaa ndio wanatoa fatwa fanya hivi ama usifanye hivi, sijawahi ona maisha yangu yote hata Scholar mmoja akihalalisha hivyo vikundi, na siku Zote makundi kama Isis na Al Qaeda utaona Scholars wengi wana Wa Refer kama mbwa wa Motoni, Sababu Media ina wa refer kMa Salafi haimaanishiwapo Sahihi na Uisilamu ama Scholars wa Kiisilamu wa nakubaliana na Hilo.
 
Back
Top Bottom