Vita vya Urusi na NATO kupanuka mpaka Afrika Magharibi nani atashinda?

Kumekuwepo na fununu za muda mrefu juu ya kuwepo kwa wapiganaji wa kikundi cha Wagner kilichohusishwa na kiongozi wa Urusi,Vladmir Putin.Hii ilikuwa ni kabla hata ya kuanza kwa vita vinavyoendelea sasa baina ya Ukraine na Urusi.

Katika kipindi kifupi fununu hizo ziliongezeka baada ya kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi kwenye nchi za Afrika magharibi na kati kama vile Mali na Burkinafaso. Mapinduzi hayo mara zote yameambatana na kufukuzwa kwa majeshi ya Ufaransa ambayo ni mwanachama wa jumuiya ya kujihami ya NATO. Hali hiyo ilipelekea Ufaransa kuhamishia shughuli zake Niger ambako tayari Marekani ina kituo chake kikubwa cha kuongozea droni za kupambana na inaowaita wanamgambo wa ISIS na Alqaeda na Bokoharam.

Wiki iliyopita mapinduzi mengine yameendelea nchini huko ambako ilikuwa kama ni ngome kubwa ya washirika wa NATO kwa magharibi ya Afrika.Kilichoshangaza ni kutokea waandamanaji wengi wakiunga mkono mapinduzi hayo na kupeperusha bendera za Urusi.

Nchi ya Ufaransa na nchi nyengine zimehamisha wananchi wake lakini inaonekana ni kwa shingo upande huku ikitafuta mwanya wa kubaki.Kitu kilichowapa moyo kutokutoa tamko la kuondoka moja kwa moja ni tangazo la ECOWAS la kuwataka wanajeshi waliopindua kumrudisha kiongozi wa kidemokrasia,raisi Bazoum ambaye wanasema alichaguliwa kidemokrasia.

Kwa upande mwengine majirani wa Niger,Burkinafaso na Mali na nchi ya Guinea nao wametoa onyo iwapo ECOWAS itatumia nguvu kama walivyotangaza za kumrudisha madarakani raisi Bazoum basi na wao watakuwa pamoja na Niger.

Maamuzi ya ECOWAS ni kama kwamba yanaonekana kuwaunga mkono NATO na kwa upande mwengine NATO nao wameamua kuunga mkono uamuzi huo kwa maslahi ya kubaki Niger hapo.

Jana kiongozi Kuonesha kuwa ECOWAS imedhamiria kufanya kweli hapo juzi mwanachama mkubwa wa umoja huo Nigeria iliizimia umeme Niger ambayo inapata nguvu za nishati ya umeme zaidi ya asilimia 70 kutoka nchini humo.

Kwa upande wa kuonesha Niger nayo imedhamiria kweli kulinda mapinduzi yake hapo jana mmoja wa viongozi wa juu wa mapoinduzi ya kijeshi General Salifou Mody alikwenda Mali kukutana rasmi na wawakilishi wa Wagner kupanga namna ya kuyalinda mapinduzi hayo ambayo yakikamilika na kufanikiwa itakuwa na faida kubwa kwa taifa la Urusi kiuchumi na kisiasa.
Mimi najiuliza Russia inapata wapi fedha za kuendesha Vita na Ukraine! Na wakati huo huo kuendesha vita Africa kuwatimua wakaloni wa nchi za Africa! Imewekewa vikwazo lukuki na nchi za Magharibi lakini bado inaupiga mwingi. Lakini amezihakikishia nchi za Africa kupata nafaka kwa bei ya chini,tena kama sikusahahu bila transport charges,na pia ameahidi kuzifutia madeni baadhi ya nchi!
Fedha za raslimali za waafrica wajinga kama vile oil.gold, uranium, cobalt, nickel etecetera
 
Hizo source uchwara ndio zinatangaza kwamba Russia anamtegemea pia Iran kwa ammunition mbalimbali hasa makombora na zile Shaheed drones sio!?

Mpaka hapo huoni kwamba Ukraine kamkaba koo huyu super pawer wa mchongo?
kama unataka kuelewa analyse mawazo ya watu usiwe conservative kushikilia iman yako. Mrusi Alisha forecast maybe patakuwa na battle kubwa zaid ya hata Ukraine unatakiwa ujipange kuangalia stock ya silaha unazokuwa nazo usije zubaishwa ukraine mbelen ukachapika.

kama umefuatilia vema habar hakuna shambuliz dhid ya Moscow ambalo Ukraine kajitokeza kudai kwamba wao wamehusika directly ushawah jiuliza kwa nn. urusi wao wanasema waz waz
 
Unajua kama USA anaogopa vita ya moja kwa moja na mrusi ?
Haogopi siku akiamua vita itakwisha baada ya masaa 24 na Russia knows that that’s why they don’t dare to use nuclear weapons it’s going to be the biggest mistake in Russian history
 
Be serious, hakuna taifa hata moja la America au Ulaya Magharibi lenye uwezo wa kupigana na Russia eye to eye.
 
Kaangalie Ruble iko ngapi huko

Kaangalie Landing Ship yenu ina hali gani
@HIMARS huna unaloelewa ktk ulimwengu wa uchumi kuwa na currency yenye thaman so kuwa na uchumi mkubwa kk .value ya currency ina impact moja kwa moja kwnye biashara za kimataifa
 
Iko 96 sasa we endelea piga kelele.

Na meli yenu inasaidia na tug boats
 
@HIMARS huna unaloelewa ktk ulimwengu wa uchumi kuwa na currency yenye thaman so kuwa na uchumi mkubwa kk .value ya currency ina impact moja kwa moja kwnye biashara za kimataifa
Mbona luble ilipokuwa juu dhidi ya Dola mlikuwa mnashangilia kama mazombi?
 
Kumekuwepo na fununu za muda mrefu juu ya kuwepo kwa wapiganaji wa kikundi cha Wagner kilichohusishwa na kiongozi wa Urusi,Vladmir Putin.Hii ilikuwa ni kabla hata ya kuanza kwa vita vinavyoendelea sasa baina ya Ukraine na Urusi.

Katika kipindi kifupi fununu hizo ziliongezeka baada ya kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi kwenye nchi za Afrika magharibi na kati kama vile Mali na Burkinafaso. Mapinduzi hayo mara zote yameambatana na kufukuzwa kwa majeshi ya Ufaransa ambayo ni mwanachama wa jumuiya ya kujihami ya NATO. Hali hiyo ilipelekea Ufaransa kuhamishia shughuli zake Niger ambako tayari Marekani ina kituo chake kikubwa cha kuongozea droni za kupambana na inaowaita wanamgambo wa ISIS na Alqaeda na Bokoharam.

Wiki iliyopita mapinduzi mengine yameendelea nchini huko ambako ilikuwa kama ni ngome kubwa ya washirika wa NATO kwa magharibi ya Afrika.Kilichoshangaza ni kutokea waandamanaji wengi wakiunga mkono mapinduzi hayo na kupeperusha bendera za Urusi.

Nchi ya Ufaransa na nchi nyengine zimehamisha wananchi wake lakini inaonekana ni kwa shingo upande huku ikitafuta mwanya wa kubaki.Kitu kilichowapa moyo kutokutoa tamko la kuondoka moja kwa moja ni tangazo la ECOWAS la kuwataka wanajeshi waliopindua kumrudisha kiongozi wa kidemokrasia,raisi Bazoum ambaye wanasema alichaguliwa kidemokrasia.

Kwa upande mwengine majirani wa Niger,Burkinafaso na Mali na nchi ya Guinea nao wametoa onyo iwapo ECOWAS itatumia nguvu kama walivyotangaza za kumrudisha madarakani raisi Bazoum basi na wao watakuwa pamoja na Niger.

Maamuzi ya ECOWAS ni kama kwamba yanaonekana kuwaunga mkono NATO na kwa upande mwengine NATO nao wameamua kuunga mkono uamuzi huo kwa maslahi ya kubaki Niger hapo.

Jana kiongozi Kuonesha kuwa ECOWAS imedhamiria kufanya kweli hapo juzi mwanachama mkubwa wa umoja huo Nigeria iliizimia umeme Niger ambayo inapata nguvu za nishati ya umeme zaidi ya asilimia 70 kutoka nchini humo.

Kwa upande wa kuonesha Niger nayo imedhamiria kweli kulinda mapinduzi yake hapo jana mmoja wa viongozi wa juu wa mapoinduzi ya kijeshi General Salifou Mody alikwenda Mali kukutana rasmi na wawakilishi wa Wagner kupanga namna ya kuyalinda mapinduzi hayo ambayo yakikamilika na kufanikiwa itakuwa na faida kubwa kwa taifa la Urusi kiuchumi na kisiasa.
Waafrika tujitokeze kwa wingi tukawashangilie Wagner.
 
Hata US kwa sasa ananunua Korea, Poland, na nchi nyingine za Ulaya. Hapo kila mtu ashinde mechi zake
Hana akili huyo ,anadhani kununua siraha ni kutokua na siraha hajui kama siraha inakua tofauti bei kutokana na technology na uchumi wa nchi. Unaweza ukapata siraha nzuri tu kwa bei nafuu ikakusaidia kwenye vita yako huku siraha zako zenye high technology unazo mfano ndege za IRAN zisizo na rubani .
 
Hali ya kiusalama tangu hapo si shwari nchi zote za Afrika Magharibi.Nigeria kujiweka kimbelembele sana kuyapinga mapinduzi ya Niger kwa kuwashawishi wengine watumie jeshi kunaweza kuwatumbukiza kwenye mzozo mkubwa wa kiusalama na kusambaratika kuliko nchi nyengine yoyote ya jimbo hilo.
 
ni nchi kubwa mambo yamekaa vibaya mno
USA yupo kuboresha sela zake za kifedha asipoteze say dunian.

USA yupo katika kupambana na lengo la brics wasilete sarafu yao isijewaumiza

Europe wao wapo na kulinda uchumi wao (inflation) mfumuko wa bei ni kikwazo kwao lakin hata kule wanakovunia malighafi kwa (Neo-colonialism ) nako hali c shwari.

wajapan nao hali so shwari kiduku na xi-jing wamewakomalia

huko middle east ni kama wale ndugu waliofarakanishwa na USA+western Europe wameanza kupatana kibaraka wao Israel nae anaweza kuwa mashakan .

Russia katibua mipango mambo ni moto lakin hii ndo vita (The truely definition of WAR ) kila kete inasukumwa sio Military,Diplomacy,Political ,economically wazungu walisha tuacha mbali mno
Macho yote yako Afrika.Kwa upande wa Ulaya wako hali mbaya zaidi kwani hawana maliasili nyingi.Zaidi wanatumia ujanja ule ule wa kinyonyaji wa kikoloni.Wanayatawala mataifa kikoloni kwa kutumia teknolojia za kisasa.
Kwa mfano wafaransa wanawanyonya sana watu wa Afrika magharibi kwa kuanzisha miradi inayowatia utumwani wananchi wake na faida kuenda Ufaransa.
 
Back
Top Bottom