Nakwenda CHATO kupitia bandiko hili,siendi CHATO kutazama mji ulivyokuzwa haraka kwa vitu wala siendi chato kutazama uwanja wa kisasa wa ndege.
Nakwenda chato kumuona amiri jeshi mkuu yes ndiye mh JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Amiri Jeshi Mkuu tunajua uko likizo hilio ni jambo jema hasa kwa kazi kubwa ulionayo ya kuliongoza Taifa hili lenye matatizo lukuki
Mh Amiri jeshi mkuu wakati unakwenda likizo dunia ilianzwa kutikiswa na ugonjwa uitwao corrona Tanzania tulikuwa amepatikana mmoja tu Arusha bado haikuwa tishio japo usambaaji wake kwa nchi zilizoendelea ulionesha kuanza kwa taratibu mwishowe unachanganya kwa haraka
Mh Rais kuna nchi zilidharau huuu ugonjwa Leo zimegeuka vilioo tupu na sisi tulikuwa na cha kujifunza sitaki kulaumu huu sio muda wa kulaumiana ni muda wa kuziba makosa yetu wenyewe.
Ulipokwenda likizo mh Rais mgonjwa alikuwa mmoja hata ww ukiwa kanisani ulituambia ni kagonjwa kadogo hata mwanao makonda alituaminisha pia japo juzi kasarenda mwenyewe
Hivi Leo jumla ya visa 254 vimeripotiwa na 10 washafariki kupitia huu ugonjwa
Najua dhamira yako njema ya ujenzi wa miradi mikubwa ambayo imekupelekea ukashindwakuzuia ndege na kufungwa mipaka najua kwa mujibu wa katiba yetu ww ni chief comforter yaani mfariji mkuu na hili Taifa liendelee lazima afya za watu wake ziwe imara ndio uchumi utapanda.
Mh Rais waziri wa afya chini ya waziri mkuu amefanya kazi kubwa sana madaktari wauguzi wako kazini usiku na mchana Hilo halina shida tuwaombee kwa mungu waendelee na wito
Mh Rais ujumbe wangu kwa kwako katiza likizo njoo kwenye uwanja wa vita adui ameshajitanua sasa rudi DSM ama DODOMA njoo uongoze vitaa hii najua praise team watakwambia usijali Dada yangu ummy mwalimu yupo.
Nikwambie mh Rais kutukuwepo kwako kumepelekea mkuu wa mkoa Dar es saalam akiongea wanadhani umemuachia jahazi mara zote amekosea amegeuza gonjwa hili kuwa siasa rejea alipotoa Siri ya mgonjwa mtoto wa mh freeman mbowe kuwa kapatwa corrona rejea kauli zake za kuudharau maambukizi haya Leo anatuambia watu wa DSm tujadiliane jee tunataka kufa na corrona ama la kwa kauli yake ashakata tamaa.
Mh Rais rudi uzibe gape kati ya waziri wako na ww njoo uwafariji wananchi wako wameumia na wanazidi kuumia na hili gonjwa. Baba mh Rais ugonjwa huu sio aibu kwa serikali yako rudi upiganie afya za wananchi wako sitaki kutaja marais wanaopigana vita wakiwa ofisini nitakuwa sikutendei haki kama ulivyootuomba tufanye maombi tumefanya ni muda wakuja kuongeza nguvu ktk kuukabili ugonjwa huu
Mh Rais hakuna vita nyepesi hakika ww kama jemedari mkuu tunakutegemea sana njooo ufute zile kauli zako za “haka kagonjwa ni kadogo”
Wako dizzo mtawala
Sent using
Jamii Forums mobile app