Jamami, msiwe wepesi wa kusahau kuhusu kauli na matamshi ya huyu bwana mnaemtaka atoke huko aliko na aseme japo mawili machache katika kupambana na hii janga.
Naomba niwatahadhirihe tu kuwa akitoka mafichoni na kufanya mnachokitaka na ambacho ni wajibu wake kwa nafasi yake,tutaishia kusema ni bora tu angebaki huko aliko na zaidi tutabaki kusononeka tu katika nafsi zetu.
Kwa mtazamo wangu,mbali na uwezekano wa kutamka msiyoyatarajia,anaweza hata kuwatolea uvivu badala ya ku-address tatizo la msingi.
Hivyo, muacheni tu abaki huko aliko na sisi tujiongoze wenyewe ingawa kwa nafasi yake yeye ni mtu muhimu katika mapambano haya.
Muda utaongea.