Ndiyo! Where is Mr. President?
Mwenye habari kamili za alipo rais wa Tanzania atujibu haya maswali...
Anafanya nini huko alipo?
Je, yupo karantini au self lockdown?
Je, anaumwa? Kama ndiyo anaumwa nini?
Kama haumwi je yupo likizo? Kama ndiyo je ni unpaid leave?
Kama hayupo likizo je ni lini atarudi ofisini?
Je serikali yake ina mikakati gani ya muda mfupi na ya muda mrefu kukabiliana na kusambaa kwa Covid-19?
Je serikali yake ina mikakati gani ya kuwakinga wahudumu wa afya dhidi ya maambukizi ya Covid-19?
Je serikali yake ina mikakati gani ya kuboresha miundombinu, vifaatiba na huduma muhimu kwenye hospitali za umma?
Je serikali yake ina mikakati ipi ya kutoa nafuu ya kiuchumi kwa wananchi ambao hali zao zinazidi kuwa tete??