Vita ya Uchumi haijawahi kuwa nyepesi, Hayati Magufuli aheshimiwe



Hii statement hapa inakuvua uhalisia wako.

Ina maana unashindwa kabisa kutenganisha personalities za mtu na utendaji kazi wake?

1) Kupenda kusifiwa- anaweza kumzidi aliyebariki taasisi ya “Chawa wa Mama? Na mwana mtandao mashughuli wa “Boys 2 Men?

2) Kupenda baadhi ya watu kutoka kanda fulani - kwamba hapa amewazidi wengine wote waliomtangulia kukalia hicho kiti? Kabisa?!


Ni hatari kujifanya kipofu na kuchangia mjadala huku ukivutia upande wako ilhali dhamira yako sio safi kihivyo.
 
Kuna watu wanajiita chawa wa mama
 
Hamna hoja. Nilidhani huwa wanakuja na silaha kupora. Kumbe ni tamaa za viongozi wetu ndiyo zinasababisha haya yote? Sasa unalia nini?
Wakuu mnafikiri kwanini tunashidwa kuzalisha vyakujitosheleza na ziada, Hapa tuzungumzie mazao ya kimkakati na industry zinazohitaji capital na mobilization kubwa achana na single individual ambao scale yao ya uzalishaji haina impact kwa taifa. eg. Sukari, ngano, mafuta ya kula, hata nishati.
Yaani kila awamu makosa ni yale yale.

Nakili ya kwamba sisi wa Africa tunachangamoto zetu lakini si kwa level hizi, pia mimi mwenyewe sipendi kuona mtu analalamika tu na kuwatupia watu lawama kwa mambo ambayo ni wajibu wake yeye kuyatekeleza, ni ujinga kama sio upumbavu.

Lakini mbali na hizo changamoto tulizonazo kama wa Afrika, wajanja wanaishi na sisi humo humo wanatumia udhaifu wetu kama fursa kupitia uishawishi wa kidiplomasia na nguvu ya kiuchumi walionayo ni rahisi sana kuhadaa viongozi wetu, na kumbuka yupo madarakani under pressure anahitaji support kuendelea kubaki.

Na ukikataa wenzako wanakula ukitafakari unagundua hakuna ulichofanya maana ulichopigania wezako wanakigawa maisha yanaendelea ila wewe unakua umejiweka kwenye angle mbaya, na wakikuamulia wanakuchafua kwa propaganda ile iwe fundisho kwa wazalendo waliobakia(discourage). Yaani unakufa maskini na skendo juu.👇👇👇

Kwenye vita ya uchumi hawapandikizwi viongozi tu, kila sector ambayo ni potential kunakua na agent wao hasa hasa hizi sector ambazo moja kwa moja zinashikilia uchumi wa nchi mfano. Nishati, wafanyabiashara wakubwa wa bidhaa muhimu ie, vyakula. Sasa hawa kuna michezo hua wanaicheza kwa kufuata maelekezo kuhakikisha nchi haiwi stable katika uzalishaji at the same time wanalinda soko la bidhaa zao kutoka nje ya nchi ambako ndio kwa wenyewe(mabeberu) Kwahiyo wao wanarisha raia wao wanapata ajira kupitia mnyororo wa thamani sisi tunatumia kwa gharama kubwa tunaishia kurumbana vijiweni.


Vita vya kiuchumi achia warusi, wachina, Iran, NK , Venezuela at least Zimbabwe akiongea Nita muelewa.
Mbinu mbalimbali hua zinatumia Kulingana na aina(nature) ya nchi na level ya maendeleo na ushawishi ilipofikia nchi husika.
Namna USA wanavyod-deal na mchina au mrusi ni tofauti watakavyo deal na sisi huku. Inaonekana sisi sio stubborn saana hivyo haina haja ya kutumia nguvu kubwa.

Nb vita ya kiuchumi kati ya USA na China hata sisi huku tunahusika kwa maana maslahi yao mapana yaliyopo kwetu huku yako rehani. Hii kasheshe sisi tukiwa bado tunapambania masrahi mapana ya nchi yetu. Kumbe wezetu wana masrahi yoa mapana juu ya nchi yetu (ukanda wetu).
 
Hakuna cha vita vya uchumi wala nini roho ni mbaya tu ndiyo ilikuwa inamsumbua na uroho wa hela maana alihakikisha anavunja mikataba waliyoingia wenzake ili apige yeye.
 
Hamna hoja. Nilidhani huwa wanakuja na silaha kupora. Kumbe ni tamaa za viongozi wetu ndiyo zinasababisha haya yote? Sasa unalia nini?
Wewe hata walichoongea hao viongozi kwenye hizo clip huelewi kitu. Uchawa umekuzidi sana. Acha upuuzi na kujitoa akili. Tumia utimamu wa akili zako.

Hivyo ulivyo ndio tofauti ya "wale" na wewe.

Hamna mtu anaelia hapo, Nyerere kaongea na vicheko kaweka. JPM kaongea sijaona kalia.

Kwenyejadala watu wanaeleza ukweli wa mambo yalivyo, wewe u akuja kulaumu viongozi kua wanatamaa.

Wewe unaweza muachaniza hata mkeo akaliwa na wadau na u kumlaumu mkeo kua anatamaa bila kuangalia deep inside Kwa nini imekua hivyo.

Tumia akili Yako acha uchawa.
 
Nice analysis
 
Nice view
 
Uchambuzi murua
 
Umeeleweka vizuri ingawa kuna wachache hawawezi kukuelewa
 
Wajinga watabaki kuwa wajinga unajua kwanini alimrudisha Rostam ? Mambo yalikuwa hayaendi. JPM alidhani nyerere alikuwa mjinga kutopendelea kabila lake bali kuteua watu kutokana na uwezo wao. Baada ya JPM mama ameiga sasa kajaza watu wa visiwani na wavaa makobazi. Na Rais atakayekuja nae ataendelea na mwendo aliouanzisha JPM. Viongozi wa kiafrika wanafikiria leo lakini hawafikirii kesho. Hakuna nchi ambayo haina amani ilipata uhuru kwa njia ya amani. Nyerere alikuwa na mapungufu lakini hakuna Rais mzuri kuliko yeye na hatokaa atokee. Alikuwa kati ya watu wachache waliokuwa exposed angeweza kutumia ujuzi wake kutunyonya kama alivyofanya Jomo Kenyata Kenya.
 
Hakuna rais aliekuwa na ukabila katika serikali yake kabla ya 2015. JPM ndio alioanzisha ukabila ndani ya serikali na Mama ndio anaendeleza. Na kama hakuna kitakachofanyika Rais atakaefuata atafanya hivyo hivyo. Tuangalie kijijini kwa Mkapa, Nyerere, Mwinyi na Kikwete. Halafu tuje tuangalie Mkoa aliotoka JPM. Baada ya hapo tuangalie Rais gani aliyetaka kugeuza wilaya aliyotoka kuwa mkoa ? Rais gani aliyetaka kuweka mbuga ya wanyama kwao ? Rais gani aliyejenga uwanja wa ndege kwao ? Rais gani aliyejenga hospitali ya rufaa kwao ? Rais gani aliyejenga Ikulu kwao ? Rais gani aliyeagiza kufungua tawi la CRDB kwao ? JPM alikuwa Rais wa wasukuma na sio wa watanzania. Hii ipo wazi kabisa na mbaya zaidi ukitumia hii system unapata wanafiki wengi kama H.K. Hata ukiwa na biashara ukimuweka ndugu yako haogopi kuiba na hata ukiambiwa anaiba hauwezi kuamini kwa sababu ni ndugu. Na kaa chini uangalie mama anaendeleza alipoishia JPM mbadala wa chato ni kizimkazi. Nchi inapasuka vibaya sana na sijui nani atairudisha Tanzania ya umoja.
 
Chato wanakaa Watanzania au warundi?
 


Too biased.

Kwamba hujui angalau kila mkoa aliotokea Rais wa nchi hii na mikoa mikuu ya nchi kuna Ikulu ndogo za Rais?

Kwamba Magufuli kwa kauli yake aliagiza CRDB kufungua tawi Chato?! Una akili timamu kweli?

Kwamba kabla ya 2015 kwenye utumishi wa ummah hakukua na upendeleo wa kikabila/kikanda? Una hakika?

Wakati wa Nyerere wale wanajeshi zaidi ya asilimia 50 kutoka ukanda wake ilikua ni bahati mbaya ama kwamba wao ndio majasiri sana wa kukaa jeshini?

Kwa Mwinyi hata usiseme sana nenda Loliondo bado alama yake na leo yupo bado bara na visiwani. Huna macho?!

Mkapa? Hapa ukitaka kuifahamu vizuri definition ya Selfishness, msome vizuri.

Kikwete wala sihitaji kukumbusha style yake na wenzake ya wanamtando aka Boys 2 Men. Hapa ndio kulizaliwa Chama jipya Chukua Chako Mapema.

Magufuli kuwakumbuka watu wa kanda ya ziwa na kuwapa vipaumbele sio dhambi maana kwa kiasi kikubwa walisahaulika kwa kisingizio eti Nyerere aliwahi kuonya kutowapa uongozi watu wa kanda hiyo (waliokuwepo enzi hizo wanasema alikua anawasema watu wa Kaskazini)

Rais Samia anafuata nyayo za watangulizi wake na mfumo ndivyo ulivyo tangu enzi.

Wakati wa ukoloni wakoloni waliwapendelea zaidi watoto wa wafalme (machifu) na ndugu zao kwa kuwapa elimu na majukumu na hata baada ya kupata Uhuru wa kwenye makaratasi Nyerere hakufanya tofauti sana haswa pale alipokoswakoswa kupinduliwa akakimbilia Kigamboni, aliwakumbuka ndugu zake na kuwajaza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…