Vita ya Ukraine - Urusi ina hadhi ya kuziangusha serikali za Ulaya na Marekani

Naomba orodhesha mafanikio ya Urusi toka avamie ukraine., andika kwa namba tafadhali, Umesikia ile habari ya majeshi 1000 ya urusi juzi kuzamishwa kwenye ule mto wakijarib kuvuka kuingia ukrain?

Vipi kuhusu Finland na Sweden putin alisema wakijiunga na NATO atapiga nuclear ulaya, sasa jana rasmi wamepeleka maombi NATO, hizo nuclear ziko wapi?
 
Kwani Finland na Sweden tayari ni wanachama wa nato? maajabu makubwa
 
Safi sana mkuu
 
mtu mwenye msimamo ni yule anaejitegemea, kama wewe ni tegemezi huwezi kuwa na msimamo wenye maana. Wazungu wamekosana sana na kiongozi au nchi inayoelekea kwenye kujitegemea. Wanapenda nchi na kiongozi ombaomba kwao maana watautumia udhaifu huo kupitisha agenda zAO ZENYE MANUFAA KWAO. usikubali kupewa msaada au mkopo na kuupeleka sehemu isiyozalisha kama vile kununua madawati, kujenga madarasa, kununua chakula, nk, ukifanya hivyo utaendelea kuwa tegemezi na ombaomba milele. hata marekani wanakopa China kwa riba ndogo na kukopesha wengine kwa riba kubwa, wanakopa na kwenda kuwekeza kwenye uzalishaji wa silaha za kivita halafu wanauza silaha hizo kwa wengine kwa bei kubwa.

Misaada yenye maslahi kwetu ni ile itakayokwenda kuwekezwa kwenye maeneo ambayo yatazalisha zaidi kama vile kwenye kilimo, kuonyeza thamani ya madini yetu, au kuboresha vivutio vyetu vya utalii na kuvitangaza. Tusikope kujenga darasa au kununua madawati au kulipana mishahara. Siku moja nilitembelea kijiji kimoja kule marekan nikakuta shule ya msingi ya serikali imeezuliwa na upepo wanafunzi wanasoma kwenye shule ya hivyo kwa muda mrefu tu, nikashikwa na bumbuazi na kwikwi. Wenzetu wanajali uzalishaji tu sio huduma kwa wananchi.


Alichokuwa akifanya JPM ndicho wazungu wanachokifanya kwao na kwa wananchi wao
 
Lengo la Urusi sio kuiteka Ukraine, kama lengo lingekuwa hilo angeshaiteka kwa siku tatu tu. Lengo lake kuu sio kuisambaratisha Ukraine bali kumaliza uwezo wake wa kijeshi anaotumia kuwapiga wale wazaozungumza Kirusi wanaotaka kujitenga. Anahakikisha kuwa analenga zana na vituo vya kijeshi tu na zile njia zinazotumika kuingiza silaha kutoka NATO baaasi, hii ndio inayosababisha achukue muda mrefu kufanisha hilo bila ya kuiharibu Ukraine. Kosa alilofanya Voladymil Zelensky ni kuwatumia raia wake kama askari kwa kuwapa silaha wapigane na Urusi, hii ndio inayosababisha Russia ipige hata majengo ya kiraia wanamoishi watu wa kawaida waliopewa silaha.

 
Hata wazungu ni wajinga, kwenye hili hesabu zao hazitakwenda vizuri. Wameshindwa kutofautisha kati ya Urusi na Afghanstan, au syria, au Iraq au Somalia au Libya

 
Sasa mbona mizigo ya silaha inaendelea kumiminika Ukraine? Nakumbuka siku ya kwanza ya uvamizi alisema Donbas ishakuwa huru watu wa miji ile wakasherehekea na kupeperusha bendera imekuwaje tena saivi bado anapapatua na alishatangaza kabla kwamba ni huru?

Kama mpango sio kuiteka Ukraine kule Kyiv ambako alipata kichapo na kurudi zake Donbas alienda kufanya nini hasa? Kwanini tuliambiwa Kyiv imezingirwa na akawataka jeshi la ukraine lijisalimishe na mpaka kutoa masaa mara kadhaa ivi putini alipatwa na nini hasa kule Kyiv, em kokomoka tujue alichofata lakini kwanini alichomoa baadae na yale masaa yalipita na kupitiliza hadi leo ni ipi adhabu yake baada ya majeshi ya Ukraine kukataa kusarenda masaa yalipoisha?

Je unayo habari ya Finland na Sweden?
 
[emoji91][emoji91][emoji91] Vice-President of the European Commission Timmermans: it turned out that a number of large European gas companies opened accounts with Gazprombank, through which payments made in euros are converted into Russian rubles, this is not normal[emoji91][emoji91][emoji91]
 
Ni ngumu kujua NATO imepanga nini juu ya Russia, yeye ndo mwenye kauli ya Russia ashinde au asishinde. Hivi sasa russi amenza tumia laser weapons, hypersonic missiles n.k hii inaashiria pale maji yamekuwa kina kirefu kwake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni vile russia vyombo vya habar kote vimepigwa pini, la sivyo tungesikia mengi yanayofukuta huko russia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
alichofuata kyiv ilikuwa kusambaratisha miundombinu yote inayotumika kuchochea vita kama maghala na viwanda vya silaha, njia za kurukia ndege, miundombinu ya mawasiliano ili iwe vigumu kuratibu vita. alipofanikisha hilo hakuona umuhimu wa kukaa kule tena, maana lengo sio kumkamata Rais Zelensky bali kudhoofisha nguvu za kijeshi za Ukraine na washirika wake. Kama Ukrane na NATO wangekuwa na ubavu wangeifukuza Urusi pale Mariupol na kuwaokoa askari wao waliokwama kwenye kiwanda cha chuma. Kumba pale kwenye kiwanda kuna askari wengi sana wa kigeni (US, UK, Canada) na waukraine wenyewe. Kama NATO na Ukraine ingekuwa na uwezo basi wangewaokoa watu wao pale, lakini wameshindwa hadi askari wale wakajisalimisha kwa majeshi ya urusi,
 
Upo sahihi kabisa, na sio vijana tu, hata watu wazima, ndo maana china, nchi za falme za kiarabu, russia wenyewe n.k wanakimbilia saaana kula bata la nchi za Ulaya na US.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya ndege kudunguliwa akaanza kurusha makombora ya masafa marefu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je, nguvu ya kijeshi ya Ukraine sasa imedhoofika? kama lengo ni kuvuruga miundombinu kwanini viongozi wa ulaya na marekani hutembelea Kyiv muda wowote huwa wanatua kwenye viwanja vipi? niliwaona uropean union, boris johnson, katibu mkuu wa umoja wa mataifa, mke wa rais wa marekani na wengine hawa wote walipitia wapi?

Ivi hufahamu kama hayo mateka kila upande yako? kwa nini unajitoa fahamu na juzijuzi wamebadilishana? lakini Mbona Russia kama ina nguvu ilishindwa kuwaokoa wanajeshi wao karibu 1000 walikwama na kufa kwenye ule mto waliokuwa wakivuka kuingia Ukraine ukraine? kwanini walishindwa kuwaokoa? Lakini kwanini russia hawajamuokoa yule mwanajeshi wao aliefunguliwa kesi ya mauaji Kyiv? au tuseme urusi haijali raia wake?

Hili suali la putin kabla kutangaza uhuru wa majimbo ya Donbas na raia kusherehekea ule uhuru umefikia wapi naona bado ameganda Donbas kuna nini? na kwanini hasa imefikia leo mwezi 3 na tuliambiwa russia ni giant kwneye vita na silaha kali zaidi duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…