Vita ya Ukraine - Urusi ina hadhi ya kuziangusha serikali za Ulaya na Marekani

Vita ya Ukraine - Urusi ina hadhi ya kuziangusha serikali za Ulaya na Marekani

Ujerumami haipendi kushiriki kwenye vita hii kwa njia yoyote lakini inalazimishwa na Marekani na uingereza ili ishushe uzalishaji hatimae ishushe kiuchumi ndani ya EU. Baada ya kuondoka kwa UK kwenye EU kushindwa kuusambaratisha umoja wa Ulaya Sasa wamekuja na mbinu hii ya Ukraine. EU isipokuwa makini itasambaratika kabisa.
yaan unahis hao US na UK hawaoni idad ya maadui inavyoongeza huku NK , kule India , hapa China , huko Iran , Humu Venezuela , Huko Syria bila kusahau URUSI hlf waanze kushushana wao km wao , hv unazani wana akili km zako hao wazungu ?
 
Tena Russia wamesema wanasubiri kura ya maoni ya lile jimbo la Mashariki (wakikubali kujitenga na Ukraine, watakuwa wamefanikiwa lengo lao, wataacha kupigana), lakini ukweli Urusi mambo yapo shingoni, anatafuta mlango wa kutokea bila aibu.

Ni vigumu sana Russia yenye uchumi dhaifu kiulinganifu, kuwashinda wenzake wengi wenye uchumi mzuri, walioungana.

Ndege za Urusi zilizotunguliwa, zimeonekana kutumia GPS za kawaida za kusafiria kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha kuhudumia ndege zake za kivita. Kwa sasa ndege zake kila zikiruka zinadunguliwa. Wamebakia tu kurusha makombora, lakini siyo kuruka angani kama mwanzo.
Alisikika mkaazi mmoja wa manyovu aliyelewa kidogo!! akichambua vita ya Ukraine
 
Kwanza anatakiwa aelewe kwamba vyanzo vyote vya habari zinazohusu vita vya Ukraine vimedhibitiwa na nchi za MAGHARIBI (NATO) kwahiyo habari nyingi eti za kushindwa Russia ni propaganda za NATO !! Naye alishawaambia na anarudia Mara kwa Mara kwamba atakayejiingiza kwenye hiyo vita atapiga nyumbani kwao within half an hour atavuruga Nchi yao kiasi ambacho hawajapata kuona katika maisha yao !!

Point, hii vita inaenda kuwangusha Biden, Boris na chancellor wa ujerumani ktk box la kura, hili anguko lipo wazi
Silaha wanazopeleka zinaangamizwa kabla hazijatumika. Kama NATO ingekuwa inashinda vita huko Ukraine wazingeongelea habari za kuongeza misaada, kuongeza vikwazo, kuzilaumu China, India, na ujerumami. Hali sio nzuri kwao ila wamebana taarifa zao za kushindwa zisitoke nje,
 
unaandika ukwel ila ttzo 2po vzr kwny kuandik kuliko utendaj kituko ni kuwa hata ww ukipewa fursa ya kuwatumikia wananchi utaishia kulitumikia kwanz tumbo lako , UJINGA bado kamudu kuwa adui wa kwanza kwa mtu mweusi
Kutumikia tumbo ndio upumbavu mkubwa binadamu anaoufanyia dunia hii. Ulizaliwa bila kitu na utazikwa bila kitu, ni heri ya yule aliyepanda japo mti mmoja wa kivuli dunia itamkumbuka vema kuliko aliyehangaika na matumbo ya ukoo wake TU.
 
kwan West ndio waliovamia Ukraine ? siku ukivamiwa utawashukur tu uwepo wao dunian
Hutaki kufahamu ni kwanini Ukraine imevamiwa na Russia lakini unafahamu ni kwanini Cuba inavamiwa na USA na Palestine inavamiwa na Israel, DRC inavamiwa na Rwanda, nk. Una safari ndefu sana.
 
lkn si mlisema RUSSIA ni superpower ? nan huyo hamwogopi superpower mpk amsingizie
Kama NATO imeshindwa Afghanistan isiyokuwa na mafuta, gesi Wala nguvu na nuclear itaiweza Russia yenye kila kitu? Kusema Russia itashindwa na NATO ni ndoto TU za asubihi. Russia ilijipanga kwa muda mrefu kwenye hili. Sasa hivi kazuia mafuta, gesi na chakula kwenda nchi za NATO hadi zilipe kwa Rubble. Vikwazo walivyoweka ni eye opener kwa wananchi wao kuhusu upuuzi wa viongozi wao.
 
Hizo ni ramli tuu mlisema pia raisi wa ufaransa atakosa uraisi akapata kwa kishindo na issue ya Ukraine ndio ilimpa kura nyingi

Wazungu wengi hawaipendi urusi wanaipenda Ukraine hivyo wanaunga mkono juhudi zote za kuisaidia Ukraine..

Hivyo tuu jifanye unaipinga Ukraine alafu kagombee

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
Putin kidume, Scholz ameanza kuangushwa huko ujerumani:

Kama hujui Kiingera sikiliza hapa mpaka mwisho:
 
Wamarekani na wazungu wengi hawajui kile serikali zao zinachokifanya kwenye mataifa mengine lakini safari hii ni tofauti sana, wameamza kuufahamu upuuzi wa wanasiasa wao. Na hii ni baada ya maisha Yao kuguswa na kupanda kwa gharama za maisha kunakotokana na uhaba wa ngano, mafuta ya kupikia, gesi ya kupikia, petrol, umeme na wakimbizi wengi ambao ni wazungu wenzao kwenye mitaa Yao.

Wazungu wengi wengi ndio kwanza wanagundua kuwa kumbe nchi zao zinakopa ili kusaidia kutoa misaada kwa nchi nyingine. Wanagundua kuwa kumbe Kodi zao hazitumiki vizuri.

Vita hii inaweza kuusambaratisha umoja wa Ulaya EU kama hawatakiwa makini, vita hii inaweza kumuondoa madarakani Joe Biden, Boris Johnson na wengine kama yule chancellor wa ujerumami.

Vikwazo vyote dhidi ya Urusi vinarudi kwenye nchi zao na watu wao, hii haijawahi kutokea kwao huko nyuma wakati wanaziwekea vikwazo nchi nyingine kama Iran, somalia, Ethiopia, north Korea, au Venezuela.

Wazungu lazima watalazimika kuachana na vita hii maana baadhi ya washirika wa NATO wamegundua kuwa vita hii inanufaisha makampuni ya silaha ya kimarekani .
Kwa nini huongelei Russia kuondoa majeshi yake kwenye ardhi ya Ukraine, mbona unaongea kishabiki tu.
 
Wazungu hawampendi mtu. Wale ni monsters wa rasilimali. Pale Ukraine kuna natural gas, kuna coal, kuna chuma, kuna mafuta, wazungu wanataka hizo rasilimali.
Pia ni eneo muhimu kiusalama ili kumthibiti Urusia.
Ingewezekana Ukraine ingefanywa pori tupu lisilokuwa na watu ili kuwa kama DMZ(Dimilitarized zone kati ya Urussi na Marekani akiwa na vibaraka wake wa Ulaya Magharibi.
Hiyo ni bangi ya milima Usambaa inaongea.
 
Hutaki kufahamu ni kwanini Ukraine imevamiwa na Russia lakini unafahamu ni kwanini Cuba inavamiwa na USA na Palestine inavamiwa na Israel, DRC inavamiwa na Rwanda, nk. Una safari ndefu sana.
mkuu tupo current tunalenga kupunguza huu ujinga in future , kuunga mkono , uvamiz ni kukubali uvamiz uendele , hakuna kosa halijawai kufanywa ila hatuez tokomeza kwa kuunga mkono kosa kila wapo waliokosea pia
 
Kama NATO imeshindwa Afghanistan isiyokuwa na mafuta, gesi Wala nguvu na nuclear itaiweza Russia yenye kila kitu? Kusema Russia itashindwa na NATO ni ndoto TU za asubihi. Russia ilijipanga kwa muda mrefu kwenye hili. Sasa hivi kazuia mafuta, gesi na chakula kwenda nchi za NATO hadi zilipe kwa Rubble. Vikwazo walivyoweka ni eye opener kwa wananchi wao kuhusu upuuzi wa viongozi wao.
nimeuliza tu kuwa si tulikubaliana Russia ni superpower ?
 
Macron ndiye anayepigia chapuo nchi za EU ziachane na manunuzi ya gesi na mafuta ya Russia. Hilo lingefanyika hiyo vita ingeisha kesho saa nne asubuhi.
Lakini ushafuatilia misimamo ya Macron katika vita hiyo ilivyo? Angalia kwa karibu zaidi, utaona utofauti wake na wengine waliomo NATO.
 
Wewe akili ndogo shabikia siasa uchwara za aina ya jiwe tu nchini kwako, hizo za Ulaya na Marekani zinahitaji akili kubwa kuzielewa.
Umeongea ukweli kabisa angekuwepo Angela Merkel asingekubali huu upuuzi wa maamuzi ya hisia ambayo yangeimuza ujeremani nchi anbayo ni heavily dependant wa nishati za Russia; chini yake US kuweka military base Ukraine in kitu ambacho kisingewezekana under her watch kwa sababu anaelewa athari zake kwa uchumi wa nchi yake na bara.

Hawa viongozi wengine wa EU ni US puppets bila ya Mrs Merkel na huu mziki unawaumiza kweli uzuri wao ni watu wa kujifunza. Mfano U.K. washatumia zaidi ya £20 billion katika miezi mitatu kama subsidisation ya kupambana na inflation ya energy sector alone sasa hivi hizo hela zimezua mjadala kumbuka hawa wana reserve zao za mafuta ya kutosha North Sea wakiamua kujitegemea inapobidi they don’t have to import, na wana storage za miezi sita dunia ikikosa mafuta kabisa ya kuwatosheleza bila ya kuagiza mafuta. Achilia mbali North Sea ambayo na yenyewe reserve inauwezo wa kuwahudumia kati ya miaka 35-40 peke yao wasipo export (hayatumiwi sana kwa sababu ni Brent crude, crude zinatofautiana ika ukisikia hilo neno jua ni mafuta ya U.K. ambayo ni very high quality, kama ilivyo kwa mafuta ya Uganda) sasa ukiona watu wanazungumzia Tanzania kununua mafuta ya Uganda elewa ni wazimu tu huo. Vinginevyo utauziwa litre tsh 5000 maana ni very high quality.

Upuuzi upo African Union as a continent we don’t know how to protect our interest sisi tukifika UN tunabariki kila sanctions hatuna agenda za pamoja na wala atujifunzi madhara ya maamuzi.

Sasa hivi kinachoendelea kwenye hizi sanction AU walitakiwa kuitisha crisis meeting na kuja na agenda ya pamoja to save the continent woes. Wawarudie hao mabeberu wao ndio volumes kubwa za trade za mafuta na nchi zilizo kwenye sanctions so kuacha kwao kununua ndio muhimu kuwaumiza kiuchumi na wana mitigating strategies tayari za kupambana na uhaba wa mafuta.

Sisi waafrica hatuna shida na siasa za Arab-Israel wala ideological wars za West and East na hatuna impact ivyo; so kwenye hizi sanctions watutoe tununue mafuta popote kwa bei rahisi vinginevyo wanatubebesha mzigo mkubwa kuliko uwezo wetu wa kiuchumi wao wana resources na mitigating strategies ambazo sisi hatuna.

Somo ni nini hapo AU ni chombo tu ambacho kipo lakini hakina agenda za pamoja; haya mambo uwezi kukuta EU ambao wana assess risk zao za pamoja kabla ya kuamua wakati protecting their interest is at foremost.
 
mkuu tupo current tunalenga kupunguza huu ujinga in future , kuunga mkono , uvamiz ni kukubali uvamiz uendele , hakuna kosa halijawai kufanywa ila hatuez tokomeza kwa kuunga mkono kosa kila wapo waliokosea pia
Ukiona NATO kila siku ina vikao vya kuchangia na kuweka vikwazo vipya ujue hali zao sio njema. Russia inayo mengi ambayo haijayafanya kwa NATO. Russia ni technolojia hata ya kuzima satellites zote za nchi za NATO. Kuishinda Russia ni gumu kuliko ngamia kupita tundu la sindano.
 
Wewe akili ndogo shabikia siasa uchwara za aina ya jiwe tu nchini kwako, hizo za Ulaya na Marekani zinahitaji akili kubwa kuzielewa.
akili yako pia inahitaji vipuli. Angalia kwa karibu utagundua kuwa waanzilishi wakuu wa NATO ni zile nchi zilizokuwa na makoloni mengi duniani. Ni zile nchi ambazo zilikutana Berlin kugawana makoloni na kuchora mipaka ya Afrika ili wagawane makoloni kwa amani chini ya Chancellor Bismarck ili kupata malighafi ya bure, nguvukazi rahisi, na masoko ya kuuza bidhaa zao za viwandani. hadi leo hii mataifa hayo bado na shida zilezile za malighafi, cheap labour, na masoko ya kuuza bidhaa zao, lakini mara hii wanatumia majeshi ya NATO kuvipata vitu hivyo kwenye nchi zenye rasilimali nyingi zenye viongozi wanaojitambua. Wamefanya hivyo Sudani, Syria, Yemen, Iraq, Libya, DRC Congo, Afrika ya kati, Yugoslavia, Venezuela, nk. Ukrane inaponzwa na gesi, chuma, uranium na ardhi yake nzuri kwa kilimo. Mabeberu wanaitaka. Siku Urusi ikianguka basi hali ya dunia itakuwa mbaya sana.
 
Wamarekani na wazungu wengi hawajui kile serikali zao zinachokifanya kwenye mataifa mengine lakini safari hii ni tofauti sana, wameamza kuufahamu upuuzi wa wanasiasa wao. Na hii ni baada ya maisha Yao kuguswa na kupanda kwa gharama za maisha kunakotokana na uhaba wa ngano, mafuta ya kupikia, gesi ya kupikia, petrol, umeme na wakimbizi wengi ambao ni wazungu wenzao kwenye mitaa Yao.

Wazungu wengi wengi ndio kwanza wanagundua kuwa kumbe nchi zao zinakopa ili kusaidia kutoa misaada kwa nchi nyingine. Wanagundua kuwa kumbe Kodi zao hazitumiki vizuri.

Vita hii inaweza kuusambaratisha umoja wa Ulaya EU kama hawatakiwa makini, vita hii inaweza kumuondoa madarakani Joe Biden, Boris Johnson na wengine kama yule chancellor wa ujerumami.

Vikwazo vyote dhidi ya Urusi vinarudi kwenye nchi zao na watu wao, hii haijawahi kutokea kwao huko nyuma wakati wanaziwekea vikwazo nchi nyingine kama Iran, somalia, Ethiopia, north Korea, au Venezuela.

Wazungu lazima watalazimika kuachana na vita hii maana baadhi ya washirika wa NATO wamegundua kuwa vita hii inanufaisha makampuni ya silaha ya kimarekani .
Huo ndio ukweli vita hii ni ya tofauti sana.
 
Back
Top Bottom