Pia wizara haitoi mwanya kwa wajasriamali wadogo wanaitaka kuingia ktk biashara hiyo rasmi ndio maaana huishia kufanya kazi kinyemela bila hata kulipa kodi..
Mfabo masharti ya leseni ya utalii ni magumu saana ya kuwa na idada ya magari 4x4 na dola 2000 kama ada ya TALA kwa mwaka.
Walau kungekuwa na categories zaidi ili kutoa mwanya kwa wanaotaka kuanza biashara hiyo.
Hii ni Kweli
Juzi tu Waziri wa Mali Asili aliombwa hili na akaahidi kutoa majibu kabla ya Christmas
Ila Christmas imepita na majibu hakuna, sijui Faru John anamsumbua? [HASHTAG]#farujohn[/HASHTAG]
Apongezwe Mkuu wa Mkoa wa Arusha na alisaidia kumwomba waziri aangalie hili
Hii ni Kweli
Juzi tu Waziri wa Mali Asili aliombwa hili na akaahidi kutoa majibu kabla ya Christmas
Ila Christmas imepita na majibu hakuna, sijui Faru John anamsumbua? [HASHTAG]#farujohn[/HASHTAG]
Apongezwe Mkuu wa Mkoa wa Arusha na alisaidia kumwomba waziri aangalie hili
Sekta ya utalii Tanzania bado haijapata watu muhimu wenye kufahamu namna ya kuipata tija inayotakiwa ipatikane.
Huo ni vichekesho kuona kuwa kwenye siku ya utalii ya Tanzania huko Ulaya, sisi tunaotangaza bia na konyagi, kama vile tumeumbiwa ulevi.
Kenya pamoja na ukabila wao wa chini kwa chini, siku ya utalii huhakikisha na inapambwa na kikundi chao cha ngoma, kinachogharamiwa na serikali kuu.
Wakenya wanakuwa wamoja kwenye kuiuza nchi yao, sisi tunatazama ubinafsi wetu na kufaidika kwetu badala ya kujikita katika kuitangaza Tanzania moja kiutalii.
Miaka inakwenda haya makosa yetu makubwa wala hatujisumbui katika kuyapatia suluhisho la kudumu.
Wizara ya maliasili na utalii inapewa watu ambao hawana mguso wa kimataifa ambao utaifanya Tanzania iheshimiwe kupitia utalii. Wale wanasiasa wabinafsi na wenye viburi vya usomi wao ndio wanaopokezana nafasi ya juu kabisa.
Rais John Magufuli ambaye wazo la maendeleo kwake siku zote linaungwa mkono, anayo nafasi ya kukaa na wenye kuufahamu utalii, lakini wanafanyiwa kauzibe na wachumia tumbo wachache.
Hawa watu watamueleza ni namna gani mamlaka za utalii zinavyojitambulisha zenyewe kimataifa pasipo kuitanguliza kwanza Tanzania.
Tanzania itakuwa unaburuzwa na Kenya kwenye michakato ya kupata watalii wengi kila mwaka, kwa sababu Kenya inahakikisha utamaduni wao unakuwa ni sehemu ya tangazo la utalii.
Kutangaza konyagi na bia kwenye matamasha makubwa ya kiutalii ni ukosefu mkubwa wa ubunifu, na kwa hali hii sio ajabu tukabakia kuwa watu wa kutazamana na kutafutana ubaya kwa sababu tu ya kufikiria riziki zetu badala ya ile riziki kubwa ambayo ni pato la Taifa kupitia utalii.
nili jaribu kufanya research ndogo kuhusu utalii wa ndani nilicho baini ni kwamba wa Tanzania wengi hatujui vivutio tulivyo navyo na kuna baadhi ya watu nilio jaribu kuuliza wanazijua mbuga zilizopo kwenye ule wimbo wa shule ya msingi kwa upande wa historical sites wanao zifahamu kati ya watu 10 basi ni 1 au w2 na kiuhalisia ule wimbo umaharibu kiasi kikubwa kama 80% ya wa Tanzania si watoto kwa wa kubwa.....nacho taka kusema ni hivi tuwafanye wa Tanzania waweze kujua vivutio vyao vya utalii ili hata wanao enda out of this country wa weze kueleza vizuri the beauty of Tz.....kwa sababu tuna tangaza kuhusu Serengeti,Ngorongoro na Mt.Kilimanjaro maana yake tuna pata watalii wana panda milima na mbuga za wanyama ila watalii wa historical sites tumewasahau utalii una uwanja mpana ila nafikiri viongozi wenye dhamana hawana passion na sector zao as if wapo kwa maslahi yao na pia tu ondoe intrest za kimikoa,kikanda tuhubiri kuhusu TZ nasio ukanda fulani huwezi kupandisha pato la utalii kwa Serengeti,Ngorongoro na Mt.Kilimanjaro pekee try to balance .......
Mkuu unaweza kutujuza mwamko aliokuja nao Kigwangalla kwenye sekta ya Utalii....Nampongeza Waziri Kigwangala amekuja na mwamko mpya na anaweza kufanya mageuzi makubwa
Mkuu unaweza kutujuza mwamko aliokuja nao Kigwangalla kwenye sekta ya Utalii....
Mikakati gani amekuja nayo.?