Vivutio vya utalii Tanzania na faida za utalii wa ndani

[HASHTAG]#FARUJONN[/HASHTAG]

Tourism: Tourism ilikuwa njia rahisi nchi kupata forex nyingi sana

Matokeo yake serikali imeshindwa kuchochea ukuaji wa utalii

A - Matangazo mengi (adverts)

B- Landing fee na Jet fuel kupunguza bei ili ndege nyingi zije direct Tanzania na bei za ticket zitapungua
Kununua ndege pekee haitoshi....Bado ATCL italipa landing fee na bado bei ya mafuta ni juu, ATCL hawataweza kutoa cheap tickets

C - VAT za ghafla (Destination inakuwa ghali sana) na wakati bado miundo mbinu ni duni..Why?

D - Kuboresha sehemu na makazi ya watalii matajiri--- bado
 
Pia wizara haitoi mwanya kwa wajasriamali wadogo wanaitaka kuingia ktk biashara hiyo rasmi ndio maaana huishia kufanya kazi kinyemela bila hata kulipa kodi..
Mfabo masharti ya leseni ya utalii ni magumu saana ya kuwa na idada ya magari 4x4 na dola 2000 kama ada ya TALA kwa mwaka.

Walau kungekuwa na categories zaidi ili kutoa mwanya kwa wanaotaka kuanza biashara hiyo.

Hii ni Kweli

Juzi tu Waziri wa Mali Asili aliombwa hili na akaahidi kutoa majibu kabla ya Christmas

Ila Christmas imepita na majibu hakuna, sijui Faru John anamsumbua? [HASHTAG]#farujohn[/HASHTAG]

Apongezwe Mkuu wa Mkoa wa Arusha na alisaidia kumwomba waziri aangalie hili
 
Majibu bado hayajatoka hadi leo au?
 
Hii ni Kweli

Juzi tu Waziri wa Mali Asili aliombwa hili na akaahidi kutoa majibu kabla ya Christmas
Ila Christmas imepita na majibu hakuna, sijui Faru John anamsumbua? [HASHTAG]#farujohn[/HASHTAG]
Apongezwe Mkuu wa Mkoa wa Arusha na alisaidia kumwomba waziri aangalie hili

Yawezekanai, FaruJohn anasumbua ila mashaka kama kweli yeye anaweza kutoa majibu au hadi akae na jopo lake!!! Japo TATO nao wameoneka kutokuwa na msaada sana, au vinginevyo kuwatumia umoja wa maguides kulisemea hili hadi lipate ufumbuzi!!!!
 
Wakenya wanafanya kazi nzuri ya kutangaza utalii wetu kuliko sisi wenyewe.
Saa nyingine nasema waache wafaidi maana sisi tumelala.
 
Tunaendelea kusinzia

UK.jpg
 
Sekta ya utalii Tanzania bado haijapata watu muhimu wenye kufahamu namna ya kuipata tija inayotakiwa ipatikane.

Huo ni vichekesho kuona kuwa kwenye siku ya utalii ya Tanzania huko Ulaya, sisi tunaotangaza bia na konyagi, kama vile tumeumbiwa ulevi.

Kenya pamoja na ukabila wao wa chini kwa chini, siku ya utalii huhakikisha na inapambwa na kikundi chao cha ngoma, kinachogharamiwa na serikali kuu.

Wakenya wanakuwa wamoja kwenye kuiuza nchi yao, sisi tunatazama ubinafsi wetu na kufaidika kwetu badala ya kujikita katika kuitangaza Tanzania moja kiutalii.

Miaka inakwenda haya makosa yetu makubwa wala hatujisumbui katika kuyapatia suluhisho la kudumu.

Wizara ya maliasili na utalii inapewa watu ambao hawana mguso wa kimataifa ambao utaifanya Tanzania iheshimiwe kupitia utalii. Wale wanasiasa wabinafsi na wenye viburi vya usomi wao ndio wanaopokezana nafasi ya juu kabisa.

Rais John Magufuli ambaye wazo la maendeleo kwake siku zote linaungwa mkono, anayo nafasi ya kukaa na wenye kuufahamu utalii, lakini wanafanyiwa kauzibe na wachumia tumbo wachache.

Hawa watu watamueleza ni namna gani mamlaka za utalii zinavyojitambulisha zenyewe kimataifa pasipo kuitanguliza kwanza Tanzania.

Tanzania itakuwa unaburuzwa na Kenya kwenye michakato ya kupata watalii wengi kila mwaka, kwa sababu Kenya inahakikisha utamaduni wao unakuwa ni sehemu ya tangazo la utalii.

Kutangaza konyagi na bia kwenye matamasha makubwa ya kiutalii ni ukosefu mkubwa wa ubunifu, na kwa hali hii sio ajabu tukabakia kuwa watu wa kutazamana na kutafutana ubaya kwa sababu tu ya kufikiria riziki zetu badala ya ile riziki kubwa ambayo ni pato la Taifa kupitia utalii.
 
Tuko busy na TL kwa sasa hayo mengine yatasubiri
 
Knjaro.jpg

Dar es Salaam. Tanzania na Mlima Kilimanjaro imeorodheshwa kwenye tuzo za vivutio bora vya utalii zinazotarajiwa kutolewa Desemba.

Tuzo hizo zinazoandaliwa na Shirika la World Travel (WTO) ambazo zinatolewa kwa mara ya 24 mwaka huu, zimeiweka Tanzania kwenye kipengele cha nchi bora kuzitembelea kutokana na vivutio ilivyonavyo, wakati Mlima Kilimanjaro ukishindania kivutio bora cha utalii duniani.

Tuzo hizo zitakazotolewa kutokana na wingi wa kura ambazo kila kivutio kitapata kutoka kwa watalii, wataalamu wa sekta hiyo na watoa huduma, zitahitimishwa Desemba 10 nchini Vietnam.

Kwenye kipengele cha nchi yenye vivutio vingi, Tanzania inachuana na Botswana, Kenya, Namibia, Afrika Kusini, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

Mlima Kilimanjaro unachuana na vivutio vingine vya jengo refu la Burj Khalifa (Dubai), Ferrari World (Abu Dhabi), The Great Wall (China) na Intramuros (Ufilipino).

Vivutio vingine vilivyo pamoja na mlima huo mrefu zaidi Afrika ni Las Vegas Strip (Nevada, Marekani), Machu Picchu (Peru), Spike Island (Ireland) na Mlima Sugarloaf.

Kupata ushindi, wadau wanatakiwa kujiandikisha na kupiga kura za kutosha kupitia tovuti ya waandaaji ambayo ni www.worldtravelawards.com/register.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Utalii nchini (TTB) imewaomba Watanzania waliopo ndani na nje ya nchi kupiga kura kwa wingi ili vivutio hivyo vishinde na kubeba tuzo zilizoanzishwa mwaka 1983.

Sekta ya utalii nchini ilikua kwa asilimia 12.6 kati ya mwaka 2015 na 2016, hivyo kuongeza mchango kwenye Pato la Taifa (GDP) licha ya ajira zaidi ya 500,000 inazotoa.

Huenda hali ikawa hivyo mwaka huu baada ya watu kadhaa maarufu duniani kutembelea vivutio vilivyopo nchini. Kwenye orodha hiyo wamo wanasoka, wanamuziki, waandishi wa habari na wanasiasa wa kimataifa.

Chanzo: Mwananchi
 
tutapiga...
mlima huo ungekuwa US ungeshafanywa nembo ya UN ila sisi hadi kura kukubalika tu.
 
Sekta ya utalii Tanzania bado haijapata watu muhimu wenye kufahamu namna ya kuipata tija inayotakiwa ipatikane.

Huo ni vichekesho kuona kuwa kwenye siku ya utalii ya Tanzania huko Ulaya, sisi tunaotangaza bia na konyagi, kama vile tumeumbiwa ulevi.

Kenya pamoja na ukabila wao wa chini kwa chini, siku ya utalii huhakikisha na inapambwa na kikundi chao cha ngoma, kinachogharamiwa na serikali kuu.

Wakenya wanakuwa wamoja kwenye kuiuza nchi yao, sisi tunatazama ubinafsi wetu na kufaidika kwetu badala ya kujikita katika kuitangaza Tanzania moja kiutalii.

Miaka inakwenda haya makosa yetu makubwa wala hatujisumbui katika kuyapatia suluhisho la kudumu.

Wizara ya maliasili na utalii inapewa watu ambao hawana mguso wa kimataifa ambao utaifanya Tanzania iheshimiwe kupitia utalii. Wale wanasiasa wabinafsi na wenye viburi vya usomi wao ndio wanaopokezana nafasi ya juu kabisa.

Rais John Magufuli ambaye wazo la maendeleo kwake siku zote linaungwa mkono, anayo nafasi ya kukaa na wenye kuufahamu utalii, lakini wanafanyiwa kauzibe na wachumia tumbo wachache.

Hawa watu watamueleza ni namna gani mamlaka za utalii zinavyojitambulisha zenyewe kimataifa pasipo kuitanguliza kwanza Tanzania.

Tanzania itakuwa unaburuzwa na Kenya kwenye michakato ya kupata watalii wengi kila mwaka, kwa sababu Kenya inahakikisha utamaduni wao unakuwa ni sehemu ya tangazo la utalii.

Kutangaza konyagi na bia kwenye matamasha makubwa ya kiutalii ni ukosefu mkubwa wa ubunifu, na kwa hali hii sio ajabu tukabakia kuwa watu wa kutazamana na kutafutana ubaya kwa sababu tu ya kufikiria riziki zetu badala ya ile riziki kubwa ambayo ni pato la Taifa kupitia utalii.

Good point

Utalii una multiple economic effect kwa Serikali na wananchi, NOT only Park entry fees and tax

Utalii una stimulate secta nyingine kama Kilimo na Madini

Hotels wananunua vyakula, na matunda, na pia wazungu wananunua bidhaa za mikono na madini kama Tanzanite

TTB inafanya juhudi katika kutangaza utalii, kuna ongezeko la wageni, ila bado ongezeko ni kidogo sana kwa Mwaka. Tanzania ina vivutio vya kipekee Africa kama Mount Kilimanjaro and Ngorongoro, maarifa zaidi yafanywe. KIla mwaka inatakiwa kuongezeka 50% ya watalii...

Kuna tatizo mahali, Ndege mfano Southern Airlines ya China inatua Nairobi, Tanzania haifiki

Rais Magufuli amefanya jambo la maana kumteua Kigwangala, ni waziri mwenye ubunifu
 
nili jaribu kufanya research ndogo kuhusu utalii wa ndani nilicho baini ni kwamba wa Tanzania wengi hatujui vivutio tulivyo navyo na kuna baadhi ya watu nilio jaribu kuuliza wanazijua mbuga zilizopo kwenye ule wimbo wa shule ya msingi kwa upande wa historical sites wanao zifahamu kati ya watu 10 basi ni 1 au w2 na kiuhalisia ule wimbo umaharibu kiasi kikubwa kama 80% ya wa Tanzania si watoto kwa wa kubwa.....nacho taka kusema ni hivi tuwafanye wa Tanzania waweze kujua vivutio vyao vya utalii ili hata wanao enda out of this country wa weze kueleza vizuri the beauty of Tz.....kwa sababu tuna tangaza kuhusu Serengeti,Ngorongoro na Mt.Kilimanjaro maana yake tuna pata watalii wana panda milima na mbuga za wanyama ila watalii wa historical sites tumewasahau utalii una uwanja mpana ila nafikiri viongozi wenye dhamana hawana passion na sector zao as if wapo kwa maslahi yao na pia tu ondoe intrest za kimikoa,kikanda tuhubiri kuhusu TZ nasio ukanda fulani huwezi kupandisha pato la utalii kwa Serengeti,Ngorongoro na Mt.Kilimanjaro pekee try to balance .......
 
Sera za serikali nazo ngumu

Infrastructure nazo hafifu
 
Nampongeza Waziri Kigwangala amekuja na mwamko mpya na anaweza kufanya mageuzi makubwa
 
Mkuu unaweza kutujuza mwamko aliokuja nao Kigwangalla kwenye sekta ya Utalii....
Mikakati gani amekuja nayo.?

Soma Media, Nenda Google search Kigwangala..

Kama wewe ni kilaza, mwombe hata Mke wako, au hata mchepuko akusomee
 
Back
Top Bottom