Vizazi Vinne Kutokea Sasa Waafrika Wote watakuwa na Majina ya Kizungu, Very Sad

Kuna wamama walizaa watoto wakawaita Tyson, Evander, John Cena, Rambo, Morris, Aaliyah, Mariah, Wheatney, Monica, Diego, sijawahi kuona mzazi mtanzania akiita mtoto wake Schwarzenegger
 
Sijawahi kuona watanzania wenye majina ya kirusi na kichina
 
Prisca Hamberg!!! 😀😀😀😀
 
Watoto wangu Mimi hawawezi kuwa na majina ya kipuuzi na ya utamauni wa Wazungu.
 
Nani anapenda majina ya kwetu ya hovyo hovyo , ambayo hayana ubunifu wowote zaidi ya kuwaza uchawi , pesa za majini , chuma ulete, maombi ya kukanyaga mafuta 24hrs?
Lilian lina ubunifu upi? Una uhakika sio jina la mchawi wa kizungu?
 
That is kind of nonsense 🚮🚮🚮

Huwa napenda sana siku Moja nije niingie kwenye mjadala na hao mapadri wenu Ili niwaoneshe kwamba sio watu wote wako brainwashed na tamaduni za Wazungu.
 
Mkuu ebu we zaa mtoto umuite mateso, shida, matatizo uone kama yanaleta amani!
Majina hutolewa Kwa sababu maalumu.

Walioitwa matesi,shida etc by then Walipewa hayo majina kulingana na mazingira husika.

Kwani hakuna majina yenye maana tofauti na hayo kulingana na tamaduni zenu?

Mwisho jumuiya John hakumuondolei hizi tabu hapo Juu sana sana kunaondoa identify na kunaonesha huna utamaduni ukitokea Duniani kama bahati mbaya.
 
Mchina katika mambo aliyofanikiwa ni kudhibiti dini, from there ameweza kutunza asili yake
Sema kudhibiti dini za Wazungu na Waarabu,wao Wana dini zao ambapo na sisi tulikuwa na dini zetu.

Haya hapa ndio matokeo ya kukumbatia dini za wageni Sasa 😁😁😁👇👇
 
Sema kudhibiti dini za Wazungu na Waarabu,wao Wana dini zao ambapo na sisi tulikuwa na dini zetu.

Haya hapa ndio matokeo ya kukumbatia dini za wageni Sasa 😁😁😁👇👇
View attachment 3558901
Naam nakubaliana na wewe. Dini zao za asili walizitunza na kudhibiti influence ya nje.

Wakati sis tulizichukua kaka zilivyo, leo hii ni wachache wanaokumbuka tamaduni za asili
 
Kwa kweli inasikitisha mnooo...

Wazazi wetu walikuwa na majina ya kizungu na naamini wwngi wao hawakuwa na maana sahihi ya hayo majina,just because lili sound vizur tu au lilimpendeza tu kulitumia ilitosha!

Shida inazidi hawa wasomi weengi walioongezeka nao wanafuta mikumbo ile ile yaani onafika maali naanza kuamini,ELIMU YETU INASHIDA!

Southern African countries zinajitahid sana,hata Nigeria ila sisi hapa,ihali inasikitisha sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…