Voices From Within: Nimeambiwa Watanzania wote Wazalendo wa kweli kwa Taifa, Tumuombee Rais Samia Afya njema

Wacha kuzungusha hadithi kama kuna zaidi unachokijua we sema tu.
 
Leo ndiyo nimeamini kwamba Samuya anaumwa baada ya bandiko la PASKALI.
 
Mzee habari hii inaleta taharuki
 
Sauti from within!

Inakushawishi tumuombee Rais!

Rai yako 'inaelea' kwa sababu haujasema tumuombee kwa ajili gani?

Anaumwa au ana changamoto yoyote?

Kumbuka maombi bila kuyaelekeza hitaji lako ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa, hawezi cheza.
 
bila shaka dua yangu najua itakavyokuwa
 
Mkutano wa Iringa ulihusu nini na ulifanyika lini na ninani alipreside?

Emb fafanua ili niutafute You tube niusikilize.
 
Aisee 😭😭😭

Tarehe 29 October mwaka jana ilinibadilisha mtazamo kabisa , sikuwahi kuamini kuna siku tutaona kwenye media za kimataifa maiti za watanzania zimezagaa mitaani halafu kuna wapumbavu kadhaa waliovaa suti na kupewa ulinzi wa mabunduki wanasema hakuna mauaji.

Hawakuishia hapo wanachota pesa za hao hao wanaowaua wanaunda vikundi vya mipasho wakiita tume za kuchunguza sijui vurugu kumbe wanapoteza,ushahidi na kuwalinda wauaji.

Wameua maelfu ya watu na bado maiti wakazichukua na kuwafukia kusikojulikana , familia zina majonzi baada ya mwaka hawajui ndugu zao wapo wapi na wako hai au wafu wapo walioamua kubaki na machozi tu wengine waliamua kuzika picha, viatu na nguo kupoza maumivu ila bado hali ya uchungu ipo pale pale hatuwezi kukubali hili lipite hivi hivi hasa kama mtu una akili timamu.

Msimamo wangu tangu siku hiyo ni yeyote aliye meza moja na hawa manyang'au jambo lolote baya likimkuta kwangu ninasema ni GOOD RIDDANCE TO BAD RUBBISH.
 
Huyu kaja kuwapa taarifa kijanja kuna kitu hakipo sawa ....
 
Tupo pamoja kwenye hili suala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…