Vurugu patashika nguo kuchanika Kituo cha Mwendokasi, Kimara nyomi la watu wakigombania kupanda basi

Vurugu patashika nguo kuchanika Kituo cha Mwendokasi, Kimara nyomi la watu wakigombania kupanda basi

Mabus ni machache ila madereva nao wanazingua wanaacha abiria stand wanatoa magari matupu sijui wanakimbilia wapi....
Kuna vituo njiani huwa vina nyomi la watu ndio wanakowahi. Wanajaribu kubalance ila ndio hivyo.
 
Nimesoma page ya kwanza hadi hapo, sijaona aliyesifu Mama anaupiga mwingi. Tutatatuaje hili tatizo kama kusifu tu kunawashinda?
 
Huyo kifua kipana angekuwa kwenye nchi za watu wenye akili angekuwa jela muda huu anasubiri kunyongwa
 
Hiki ndicho kila siku huwa nakisema humu ndani, huwezi kujenga barabara kwa mabilioni ya fedha za umma halafu barabara hizo zinakuwa underutilized. Yaani badala ya kuweka utaratibu ili watu binafsi waingize mabasi yao makubwa yenye vigezo vya kubeba abiria mjini unaacha watu wanateseka daily. Hizo barabara ilitakiwa kuwe na Buses zaidi ya 500 zina fanya kazi masaa 24 kubeba watu. Sasa kuna faida gani watu wakiwa wanateseka kwa kung'ang'ania hizo mwendo kazi ambazo zimeshafeli?
Inasikitisha sana raia wanapokuwa na maono kupita viongozi.
 
Ni Tanzania tu arbun transport project with resources inapata hasara wakati 80% ya raia hawana usafiri binafsi wanategemea usafiri wa umma.
 
Gerezani hapa kinahappen tena. Raia wanazuia gari wanapanda.
 
Na kero kama hizi ndio wahuni walikuwa wanampiga Melo mkwara kuwa zifutwe mama yao hatakiwi kuona maana walishakuja na msemo wao kuwa bi mkubwa huna deni.
 
Hali ilivyokuwa asubuhi ya leo katika Kituo cha Mwendokasi, Kimara jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mashuhuda, abiria waliamua kuingia barabarani na kusimamisha basi kwa nguvu, baada ya kukaa kituoni kwa muda mrefu huku mabasi yakipita bila kusimama.

Baada ya kusubiri kituoni kwa saa kadhaa, wakaamua kusimamisha basi hili kwa nguvu.

Mpaka sasa ni mwaka sijapata hayo magari sitaki hat kuyasikia
 
Maisha ya dar ya kipumbavu sana!....halafu wananchi wamezoea wanaona ni sehemu ya maisha yao!

Back
Top Bottom