Vurugu patashika nguo kuchanika Kituo cha Mwendokasi, Kimara nyomi la watu wakigombania kupanda basi

Vurugu patashika nguo kuchanika Kituo cha Mwendokasi, Kimara nyomi la watu wakigombania kupanda basi

Sio kila mtu anaweza kumudu bajaji au pikipiki
Ni kweli mkuu ila haiondoi ukweli kuwa huo usafiri ni wa kipuuzi. Aidha kwa makusudi au kwa uzembe wasimamizi wa mradi husika ni lazima wafurushwe na waje wapya wenye competency.
 
Hali ilivyokuwa asubuhi ya leo katika Kituo cha Mwendokasi, Kimara jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mashuhuda, abiria waliamua kuingia barabarani na kusimamisha basi kwa nguvu, baada ya kukaa kituoni kwa muda mrefu huku mabasi yakipita bila kusimama.

Baada ya kusubiri kituoni kwa saa kadhaa, wakaamua kusimamisha basi hili kwa nguvu.

View attachment 3311886
Poleni sana
 
Kwa ss wengine tuliyokuwa mbele ya muda tunasema huo usafiri ni sawa na kusema unawabeba mangombeee.....
Unless labda viongozi nao waanze kuutumia
Huo ni usafiri wa kishenzi,wakimateso tuuu
Nashangaa mpaka sahv waziri anayehusika na sekta hiyooo yuko kimya

Ova
Nilitumwa kikazi Dar kwa 3 days bila kuwa na gari la ofisini ikabidi nitumie huo usafiri!!! Kwa kweli ni usafiri mgumu, wa kishenzi na mateso makubwa sana!!! Siku 3 cha moto nilikipata. Kwa kweli ninawahurumia wanaotegemea huo usafiri kila siku.
 
Awapangiwi hao na awafuatilii,ulaya brt inakua mpaka na inspector,dereva hajui kwanza inspector atamkuta kituo gani,then muda,ukifika kituo unajua kabisa saa 7:00 bus la kivukoni litakua wapi,hao awapangiwi na maboss zao hawajahi kutumia public transport ni mwendo wa v8 so hawajui chochote na hawataki kujua on ground raia wanateseka vp
Mtu anachaguliwa kuwa kiongozi wa udart ila anamiaka zaidi ya 10 hadi 20 iliyopita hajui adha ya usafiri ikoje kuna mambo hawezi yapa uzito

Hata viongozi wengi wa leo ni watoto wa viongozi hawajui shida za mwananchi wa kawaida ndo maana hawajali
 
Huwa umekosa tu akili, miaka kumi ijayo utasoma maandiko yako na huenda kujiona usiye na akili.
Huyo jamaa ni wakuupizia mimi nilishamshauri autumie jina halisi kidogo watamkumbuka sasa unatumua jina bandia alafu unasifia ujinga sababu anaowasifia hata hawamjui

Kuna mtu kampa matumaini akiandika ujinga na kusifia kila kitu atakumbukwa
 
Huwa umekosa tu akili, miaka kumi ijayo utasoma maandiko yako na huenda kujiona usiye na akili.
Huyo jamaa ni wakuupizia mimi nilishamshauri autumie jina halisi kidogo watamkumbuka sasa unatumua jina bandia alafu unasifia ujinga sababu anaowasifia hata hawamjui

Kuna mtu kampa matumaini akiandika ujinga na kusifia labda atakumbukwa mimi simjibugi tena hata akiniquote
 
Hali ilivyokuwa asubuhi ya leo katika Kituo cha Mwendokasi, Kimara jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mashuhuda, abiria waliamua kuingia barabarani na kusimamisha basi kwa nguvu, baada ya kukaa kituoni kwa muda mrefu huku mabasi yakipita bila kusimama.

Baada ya kusubiri kituoni kwa saa kadhaa, wakaamua kusimamisha basi hili kwa nguvu.

View attachment 3311886
Tuyaite tu MWENDOKUSUBIRIA badala ya mwendokasi
 
Pamoja na hao abiria kulinda mikoba yao na begi kuvaa tumboni lazima kuna waliobiwa tu.
 
Back
Top Bottom