Uchaguzi 2020 Vurugu zatawala ofisi za CCM Dodoma baada ya walioshinda kura za maoni Udiwani kukatwa

Uchaguzi 2020 Vurugu zatawala ofisi za CCM Dodoma baada ya walioshinda kura za maoni Udiwani kukatwa

Vurugu kubwa zimeibuka leo 18 August 2020 hapa ofisi za ccm wilaya ya dodoma opposite na white House makao makuu ya ccm Taifa,wafuasi watch toka kata ya changombe walimvamia katibu wa wilaya na kumpa kichapo Hali iliyopelekea police kuwahi kuwatuliza wafuasi hao inadaiwa walienda kumsindikiza kada wao Juma masugu inaedaiwa jina lake limerudi kugombea udiwani wa changombe.

Na aliwakusanya wafuasi wake wengi waende kumescort kufika ofsin wakakuta jina la Bakari fundikira aliyeongoza kura za maoni kwa kutumia wajumbe mamluki wanavyosemaga wao maccm,bw Masugu anadai Katibu alimpigia simu Jana na kumwambia jina limerudi ila ampe million moja kwanza sijui ilikuwa ya nini pia inasemekana bw fundikira alivyoona chama kata hakimtaki alimpigia simu Katibu mkuu Bashiru baada ya kuongea nae jina lake likarudi na ndo ugomvi ukaibuka leo ofisin na kusababisha kupigwa vibaya Sana.

Katibu wa ccm wilaya bila police kuwahi huenda angefariki,mpaka mda huu vijana wa ccm na wafuasi wao ma bodaboda wametapakaa hapa nje ya ofisi na baadhi ya wafanyabiashara wameanza kufunga maduka yao,police inaonekana wanaogopa wanapata kigugumizi kuwamwagia maji ya washawasha hao wahuni wa ccm kuwatawanya
Yaani hiki ulichohara hapo na video iliopo ni vitu million 2 tofauti 🚮🚮🚮🚮
 
Jamaa linasema

"Eti kwanini utumie dola,mimi sio mpinzani"

Ina maanawanawafanyia makusudi na ni maelekezo kutoka chama chao bumbafu.
Umeonaeeeee? Yaani hii mijamaa ni zaidi ya nyoka mwenye sumu kali kwa upinzani
 
Wanaruka na kukanyagana!
Kwa Sugu mbona salitumia nguvu kubwa?
Hiyo laana haiwaachi ccm asilani.
 
18 Aug 2020
Dodoma, Tanzania

WanaCCM waandamana kupinga maamuzi



Vurugu zinaendelea leo 18 agosti 2020 katika ofisi za CCM Wilaya ya Dodoma mjini baada ya kupokea majina ya wagombea udiwani ambao wamekatwa licha ya kuongoza.

Jana halmashauri ya CCM mkoa wa Dodoma walirudisha majina ya madiwani waliogombea kupitia chama hicho ambapo kata 7 Kati ya 41 za jiji la Dodoma walioongoza walikatwa na kurudishwa wengine ndipo wakaandamana ofisi za wilaya.

Mmoja wa diwani aliyeshinda CCM lakini jina lake lililokatwa amewaomba wanaCCM wa kata ya Changombe kuwa watulivu wasifanye maandamano wasubiri maamuzi ya Halmshauri ya wilaya CCM watakapotafuta ufumbuzi wa sintofahamu hiyo ndani ya CCM .

Source : Mwananchi digital

Ccm kifo cha mende arafu anaibuka mjinga eti ccm imeimalika
 
Back
Top Bottom