Uchaguzi 2020 Vurugu zatawala ofisi za CCM Dodoma baada ya walioshinda kura za maoni Udiwani kukatwa

Uchaguzi 2020 Vurugu zatawala ofisi za CCM Dodoma baada ya walioshinda kura za maoni Udiwani kukatwa

jimbo litaenda upinzani hilo, wao waweke watu wanaowajua wao, wajumbe wamevumiliwa sasa na nyie tena, duu
 
huyo anae arrestiwa anasema "kwa nini mnatumia dola? mimi sio mpinzani"

Yani CCM wanavyojua wao dola ni ya kushughulikia wapinzani

na kweli video inaonyesha askari wanavyo mu arrest kwa kumbembeleza bembeleza
Wamembeleza sana, wanamwambia jambo litashughulikiwa kichama
 
Chadema wameshasahau namna walivyomkata Yule bidada na kumpa nafasi John Mrema wanaanza kusheherekea ya wenzao.
 
Katika hali isiyo ya kawaida tofauti kabisa na wanavyofanyiwa wafuasi wa vyama vya upinzani polisi jijini Dodoma wamemkamata kistaarabu mno huku wakimbembeleza kwa maneno matamu mfuasi wa CCM aliyefanya vurugu na kuhatarisha amani ya nchi kwa kushiriki maandamano bila kibali na kuvamia ofisi za CCM wilaya ya Dodoma kupinga uteuzi wa mgombea udiwani.

Walisikika polisi wakimsihi na kumbembeleza kwa maneno matamu, "njoo bwana!" "Panda twende basi". Huku jamaa akikataa akisema " kwanini mtumie dola?" " kwani mimi ni mpinzani".

Huu ni upendeleo wa wazi wa jeshi la polisi nchini, ukilinganisha na tukio la karibuni mathalani jinsi alivyopigwa Tanganyika jeki Mheshimiwa Joseph Mbilinyi kule Mbeya kuna tofauti kubwa sana.

Tafashali mods huu uzi usiunganishwe na wowote tujadili upendeleo huu wa jeshi la polisi.
 
Mtu kaongoza kura za maoni kwa kuhonga wajumbe fedha nyingi halafu unamkata, badamu batamwagika!
 
Back
Top Bottom