Uchaguzi 2020 Vurugu zatawala ofisi za CCM Dodoma baada ya walioshinda kura za maoni Udiwani kukatwa

Uchaguzi 2020 Vurugu zatawala ofisi za CCM Dodoma baada ya walioshinda kura za maoni Udiwani kukatwa

Walipuane kabsa
18 Aug 2020
Dodoma, Tanzania

WanaCCM waandamana kupinga maamuzi



Vurugu zinaendelea leo 18 agosti 2020 katika ofisi za CCM Wilaya ya Dodoma mjini baada ya kupokea majina ya wagombea udiwani ambao wamekatwa licha ya kuongoza.

Jana halmashauri ya CCM mkoa wa Dodoma walirudisha majina ya madiwani waliogombea kupitia chama hicho ambapo kata 7 Kati ya 41 za jiji la Dodoma walioongoza walikatwa na kurudishwa wengine ndipo wakaandamana ofisi za wilaya.

Mmoja wa diwani aliyeshinda CCM lakini jina lake lililokatwa amewaomba wanaCCM wa kata ya Changombe kuwa watulivu wasifanye maandamano wasubiri maamuzi ya Halmshauri ya wilaya CCM watakapotafuta ufumbuzi wa sintofahamu hiyo ndani ya CCM .

Chanzo: Mwananchi digital
 
Dah..jamaa anasikika akisema ETI YEYE SIO MPINZANI hivyo polisi wasimnyanyase
Yaani nchi hii imekuwa ya kipumbavu sana ina maana wanapigwa ni wapinzani tu? Na Polisi wanafanya kosa la kipumbavu kujishikamanisha na CCM. Yaani leo huyo angekuwa mpinzani angevunjwavunjwa! Pumbavu kabisa hili jeshi!
 
Vurugu zimeibuka katika ofisi za CCM Wilaya ya Dodoma baada ya makada wa CCM wanaodai majina ya wagombea udiwani yaliyopitishwa yamebadilishwa bila sababu za msingi katika baadhi ya kata za Wilaya ya hiyo kuweka kambi katika ofisi hizo.

Vurugu zilizotokea katika ofisi za CCM Wilaya ya Dodoma zimesababisha askari kuwasili kwa ajili ya kulinda usalama katika ofisi hizo na kuzuia vurugu kufuatia malalamiko ya kubadilishwa kwa mgombea udiwani aliyetangazwa.


 
Na bado. Subiri ngazi ya wabunge. Waliotuma barua mpk kwenye mitandao wakikatwa watatuma barua UN.
 
Back
Top Bottom