Hahaha. Hapo sawa. Kwakweli kuna mazingira unaweza kuwepo ukala chochote kinachoweza kulika hata majani ya porini.
Kuna siku nipo chaka fulani umasaini huko nimekaa siku mbili sijala asee tulifika kwenye boma moja tukapewa ugali kiporo na chai ya maziwa ila ukiangalia hata hivyo vyombo vilivyo vichafu kwa hali ya kawaida hauwezi kula kamwe. Ila tulipiga fresh kabisa tena hata maji ya kunawa hakuna unashika ugali unabakia na rangi kama umepakwa udongo.
Maji unakunywa yaliyotuama na hapo hapo ng'ombe wanakunywa na kunya kwenye hilo dimbwi. Yani unafunga tu macho usione unachokunywa ila huwezi kuacha kunywa.