Vyama 12 vya upinzani nchini Vyamkana Mbowe na Chadema, vyasema vitashiriki uchaguzi chini ya NEC kwani wana Imani nayo

Vyama 12 vya upinzani nchini Vyamkana Mbowe na Chadema, vyasema vitashiriki uchaguzi chini ya NEC kwani wana Imani nayo

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Vyama 12 vya upinzani nchini vimesema vitashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu chini ya Tume ya uchaguzi iliyopo kwani wana imani nayo na pia wana imani na Rais Magufuli.

Makatibu wakuu wa vyama hivyo wakiongea na waandishi wa habari wamesema Mbowe na Chadema ni miongoni mwa waliosababisha tukose Tume huru ya uchaguzi baada ya kususia bunge la katiba halafu leo anawahadaa wananchi eti waikatae NEC.

Viongozi hao pia wamemshukia Zitto na kudai kuwa ni kiongozi mbinafsi anayetanguliza maslahi yake mbele badala ya maslahi ya taifa.

Miongoni mwa vyama vilivyozungumza kwenye mkutano huo ni pamoja na TLP, DP, CUF, UDP na NRA

Source TBC habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Naona kichwa cha habari ni vyama 12 lkn katika habari yako ni vyama 4 amakweli mumezidi uongooo yani hata hesabu kichwani huna tena kwa kushabikia kutoa uhai wa watu
 
TBC ni kama kokoro la kubeba kila aina ya uchafu wa CCM na wapambe wake. Habari za CHADEMA haziwezi kutangazwa kule mpaka ziwe mbaya kwa CHADEMA ila nzuri kwa CCM.
 
Yaani ina maana hivyo vyama havijui ni kwa nini mchakato wa katiba ulikwama ? Ni aibu kwa vyama hivyo vilivyokuwa na wawakilishi kutojua sababu za kukwama mchakato wa katiba.

Mchakato wa katika ulikwama kwenye kuelekea rasimu ilikubaliwa kwa wananchi kwa ajili ya kura ya uamuzi ( wengine huita kura ya maoni).

Serikali ilikwama kuitisha kura ya maoni
 
Sasa chama kama TLP ambacho mgombea wake wa urais ni Dr John Pombe Magufuli kitafanya maamuzi gani kwa mfano?
Dah mzee wa Kiraracha aliniacha hoi sana kipindi cha kampeni, yaani ye ni mwenyekiti wa TLP na chama chake kimesimamisha mgombea urais halafu yeye anampigia debe bwana Rais Magufuli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
FB_IMG_15413122208257667.jpg
 
Back
Top Bottom