Vyama 12 vya upinzani nchini vimesema vitashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu chini ya Tume ya uchaguzi iliyopo kwani wana imani nayo na pia wana imani na Rais Magufuli.
Makatibu wakuu wa vyama hivyo wakiongea na waandishi wa habari wamesema Mbowe na Chadema ni miongoni mwa waliosababisha tukose Tume huru ya uchaguzi baada ya kususia bunge la katiba halafu leo anawahadaa wananchi eti waikatae NEC.
Viongozi hao pia wamemshukia Zitto na kudai kuwa ni kiongozi mbinafsi anayetanguliza maslahi yake mbele badala ya maslahi ya taifa.
Miongoni mwa vyama vilivyozungumza kwenye mkutano huo ni pamoja na TLP, DP, CUF, UDP na NRA
Source TBC habari
Maendeleo hayana vyama!