Vyama 12 vya upinzani nchini Vyamkana Mbowe na Chadema, vyasema vitashiriki uchaguzi chini ya NEC kwani wana Imani nayo

Vyama 12 vya upinzani nchini Vyamkana Mbowe na Chadema, vyasema vitashiriki uchaguzi chini ya NEC kwani wana Imani nayo

Dah mzee wa Kiraracha aliniacha hoi sana kipindi cha kampeni, yaani ye ni mwenyekiti wa TLP na chama chake kimesimamisha mgombea urais halafu yeye anampigia debe bwana Rais Magufuli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aliona mpango mzima hauna maana walivyomkaba hata nafasi ya mmwenykiti wa mtaa kule Kilacha.
 
Ni aibu kwa vyama hivyo vilivyokuwa na wawakilishi kutojua sababu za kukwama mchakato wa katiba.
Ina maana wawakilishi wao walikuwa hawapeleki mrejesho kwenye vyama vyao? Tena wengi walikuwa ni Makatibu na wenyeviti wa vyama hivyo!!
 
Leo jioni baada ya kurudi home nilikuta vijana wangu nyumbani wanaangalia documentary moja ya Afrika kusini wakati wa harakati.
Ndio nikajua sababu ya Winnie Mandela pamoja na kuachana na Nelson bado wa south walikuwa wanampenda wakikumbuka mile kikundi chake cha Moira kilichokuwa na lengo la kuwafanyizia waafrika wenzao waliokuwa wanakwamisha juhudi kwa kutumiwa na watawala.
Hapa kwetu vikianza hivyo hayo ma popoma ya sijui TLP, UDP nk ndio yakufanyiwa ushenzi hadi wajue upuuzi wao huo ni hatari kwa maisha yao. Mbona kama wanataka ski wajiunge tuu na CCM!
 
Hiyo ni Gear ya kwanza.

Gear ya pili utasikia, tunamwomba Rais Wetu Mpendwa Mzalendo Mhe. Mtukufu Ndg. Dr. John Pombe Joseph Magufuli atupatie Tsh 200M Kwa Kila Chama Ili Tushiriki Uchaguzi Mkuu Bila Vikwazo.
 
Naona kichwa cha habari ni vyama 12 lkn katika habari yako ni vyama 4 amakweli mumezidi uongooo yani hata hesabu kichwani huna tena kwa kushabikia kutoa uhai wa watu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbwiga hao viongozi 4 ndio maoni yao yamerushwa na tv lakini jumla walikuwepo viongozi wa vyama 12........uwe unasoma na kuelewa bwashee!
 
Vyama 12 vya upinzani nchini vimesema vitashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu chini ya Tume ya uchaguzi iliyopo kwani wana imani nayo na pia wana imani na Rais Magufuli.

Makatibu wakuu wa vyama hivyo wakiongea na waandishi wa habari wamesema Mbowe na Chadema ni miongoni mwa waliosababisha tukose Tume huru ya uchaguzi baada ya kususia bunge la katiba halafu leo anawahadaa wananchi eti waikatae NEC.

Viongozi hao pia wamemshukia Zitto na kudai kuwa ni kiongozi mbinafsi anayetanguliza maslahi yake mbele badala ya maslahi ya taifa.

Miongoni mwa vyama vilivyozungumza kwenye mkutano huo ni pamoja na TLP, DP, CUF, UDP na NRA

Source TBC habari

Maendeleo hayana vyama!
Hayo ni matawi ya CCM wala sio vyama vya Upinzani,watanzania sio wajinga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani, hata shetani naye anawafuasi wake.
 
Hhaahaahaha kweli CCm mmeishiwaaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom