Vyama 7 vilivyojitoa uchaguzi wa mitaa vyatoa tamko la pamoja

Tatizo la JF watu wanaanzisha vurugu wakiwa nyuma ya keyboard tena wengine wakiwa Marekani na Ulaya!!

So likitokea la kutokea wao wako mbali sisi ndio tunahangaika na watoto wetu huku!!

Kama vipi na wao waje na familia zao huku tulianzishe wote na sio kutukoli sisi!
 
Ndugu zangu Watanzania Tuendelee kutii sheria bila shuruti
 
Kwa ufupi jiwe ni taahira! Tumekula hasara kama Taifa!
 

Mkuu, kama nchi hii kuibiwa ilishaibiwa sana na itaendelea kuibiwa hata kama tukikuchagua wewe kuwa kiongozi.

Wengine tunaridhi na haka kaamani tuliko nako maadam tunapata uhuru wa kupambana kulisha watoto wetu ili nao wakue!!

Kama ni vurugu na fujo, Mungu aziepushie mbali kwani hata wasipoiba, hakuna atakayekupa pesa za bure. Hivyo, bora tubaki na amani tuliyo nayo!
 

Hakuna asiyetaka amani, ila wanaopora haki ndio wanaohatarisha amani. Unaweza ukanipa sababu ya msingi ya watu kupora haki ya wengine kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa? Hata nikipewa mimi nchi hii, huo uhuru wako wa kupambania hao watoto wako sitaupora, hivyo hofu yako haina msingi.
 
Wewe ni coward; kwani sasa hivi familia ngapi zinateseka, Ben wa Saanane, Aquilina, Azory Gwanda, Mwangosi, watu 21 Pemba, mawazo, kinondoni uchaguzi mdogo; makamanda kibao wameuliwa na Green Guard; miili Coco Beach, Kibiti,na wengine wengi waliofilisiwa na kesi za uchumi kwenye jasho Lao hiyo Amani unayohubiri ipo wapi? Wakina kabendera? Tatizo bado hayajakufika ndo mana unaongea huo upuuzi wako tulia dawa ikuingie#anaitwaroma#tumehuruyauchaguzi#katibampyayawarioba
 
Hao huwezi linganisha na mamilioni ya watanzania tunaofurahia Amani na Uhuru. Inawezekana hao walitaka kuvuruga Amani. Heri wachache wapotee wengi walindwe
 
...waache uoga - wajifunze upinzani wa wenzao wa Uganda...hii habari ya kuonewa huruma haipo

.....walikosea sana pale walupopigwa mkwara kuhusu mikutano ya nje walipogwaya...na ile ya ukuta

Hapana.

Mimi nadhani walifanya vizuri kwa sababu wametumia uzoefu huo kujifunza na kumfahamu vizuri zaidi anayewaonea.
Chukua mfano wa 'UKUTA', lile lilikuwa ni bomu la wazi kabisa. Wangelazimisha maandamano yale, wakati huu hali ingekuwa ni tofauti kabisa.

Kuna watu ambao wakati huu wasingekuwepo. Hata CHADEMA yenyewe isingechanga karata zake sawsawa huenda wakati huu tungekuwa tunawakumbuka tu kwa mbali. Na hata lawama nyingi wangekuwa wanatupiwa wao kwa kufanya papara. Subira kwao, kwa maoni yangu imezaa matunda ambayo yapo tayari kuvunwa.

Kuzuiwa mikutano, wangefanya nini - walazimishe kuifanya mikutano hiyo? Hapa pia naona wasingevuta subira ili mtesi wao aonekane kwa kila mtu kwa matendo yake, lawama zingewaangukia wao.

Ninachowalaumu vyama vya upinzani ni kutegemea njia hiyo moja tu ya kmikutano kufanya siasa. Ilitakiwa waanze mbinu mhimu za siasa za 'mtu-kwa-mtu', 'mlango kwa mlango', n.k. huko mitaani waliko wanannchi na viongozi wao wa vyama hivyo.

Njia hii ya kueneza 'sumu' kwa wananchi ndiyo ilikuwa jibu sahihi ya kuwapigia CCM. Nijuavyo, hawakufanya kazi hiyo kwa ufanisi, na sasa ndio maana watakuwa na mzigo mkubwa wa kujieleza kwa wananchi, wakati njia ilishasafishwa na viongozi watawala.
 
Nakwenda Zimbabwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…