Vyama 7 vilivyojitoa uchaguzi wa mitaa vyatoa tamko la pamoja

Vyama 7 vilivyojitoa uchaguzi wa mitaa vyatoa tamko la pamoja

TUSIHUBIRI WALA KUFURAHIA VURUGU.

Siyo sahihi wala busara kutafuta suluhisho kwa kuhubiri na kushabikia vurugu.

Wawezaje kutamani kuingia kweye mauaji? Unataka damu ya nani imwagike? Unamfurahisha nani kwa kuhubiri vurugu?

Kumbuka: Nchi ikiingia kwenye vurugu watu wengi wataathirika. Tutapoteza maisha ya Watanzania wenzetu, baadhi watakuwa vilema, na wengine huenda wakawa wakimbizi. Kati ya wahanga wa vurugu unaweza kuwa wewe, watoto wako, ndugu na jamaa zako, mimi, na wengineo wengi.

NI kitu gani hicho tumekikosa hadi vurugu iwe ndiyo mbadala sahihi?
Tatizo la JF watu wanaanzisha vurugu wakiwa nyuma ya keyboard tena wengine wakiwa Marekani na Ulaya!!

So likitokea la kutokea wao wako mbali sisi ndio tunahangaika na watoto wetu huku!!

Kama vipi na wao waje na familia zao huku tulianzishe wote na sio kutukoli sisi!
 
Kwa ufupi jiwe ni taahira! Tumekula hasara kama Taifa!
 
Wangalau sasa wapinzani wanaanza kuzungumza lugha inayotakiwa kutufikisha pazuri, tunajua njia hii ni ngumu na italeta mauji, lakini kwa hapa tulipofikia hakuna njia nyingine nje ya njia hii, tena ilichelewa. Tunajua fika woga umewaingia wananchi, lakini kwenye madai halali uwoga itabidi uondoke.

Mkuu, kama nchi hii kuibiwa ilishaibiwa sana na itaendelea kuibiwa hata kama tukikuchagua wewe kuwa kiongozi.

Wengine tunaridhi na haka kaamani tuliko nako maadam tunapata uhuru wa kupambana kulisha watoto wetu ili nao wakue!!

Kama ni vurugu na fujo, Mungu aziepushie mbali kwani hata wasipoiba, hakuna atakayekupa pesa za bure. Hivyo, bora tubaki na amani tuliyo nayo!
 
[emoji80][emoji80][emoji80]
Screenshot_20191116-214442-picsay.jpeg
 
Mkuu, kama nchi hii kuibiwa ilishaibiwa sana na itaendelea kuibiwa hata kama tukikuchagua wewe kuwa kiongozi.

Wengine tunaridhi na haka kaamani tuliko nako maadam tunapata uhuru wa kupambana kulisha watoto wetu ili nao wakue!!

Kama ni vurugu na fujo, Mungu aziepushie mbali kwani hata wasipoiba, hakuna atakayekupa pesa za bure. Hivyo, bora tubaki na amani tuliyo nayo!

Hakuna asiyetaka amani, ila wanaopora haki ndio wanaohatarisha amani. Unaweza ukanipa sababu ya msingi ya watu kupora haki ya wengine kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa? Hata nikipewa mimi nchi hii, huo uhuru wako wa kupambania hao watoto wako sitaupora, hivyo hofu yako haina msingi.
 
TUSIHUBIRI WALA KUFURAHIA VURUGU.

Siyo sahihi wala busara kutafuta suluhisho kwa kuhubiri na kushabikia vurugu.

Wawezaje kutamani kuingia kweye mauaji? Unataka damu ya nani imwagike? Unamfurahisha nani kwa kuhubiri vurugu?

Kumbuka: Nchi ikiingia kwenye vurugu watu wengi wataathirika. Tutapoteza maisha ya Watanzania wenzetu, baadhi watakuwa vilema, na wengine huenda wakawa wakimbizi. Kati ya wahanga wa vurugu unaweza kuwa wewe, watoto wako, ndugu na jamaa zako, mimi, na wengineo wengi.

NI kitu gani hicho tumekikosa hadi vurugu iwe ndiyo mbadala sahihi?
Wewe ni coward; kwani sasa hivi familia ngapi zinateseka, Ben wa Saanane, Aquilina, Azory Gwanda, Mwangosi, watu 21 Pemba, mawazo, kinondoni uchaguzi mdogo; makamanda kibao wameuliwa na Green Guard; miili Coco Beach, Kibiti,na wengine wengi waliofilisiwa na kesi za uchumi kwenye jasho Lao hiyo Amani unayohubiri ipo wapi? Wakina kabendera? Tatizo bado hayajakufika ndo mana unaongea huo upuuzi wako tulia dawa ikuingie#anaitwaroma#tumehuruyauchaguzi#katibampyayawarioba
 
Wewe ni coward kwani sasa hivi familia ngapi zinateseka,Ben wa saanane, aquilina,azory gwanda,mwangosi, watu 21 Pemba, mawazo, kinondoni uchaguzi mdogo ,makamanda kibao wameuliwa na greengurd, miili Coco beach,kibiti,na wengine wengi waliofilisiwa na kesi za uchumi kwenye jasho Lao hiyo Amani unayohubiri ipo wapi? WA kina kabendera? Tatizo bado hayajakufika ndo mana unaongea huo upuuzi wako tulia dawa ikuingie#anaitwaroma#tumehuruyauchaguzi#katibampyayawarioba
Hao huwezi linganisha na mamilioni ya watanzania tunaofurahia Amani na Uhuru. Inawezekana hao walitaka kuvuruga Amani. Heri wachache wapotee wengi walindwe
 
...waache uoga - wajifunze upinzani wa wenzao wa Uganda...hii habari ya kuonewa huruma haipo

.....walikosea sana pale walupopigwa mkwara kuhusu mikutano ya nje walipogwaya...na ile ya ukuta

Hapana.

Mimi nadhani walifanya vizuri kwa sababu wametumia uzoefu huo kujifunza na kumfahamu vizuri zaidi anayewaonea.
Chukua mfano wa 'UKUTA', lile lilikuwa ni bomu la wazi kabisa. Wangelazimisha maandamano yale, wakati huu hali ingekuwa ni tofauti kabisa.

Kuna watu ambao wakati huu wasingekuwepo. Hata CHADEMA yenyewe isingechanga karata zake sawsawa huenda wakati huu tungekuwa tunawakumbuka tu kwa mbali. Na hata lawama nyingi wangekuwa wanatupiwa wao kwa kufanya papara. Subira kwao, kwa maoni yangu imezaa matunda ambayo yapo tayari kuvunwa.

Kuzuiwa mikutano, wangefanya nini - walazimishe kuifanya mikutano hiyo? Hapa pia naona wasingevuta subira ili mtesi wao aonekane kwa kila mtu kwa matendo yake, lawama zingewaangukia wao.

Ninachowalaumu vyama vya upinzani ni kutegemea njia hiyo moja tu ya kmikutano kufanya siasa. Ilitakiwa waanze mbinu mhimu za siasa za 'mtu-kwa-mtu', 'mlango kwa mlango', n.k. huko mitaani waliko wanannchi na viongozi wao wa vyama hivyo.

Njia hii ya kueneza 'sumu' kwa wananchi ndiyo ilikuwa jibu sahihi ya kuwapigia CCM. Nijuavyo, hawakufanya kazi hiyo kwa ufanisi, na sasa ndio maana watakuwa na mzigo mkubwa wa kujieleza kwa wananchi, wakati njia ilishasafishwa na viongozi watawala.
 
Dar es Salaam. Siku moja kabla ya kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuanza vyama saba vilivyojitoa katika mchakato wa uchaguzi huo vimetoa tamko vikiwataka Watanzania kujiandaa kwa maelekezo mengine yatakayotolewa baada ya kumalizia mashauriano.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Novemba 16 baada vyama vya Chadema, ACT-Wazalendo, Chaumma, CCK, NCCR Mageuzi, UPDP na NLD kutoa msimamo wao.

Akiongea kwa niaba ya vyama hivyo, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari amesema vyama hivyo vilishatoa matamko ya kujitoa kwenye uchaguzi huo kutokana na ukiukwaji wa kampuni na sheria.

Amesema baada ya vyama hivyo kujitoa kushiriki uchaguzi, serikali kwa upande wake ilitoa matamko mbalimbali yaliyokuwa yakitofautiana na kuchanganya, licha ya kuwa yalikuwa yakitolewa na mtu mmoja ambaye ni Waziri wa Tamisemi.

"Baada ya wagombea wa vyama hivyo kujitoa kwenye uchaguzi huo, waliwajulisha wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kuhusu kujitoa na kwa ngazi ya Taifa baadhi ya vyama vilimjulisha waziri wa Tamisemi kwa barua,” amesema Profesa Safari.

Baada ya kushauriana vyama hivyo vimeazimia kwa pamoja havitashiriki kwa vyovyote “kwenye kampeni na uchaguzi unaoenda kinyume na kanuni za uchaguzi” na vimewataka wanachama na wafuasi kutoshiriki.

Aidha vyama hivyo vimetoa wito “uchaguzi huo ufutwe na mchakato wake uanze upya kwa mustakabali wa amani ya Taifa.”

"Tunatoa wito kwa umma na Watanzania wajiandae kwa maelekezo yoyote yatakayotolewa baada ya mashauriano yanayoendelea miongoni mwa vyama na makundi mengine ya jamii," amesisitiza Profesa Safari.

Maazimio mengine ni pamoja na kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia uchaguzi zote nchini.

Amesema vyama hivyo vimetambua kauli na wito uliotolewa na viongozi wastaafu na viongozi wa dini nchini na kuwaomba kuchukua hatua za kuingilia kati mapema ili kunusuru amani ya Taifa.

Akizungumza katika mkutano huo, Kiongozi wa ACT –Wazalendo, Zitto Kabwe amesema Watanzania wanatakiwa kuwa tayari na kutega masikio wakati vyama hivyo na makundi mbalimbali yakiendelea na mashauriano.

"Hatutakubali kuendelea kupingwa kwa miaka minne mfululizo. Tunawataka Watanzania kuendelea kutega masikio wakati hatua zikiendelea ikiwemo mashauriano na makundi mbalimbali," amesema Zitto.

Mwenyekiti wa Chaumma, Hashimu Rungwe ametumia mkutano huo kufafanua taarifa zinazoelezwa kuwa vyama vingine vilivyojitoa havikuweka wagombea, akisema si za kweli na akashauri zipuuzwe.

"Mimi niliweka wagombea 25O ambao walitolewa wote wanaosema sikuweka wagombea muwapuze," alisema Rungwe

CHANZO: Mwananchi
Nakwenda Zimbabwe
 
Back
Top Bottom