Uchaguzi 2020 Vyama tisa vya upinzani vyatoa tamko kuhusu Uchaguzi Mkuu 2020

Uchaguzi 2020 Vyama tisa vya upinzani vyatoa tamko kuhusu Uchaguzi Mkuu 2020

Vyama tisa vya upinzani vimetoa tamko la kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 28, 2020 na mgombea wa CCM, Dkt. John Magufuli kuibuka mshindi baada ya kupata 84.4% ya kura zote.

Katika tamko lao, vyama hivyo vimempongeza mgombea huyo kwa kushinda na kusema kwamba mambo aliyoyafanya ndani ya miaka mitano iliyopita yamechangia kwa kiasi kikubwa ushindi wake.

Vyama hivyo pia vimeipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuratibu uchaguzi huo uliohusisha vyama 15.

MY TAKE:
Tamko la vyama zaidi tisa ni tamko kubwa
Hivi ni vyama vinavyomilikiwa na CCM.. havina jipya
 
Ishara zote zipo dhahiri na kwa macho zinaonekana ni ishara za maumivu kwa waliojiajiri kwa siasa za upinzani. Yote yaliyosemwa dhidi yao yanaenda kutimia kwa kasi sana.

Ni wao wenyewe ndio wanaoweza kuzuia hatma ya siku hizo chungu kama tu;

1. Watakubaliana na matokeo na kukubali kuijenga nchi yetu wakishirikiana na serikali. Watanzania wamechoshwa na maandamano yasiyo na tija huku wakijua haki ilitendeka.

2. Watajijenga katika misingi ya chama cha siasa chenye Sera na itikadi ya kueleweka badala ya kuwa wanaharakati, watetezi Wa Sera za mabeberu.

3. Watakubali na kukiri kwamba kuteleza kupo katika maisha hivyo waliteleza na wapo tayari kurudi kwenye mstari.

4. Wataondoa taswira mbaya iliyojengeka dhidi ya vyama vyao kwa watanzania watanzania wa Leo wanathibitisha kila wanachosikia na kuambiwa.

Hizo ni baadhi ya kasoro kwa baadhi ya vyama vya siasa ,kasoro hizo zisipofanyiwa kazi hakika Siku zinakuja ambazo watanzania hawatatamani kuuona wala kuusikia upinzani masikioni mwao ila kama wakizifanyia kazi inawezekana wakarudisha imani kwa watanzania iliyovunjika kwa sababu yao.
 
JPM hajachaguliwa na Watanzania kachaguliwa na NEC na TISS kwa msaada wa Jamana Printers.

Ebu tukumbushe, 2015 Magufuli alichaguliwa na nani? Wale wale waliomuchagua mwaka huo ndo wame endelea kumchagua ila wakaongezeka baada ya kuona uchapakazi wa Magufuli awamu ya kwanza - ndege, Reli, Mawasiliano, madini karudisha mikononi kwa wa Tz! Walewale waliokuwa wanasema Lowassa (aliyekuwa mpinzani mwenzao)ni fisadi ndo wanalalama. Ushaona juu ya voter suppression in Russia na nchi nyingine zilizoendelea wakati huku Tz hakuna voter suppression!
 
hivyo ni vyama vya upinzani kweli au ni utopolo tu? vyama vinajulikana kwa msajili tu,huibuka wakati wa uchaguzi tu. Hivyo vyama navyo ni mkakati wa kuua vyama vyenye upinzani wa kweli,kwa kuwa havijaathiriwa na uhuni uliofanywa vikaona ni vema vipongeze.
 
Baada ya masaa 72 Mbowe atakuwa waziri mkuu.
CHADEMA wana ndoto nzuri sana kwakweli.
 
Wewe kweli jinga. Ingekuwa na ukweli hiyo NEC wangepigia kura majumbani kwao na kuzileta vituoni kwenye mabegi na vikapu kwa nguvu ya Polisi?
Intelijensia yenu ilishindwa kuwakamata wakiwa wanaziandaa??
 
vyama vilivyounga mkono juhud.. ndo mnaviita wapinzani...
 
Yule mgombea wa kike kwa nafsi ya Urais alionyesha wazi kuwa ni mtu kutafuta kuteuliwa tu
 
Una hakika na hayo mabeg, emu acheni kuzusha vitu msivojua, trust me , huu uchaguzi mmeshindwa kihalali kabsaa! Mnajitafutia dhambi kwa hao mnaowasingizia walikuwa na mabeg!!
Kama ungejua utaratibu unaokuwapo kwenye zoezi la uchaguzi wala usingelipiga hayo makelele
Haya Sawa, mmeshinda kihalali! Upinzani wajipange 2025 kwa kuteua tume yao, wakurugenzi wa wilaya na kuchapisha karatasi za kura!
 
Wale wanavizia teuzi tu. Kuna baadhi yao wanatamani sana na kuomba wakumbukwe kama ilivyokuwa kwamama Anna Mghwira.

Wachumia Tumbo tu na hawana lolote
 
Hivi CHADEMA ina wajumbe wao Wa nyumba kumikumi?!!!

Hivi ni rahisi Kushinda uchaguzi ilihali huna WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA?!!

Hivi unashindaje uchaguzi mkuu bila ya TUME HURU?!!

Hivi si mh.Mbowe aliyewahadaa nguli wa upinzani kwa kuibadilisha GIA angani na kumchukua mh.Lowassa ule mwaka 2015?!!!

Hivi kutaka Kuheshimu katiba ya nchi hakuanzi na Kuheshimu taratibu zilizoko ndani ya vyama vya upinzani na pia katiba zao?!!!!
Sikumbuki kama mh.Mbowe alifuata taratibu za kumteua mgombea wa urais wa CHADEMA ule mwaka 2015.....

Taifa Letu....
Amani Yetu....
Mbowe amekua akitupiwa kila uchafu ambao unakua unaibuliwa na Mahasimu wake CCM kwa sababu amekua Kiongozi asieyumba, 2015 kwa mujibu wa TL aliemleta Lowasa ndani ya CHADEMA alikua Dr.slaa kupitia mawasiliano ya Gwajima. hivyo mbowe kama kiongozi wa chama alichosema ni tamko la chama halikua lake peke yake.
 
Mbowe amekua akitupiwa kila uchafu ambao unakua unaibuliwa na Mahasimu wake CCM kwa sababu amekua Kiongozi asieyumba, 2015 kwa mujibu wa TL aliemleta Lowasa ndani ya CHADEMA alikua Dr.slaa kupitia mawasiliano ya Gwajima. hivyo mbowe kama kiongozi wa chama alichosema ni tamko la chama halikua lake peke yake.
Mkuu Kama ni Mshenga Alikuwa ni Dr.Slaa,Je kilichomkimbiza na zile tuhuma zake dhidi ya Mh.Lowassa zilitokana na nini?!!!

Gwajima huyohuyo leo Yuko CCM na ni mbunge wa Kawe.....
 
Back
Top Bottom