Vyama vya siasa vya upinzani jifunzeni njia tofauti za kuomba maji ya kunywa na kupewa

Vyama vya siasa vya upinzani jifunzeni njia tofauti za kuomba maji ya kunywa na kupewa

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Unaweza kupewa glasi iliyojaa maji ya kunywa kwa njia tofauti. Unaweza kuomba au kuagiza upewe maji, unaweza kubembeleza au kufoka upatiwe maji ya kunywa ukapewa, na unaweza kuyachukuwa mwenyewe bila kuomba ukayapata. Njia zote hizi zina lengo moja tu la kupata maji glasi moja tu ukate kiu bila kujali umeyapataje maji hayo.

Siku zote na mara zote ili kuyapata maji safi na salama kwako ni kutumia mila na desturi husika za mahala hapo za namna ya kuomba maji ya kunywa. Na desturi, mila au utamaduni muhimu sana za kuzingatia zaidi ni desturi na culture ya unaemtaka akupe maji safi na salama ya kunywa.

Demokrasia yetu imefungiwa kwenye masanduku yenye makufuli na lakili za vyama tawala na watawala ambao hawana exposure kubwa za demokrasia, hata malezi na makuzi yao ndani ya familia na mashuleni hayakuruhusu demokrasia. Wazazi na walimu walitumia njia zisizokuwa za kidemokrasia katika malezi ya watoto ambao leo hii ndio viongozi wa chama na serikali. Ukweli huu ni lazima ufahamike hata wakati wa kuomba demokrasia nchini.

Hivyo, kama mtu atatumia njia na utamaduni wa Ulaya au wa sehemu nyingine kudai maji, chumvi, au demokrasia kwa watawala wa Kiafrika atahangaika sana kupata. Na wakati mwingine anaweza asipewe kabisaaa. Lazima tutumie zile njia na mbinu ambazo tulizitumia kuomba nguo mpya, chakula, nauli ya shule, kwenda kwa shangazi, au kupewa sehemu ya shamba na wazazi wetu.


Mila na Utamaduni zetu zitumike kudai katiba na tume huru ili kufupisha muda wa kuvipata, Afrika sisi hatuna utamaduni wa maandamano, matusi, na kejeli katika kufanikisha mambo yetu. Mara nyingi huwa tunatumia utamaduni wa kunyenyekea, kuheshimu, kusifu, kujikomba, kununa, kugoma, kususa, kuomba, kuiba na kusema uongo katika kufanikisha mambo yetu. Yaani "make them feel their importance" humohumo unachomekea maombi yako. kama hivi
 
Back
Top Bottom