Pre GE2025 Vyama vya Siasa vya upinzani vijikite kuwaandaa wagombea mapema kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Pre GE2025 Vyama vya Siasa vya upinzani vijikite kuwaandaa wagombea mapema kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tunapoelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 ni vyema vyama vyote vya upinzani vitakavyoshiriki vikaanza maandalizi mapema kabla giza halijazama.

Wote tunakumbuka uchafuzi uliofanyika katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 ambapo vyama vya upinzani vilipata pigo moja matata tokea kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa. Uchaguzi huo ulighubikwa na uonevu mkubwa sana wagombea wengi wa CCM walijikuta wakipita bila kupingwa kutokana na kinachodaiwa wagombea wengine wa vyama vya siasa walishindwa kujaza fomu kwa usahihi.

Tunakumbuka mwaka 2019 wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa jinsi ambavyo wagombea wa upinzani walivyoenguliwa kiubaguzi kwa kasoro ambazo hazikuwa za Kikatiba na ambazo zingeweza kusahihishwa.

Kimsingi Chaguzi za mwaka 2019 na 2020 zilirudisha nyuma mafanikio ya kuratibu chaguzi na matokeo yake.

Maandalizi yaanze mapema sana, vyama hivyo viteue wagombea wenye uwezo, kwanza wajue kusoma na kuandika. Baada ya kupata competent candidates, vyama viwajengee uwezo masuala mazima ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kujaza fomu kwa usahihi.

Ni aibu kubwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA kukuta kwenye fomu kajaza CDM badala ya CHADEMA.

Naamini wagombea wakipatikana mapema na kujengewa uwezo, basi mchakato mzima wa uchaguzi utapungua kasoro, vyama vya upinzani vitapata wawakilishi wengi Serikali za Mitaa na kuamsha ari uchaguzi mkuu 2025.

Ni hayo tu.
Mawazo yako ni mazuri sana.
 
Mimi nafikiri sio vibaya vyama vya upinzani kushiriki na kuhakiki form za wagombea wao zimejazwa vizuri na kuchukua evidence kama picha na video kwamba form zipo 100% sawa. Tamisemi ikiwakata kwa kisingizio cha hawakujaza form vizuri waweze ku-challenge hio decision kwa ushahidi tosha na itaongeza nguvu kudai tume huru kwa uchaguzi mkuu ujao.
Kwa vyombo vipi vya sheria vitakavyo wapa haki wapinzani nchi hii?
 
Mpaka Sasa Bado unahitaji hayo Ili kupata nguvu ya kudai tume huru?! Ni kipi ambacho hakipo wazi Bali ndio ushahidi utafufutwe Sasa?
Nikupoteza rasilimali fedha
 
Wagombea hawatakiwi kuondolewa katika uchaguzi kwa kujaza tu fomu vibaya. Hayo ni mambo ya hovyo sana na kuwakosesha raia haki yao ya kuchagua.
TAMISEMI ndio inatakiwa ihakikishe wagombea wote wamejaza fomu zao vizuri bila kuwaengua.
Jiwe alikuwa anawalazimisha tume kuwakataa wagombea bila sababu za msingi
 
Unaonaje wapinzani wa kweli washiriki au tusubiri miujiza ya tume huru?
Inabidi washiriki ili walau kuweka na sauti za upinzani bungeni na ktk mabaraza ya madiwani .

Ukimsusia fisi mzoga atakula mpk wanyama wazima. Kususa uchaguzi siyo option nzuri sana. Maana hata chama kinapotea masikioni mwa watu.
 
Nimeona ile video clip ya 2020,Tundu Lissu alikwenda Hai kwa shughuli za Kampeni ya Uchaguzi,halafu,apparently,anafurumushwa aondoke,vijana wa Chadema wanamfukuza.
 
Back
Top Bottom