kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Kwa namna tume ya uchaguzi, Katiba na kanuni za uchaguzi zilivyo sasa hivi itakuwa kazi bure kama vyama vya upinzani vitashiriki chaguzi bila kufanyiwa mabadiliko muhimu ya kidemokrasia, ni kweli au uongo?
Rais Samia ana exposure kubwa sana katika katika duru za kimataifa kuliko Rais yeyote yule tuliyewahi kuwa nae tangu uhuru. Kama kuna wengine ambao walikuwa na exposure kubwa kama hii walikuwa na bahati mbaya ya kumezwa na kivuli kizito cha siasa za Baba wa Taifa za chama kushika hatamu na ujamaa na kujitegemea, hivyo walishindwa kuihudumia demokrasia ya vyama vingi hata kama walikuwa na nia hiyo.
Rais Samia anafahamu kwamba adui yetu namba moja ni umaskini na sio CCM, CUF, CHADEMA wala ACT, anafahamu kuwa demokrasia ikieleweka na kushamiri vyama vya siasa vinaweza kuangushwa na kurudishwa na wapiga kura kwenye chaguzi kwa amani na furaha kama agenda zao hazitatimizwa na chama husika.
Vyama vya upinzani hebu mpeni muda Rais Samia wa kuitumikia na kuirekebisha demokrasia yetu, tumpungizie miluzi mingi itakayomtatiza njiani na kusahau kile anachowaza kuifanyania Tanzania na demokrasia yetu.
Mama Samia mdau muhimu na mnufaika namba moja wa utawala wa kidemorasia nchini, anaufahamu uzuri wa demokrasia kwakuwa yeye ni tunda halisi la demokrasia nchini.
Hebu mnielewe kwenye hili, maana imani huzaa imani na shari huzaa shari. Kazi yenu kuanzia sasa iwe ni kuviimarisha vyama vyenu hadi vitongojini tayari kwa uchaguzi wa 2030 ambao inshallah utakuwa huru na haki ili anaepata apate na anaeshindwa ashindwe bila mang'uniko ya kuipasua nchi yetu. Tukumuke sasa hivi nchi yetu haina watu kama Mwl. Nyerere, Mzee Mkapa, Mzee Karume, Mzee Maalim Seif, nk ambao walikuwa grisi yetu tunapozozana, sasa hivi grisi yetu kuu lazima iwe Katiba yetu, Tume ya Uchaguzi na kanuni za uchaguzi ( free and fair elections) baaasi.