Vyama vya upinzani mwacheni Rais Samia 2025 apite bila kupingwa ili awanyooshe mapito yenu 2030

Vyama vya upinzani mwacheni Rais Samia 2025 apite bila kupingwa ili awanyooshe mapito yenu 2030

Siku hizi mkuu unaandika vitu vya hovyo sn na wala siyo hoja kama mwanza, swali toka umeingia CCM umenufaika na nini?
mkuu weledi ni kusema "unaandika vitu ambavyo mimi sivipendi" usiseme unaandika vitu vya hovyo.
 
Tokea uhuru hujapata umeme, sidhani sababu yake fedha za nchi zilikuwa zinatumika kuandika katiba!
sababu za vijiji vyote vya kata yangu kukosa umeme na maji tangu uhuru ziko nyingi sana zikiwemo za pesa nyingi kutumika kukomboa bara la Afrika, vita ya Uganda, uchumi kugharimia na kuendesha siasa, ukwepaji kodi, ubadhilifu wa bunge la katiba ambayo haikuandikwa lakini hela zimeliwa, wizi, ubadhilifu na mikataba na miradi mibovu. Hii imesababisha Tanzania hiihii moja wengine wanafurahia uhuru na wengine wako gizani wakimulika na vijinga vya moto. Ukiwauliza watu watakwambia shida yao sio ukosefu wa demokrASI BALI UKOSEFU WA umeme, maji, vituo vya afya, barabara, shule na unyanyasaji wa polisi.

Hivyo kama wewe kijiji, kata, tarafa na wilaya yako kuna maji, umeme, zahanati, shule na barabara basi andamana leo upate Katiba mpya kesho. Kuna watu wanafuata mkumbo tu kwenye mambo haya. Ukiangalia kanda ya Kaskazini wao wana haki ya kudai demokrasia leo kwakuwa wao walishapewa jana umeme hadi kwenye migomba na mikahawa, maji, shule nyingi, masoko, zahanati na barabara zinazounganisha kata na kata. Lakini watu wanaotoka kanda za pwani, ziwa, kati na magharibi hawa hawahitaji Katiba mpya leo bali maji, umeme, shule, barabara na zahanati.

Mama Samia kasema kazi yake sasa ni kuleta ulinganifu katika upatikanaji wa umeme, maji, madarasa na shule, madawati, zahanati na barabara kwenye vijiji vyote ili sote tuwe kwenye ukurasa mmoja ili tuongee lugha moja kama nchi. Sio mwingine adai katiba kwakuwa jamii yake ina umeme, maji, shule, barabara, nk na mwingine hivyo vitu ni ndoto kwao. Hapo itakuwa anaongezewa yule aliyenacho, ambao ni upuuzi sawa na upuuzi mwingine.
 
Hatujazoea kuambiwa ukweli?
Sio hivyo, hata mkeo mwambie kile ambacho wewe hukipendi kwake, mfano, badala ya kumwambia una tabia mbaya ni bora umwambie hiyo tabia yako ya kuchelewa kurudi wewe huipendi, chumvi nyingi kwenye chakula mimi sipendi, chakula, nk. Be very specific as possible to avoid too much generalization.
 
Usinipangie
 
Naunga mkono hoja
P
Kwa nini msiache kura ziamue, wapi duniani hayo yamefanyika.
Je, Samia akisema nipeni na wabunge wote hilo bunge lijalo litakuwaje.
Kwani ikiwa ni kweli yupo vizuri kwa nini tufikiri hivi. Akili za ajabu sana. Hata ndani ya chama kungekuwa na ushindani, ni afya nzuri. leo mnasema upinzani wasisimamishe mgombea!
 
Wapinzani wamesimika wagombea kwenye chaguzi zote tangu uchaguzi wa mwaka 1995 - 2020 lakini mara zote hizo wametangazwa kushindwa uchaguzi na hakuna kwenda mahakamani kupinga kwa mujibu wa katiba yetu. Kwa katiba na tume hii ya uchaguzi iliyopo hata wakishiriki watatangazwa kushindwa tena kwa mara nyingine. Dawa pekee ya wapinzani kutangazwa wameshinda kama wameshinda ni Rais Samia kukubali tume na katiba viwe na mabadiliko muhimu. Kwakuwa Rais Samia hatakuwa mgombea mwaka 2030 ni rahisi kukubali kutengeneza Katiba na Tume ya uchaguzi ya kidemokrASIA ILI AACHE LEGACY kwenye taifa lake.

Bila kuwa na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi wapinzani wataambulia kuwatumia wananchi kama mapunda yao ya kuwabeba kuwapeleka watu wachache sana bungeni wakapate ajira binafsi ya kujijengea majumba yao ya kifahari, mahoteli yao binafsi, mastudio binafsi na magari makubwa binafsi na familia zao. Siku wakiamua wanaweza kuhama kwenda kuunga juhudi kwenye chama kingine chenye maslahi kwao binafsi.
 
Mfano , Mh. Tundu Lissu kule kwao singida kwa Sasa kwao sio zamu ya kudai Katiba mpya bali wanahitaji maji, umeme, shule nyingi, zahanati na barabara. Hii ni tofauti na Mh. Mbowe, Lema au Mnyika maana kule kwao vitu hivyo Wana ahueni kubwa sana kuliko singida
 
sababu za vijiji vyote vya kata yangu kukosa umeme na maji tangu uhuru ziko nyingi sana zikiwemo za pesa nyingi kutumika kukomboa bara la Afrika, vita ya Uganda, uchumi kugharimia na kuendesha siasa, ukwepaji kodi, ubadhilifu wa bunge la katiba ambayo haikuandikwa lakini hela zimeliwa, wizi, ubadhilifu na mikataba na miradi mibovu. Hii imesababisha Tanzania hiihii moja wengine wanafurahia uhuru na wengine wako gizani wakimulika na vijinga vya moto. Ukiwauliza watu watakwambia shida yao sio ukosefu wa demokrASI BALI UKOSEFU WA umeme, maji, vituo vya afya, barabara, shule na unyanyasaji wa polisi.

Hivyo kama wewe kijiji, kata, tarafa na wilaya yako kuna maji, umeme, zahanati, shule na barabara basi andamana leo upate Katiba mpya kesho. Kuna watu wanafuata mkumbo tu kwenye mambo haya. Ukiangalia kanda ya Kaskazini wao wana haki ya kudai demokrasia leo kwakuwa wao walishapewa jana umeme hadi kwenye migomba na mikahawa, maji, shule nyingi, masoko, zahanati na barabara zinazounganisha kata na kata. Lakini watu wanaotoka kanda za pwani, ziwa, kati na magharibi hawa hawahitaji Katiba mpya leo bali maji, umeme, shule, barabara na zahanati.

Mama Samia kasema kazi yake sasa ni kuleta ulinganifu katika upatikanaji wa umeme, maji, madarasa na shule, madawati, zahanati na barabara kwenye vijiji vyote ili sote tuwe kwenye ukurasa mmoja ili tuongee lugha moja kama nchi. Sio mwingine adai katiba kwakuwa jamii yake ina umeme, maji, shule, barabara, nk na mwingine hivyo vitu ni ndoto kwao. Hapo itakuwa anaongezewa yule aliyenacho, ambao ni upuuzi sawa na upuuzi mwingine.
Huo ulinganifu umekosekana kwasababu ya sheria mbovu tulizonazo ambapo raisi anaweza tumia rasili mali za taifa kujenga kijijini kwake viwanja vya ndege ili afike kwa urahisi! Labda utuelezee ni vipi katiba inaweza faidisha kijiji fulani na kukiwekea mguu chengine.
 
Ndio maana nikasema kwa sasa katiba mpya sio muhimu kuliko maji, umeme na zahanati kijijini kwetu. Hata Mh. Lisu ataheshimika kwao Singida kama atagombana na serikali kupeleka maji, umeme, shule na zahanati kwenye vijiji vya Singida ili vifanane kwanza na vijiji vya Kilimanjaro na mikoa mingine badala ya kupambania Katiba mpya. Katiba mpya haisambazi umeme na maji kwenye vijiji vyote ya singida. Watanzania lazima tutumie akili zetu sawasawa tusifuate mkumbo. Mimi hapa kama mtu ataniambia tuache kufanya uchaguzi wowote mwaka 2025 ili tutumie hela hizo kuwasha umeme na kusambaza maji vijiji vyote kabla ya uchaguzi wa 2030 nitamkubalia kwa mikono miwili. Mbona huko Uarabuni hakuna uchaguzi lakini maendeleo yapo?
 
CHadema chondechonde; mwachieni mama awanie uraisi na tumpe support LAKINI ktk wabunge hakuna kuibiana kura kila mmoja akapite kwa nguvu ya wapiga kura bila rushwa, wala uchafuzi wa NEC na usalama!
 
Kwa nini mnapenda sana kupita bila kupingwa? Yale Yale ya kipindi kile 2016.

Ooh huyu 2020 haitaji kupiga kampeni, Mara ooh huyu ndio tuliyemsubiri.

Watu hamna akili na hamjifunzi.

Kama mnapenda demokrasia, kubalini na ushindani. Kama ni mzuri watu watampigia kura kwa wingi. Kama ni mbovu, watamkataa
Lazima vyama vya upinzani vifanye tathimini ya kina na kuja na mbinu mbadala ya kushinda uchaaguzi badala ya kutumia mbinu zilezile ambazo hazikufua dafu tangu uchaguzi wa 1995. Mpeni heshima kubwa na muda huyu mama aitengeneze njia yenu. Huyu mama ataondoa visiki na mbigili zote kwenye njia za demokrasia yetu kama tutamuonyesha respect, hatutamtukana na kumbeza majukwaani. Huyu mama ni zao la demokrasia iliyokomaa hivyo hangependa demokrasia ichezewe na wahuni. Kama wahuni wangefanikiwa kuichezea demokrasia yetu asingekuwa Rais nakwambia. Ukimwangalia usoni huyu mama unaona kabisa ni mtu mwenye kuamini demokrasia kwa mustakabali wa nchi yetu. Hebu nendeni nae polepole na kumpa heshima yake, nae hatawaangusha, hata kidogo.

Anachotaka yeye ni chama kichaguliwe kwa mazuri yake na kishindwe kwa mabaya yake, huko ndiko anakokwenda. Anataka vyama vishindane kwa kufanya mazuri kwa wananchi kama ulaya na marekani vile.
 
Back
Top Bottom