Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kishasema hagombei
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mungu ni WA wote, anaondoa maisha na kuongeza maisha ya amtakae. Tunapanga kama vile tupo milele,Wapinzani watakubali hoja YAKO LAKINI KWA serikali mseto ijayo AMBAYO Mama Anaweza asiwe sehemu ya HIYO serikali!!2025 ni Mbali Sana kwani wewe unawasiliana na Mungu!!!???
Kuondoka nayo hakuhitaji mihemko, hata akina Nyerere kama wangedai Uhuru kwa mihemko wasingeupata haraka na wengepotea wengi.CCMni laana kwa taifa
Wahenga wanasema kama hujui unakokwenda huwezi kupotea na hata kama umepotea hujui kama umepotea. Hii tabia ya kumsifu kila Rais wa kila awamu ni dalili kuwa taifa halijui linaelekea wapi na watu hawajui pia wanaelekea wapi na walipaswa kuwa wapi. Hivyo ni vigumu kujua ni kiongozi gani anahitaji kusifiwa na yupi anastahili kuzomewa. Mfano, kama taifa tungekuwa kumekubaliana kwa pamoja tangu kupata uhuru kuwa tunataka kila mkoa uwe na vyuo vikuu 3 vya serikali ifikapo 2025 na kila wamu LAZIMA ijenge angalau vyuo vikuu 5 sisi wananchi tungeweza kumbaini ni rais yupi hakujenga vyuo 5 kwenye awamu yake ili tumsifu na yupi hakujenga hata 2 ili tumzomee.Namkumbuka hayati Benjamin Mkapa kwa kauli yake kuhusu "watu kuwa wavivu wa kufikiria"
Kila Rais mpya akitokea fikra kama hizi hujitokeza. Pale JPM alipokuwa hai, pia alipambwa kwa kauli kama hizi, na hata yakajitokeza matamanio ya kubadili katiba ili tu azidi kubakia madarakani baada ya kuhudumu kwa kipindi chake cha miaka 10.
Leo mwaka mmoja baada ya kutokuwepo kwake, unaanza unafiki kama ule ule, eti haijapata kutokea Rais kiutendaji mfano wa SSH toka tupate uhuru wa Tanganyika, ama sijui pia ulikuwa una maanisha pia na ule wa Zanzibar.
Hivi unazijua changamoto mbalimbali ambazo taifa letu ilizipitia katika vipindi tofauti vya awamu za uongozi wa taifa letu? Hivi unajua vipaumbele vya kitaifa vya kijamii na kiuchumi vilivyokuwepo, miundombinu ya nchi yetu, vyanzo vikubwa vya mapato ya nchi, miradi mikubwa ya kimkakati, deni la taifa, idadi ya rasilimali watu muhimu iliyokuwepo na vitu vingine muhimu kama hivyo, kiasi kwamba ufikie kiwango cha kutoa majisifu kama hayo?