Vyama vya upinzani mwacheni Rais Samia 2025 apite bila kupingwa ili awanyooshe mapito yenu 2030

Je atagombea ?
 

14 March 2022

LIVE: WATEMA CHECHE ZA KATIBA MPYA / HAKI ZA BINADAMU

Tundu Lissu, Helen Kijo~Bisimba, & Ananeliya Nkya | Haki na Katiba Mpya - Tanzania


Source : DarMpya TV
 
Wapinzani watakubali hoja YAKO LAKINI KWA serikali mseto ijayo AMBAYO Mama Anaweza asiwe sehemu ya HIYO serikali!!2025 ni Mbali Sana kwani wewe unawasiliana na Mungu!!!???
 
Namkumbuka hayati Benjamin Mkapa kwa kauli yake kuhusu "watu kuwa wavivu wa kufikiria"

Kila Rais mpya akitokea fikra kama hizi hujitokeza. Pale JPM alipokuwa hai, pia alipambwa kwa kauli kama hizi, na hata yakajitokeza matamanio ya kubadili katiba ili tu azidi kubakia madarakani baada ya kuhudumu kwa kipindi chake cha miaka 10.

Leo mwaka mmoja baada ya kutokuwepo kwake, unaanza unafiki kama ule ule, eti haijapata kutokea Rais kiutendaji mfano wa SSH toka tupate uhuru wa Tanganyika, ama sijui pia ulikuwa una maanisha pia na ule wa Zanzibar.

Hivi unazijua changamoto mbalimbali ambazo taifa letu ilizipitia katika vipindi tofauti vya awamu za uongozi wa taifa letu? Hivi unajua vipaumbele vya kitaifa vya kijamii na kiuchumi vilivyokuwepo, miundombinu ya nchi yetu, vyanzo vikubwa vya mapato ya nchi, miradi mikubwa ya kimkakati, deni la taifa, idadi ya rasilimali watu muhimu iliyokuwepo na vitu vingine muhimu kama hivyo, kiasi kwamba ufikie kiwango cha kutoa majisifu kama hayo?
 
Ni kweli samia anajitahidi kwa nafasi hiyo ila sio kweli kwamba anawazidi marais wote kwa exposure hiyo sio sawa.

Maana kuna mtu kama Nyerere, Mkapa na JK kwakweli wamepata exposure kubwa sana kumzidi yeye kabla ya kuwa marais.
 
Tumia basi akili yako ya kawaida. Vyama vya upinzani vilishriki chaguzi tangu 1995, 2000, 2005, 2010, 2015, na 2020 bila mafanikio. Hii ni kuonyesha kuwa CCM huwezi kuishinda kwa kutumia katiba, tume na kanuni hizi zilizopo sasa. Unahitaji Rais mwenye weledi na ufahamu mkubwa wa kuamini kuwa hata wapinzani ni watanzania pia na Tanzania ni yetu sote atakae mazingira safi ya kushinda na kushindwa chaguzi bila kuishia kwenye kususia matokeo au vurugu kama zile za Zanzibar enzi zile.

Akili yako ni sio kubwa sana kumudu kijadili mada hii, tulia TU usome michanho ya wengine
 
Nadhani ungesema tuu bila ya kutafuna maneno, unachokusudia kusema ni bora vyama vingi vifutwe kuepusha vita. Kama tatizo ni sheria mbovu na Samia ana utashi kwanini asizibadilishe tuu kuna miaka kadhaa hadi kufikia uchaguzi.
Mimi kwenye kata yetu hakuna umeme, maji, na barabara bado, hivyo Hata Mimi nisingekubali kutumike Senti hata moja kugharamia uandishi wa Katiba Sasa hivi. Focus yetu Sasa iwe ni sensa, umeme vijijini, maji kwa wote, elimu kwa wote, reli, bwawa la umeme na flyovers na mwendokasi kupunguza foleni. Mambo ya Katiba yaanze.

Tunafahamu kuwa ziko Kanda ambazo kwenye majimbo Yao Kuna umeme, maji, zahanati, shule na barabara kila Kijiji, hawa ndio wanaowaza maandamano kila dk na kila saa 1/12. Tuache nchi iwe level moja kwanza ya maendeleo ili tuongee wote lugha moja.
 
Issue kubwa hapa tunaongea kuhusu demokrasia. Mfano kwenye awamu ya kwanza, ni nani amesema Tanzania haiko huru mpaka Bara lote liwe huru wakati watanzania walipigania uhuru wao na kuupata? Nanī alishirikishwa kutoa uwamuzi wa kutumia rasilimali zetu (fedha, watu, muda na vifaa) kwenda kukombolea nchi nyingine? Huu haukua udikteta na sifa binafsi?
 
Siku hizi mkuu unaandika vitu vya hovyo sn na wala siyo hoja kama mwanza, swali toka umeingia CCM umenufaika na nini?
 
Excellent anko
 
Tokea uhuru hujapata umeme, sidhani sababu yake fedha za nchi zilikuwa zinatumika kuandika katiba!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…